Mzee wa Upako ahoji mantiki ya CCM kujifananisha na nyoka katika ngonjera ya CCM kujivua gamba

The Prophet

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
682
94
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.
 
kwakuwa CCM wamedhihirisha kwamba wao ni nyoka. tuchukue hatua madhubuti za kumuuwa nyoka huyu ili tuondokane nae. nyoka ni nyoka tuu hata akijivua gamba hawezi badilika na kuwa sii nyoka kwani sumu yake ni ile ile.
 
kuvua gamba ni lugha ya picha inayomaanisha kuanza upya kwa jambo na wala haihitaji uwe mchungaji au msomi uliebobea kuelewa nini chamaanishwa labda kama mtu anataka kupotosha makusudi.
 
Ni kweli Kujivua gamba ni lugha ya picha inayoomaanisha kuanza upya kwa jambo. Kama hivyo ndiyo basi CCM wameanza upya yale yote waliyokuwa wanayafanya kama vile ufisadi tena kwa nguvu na ari Kubwa. Kuanza Upya hakuna maana ya kubadilika. Kuvua gamba ina maana ya kuanza upya mambo yale yale uliyokuwa ukifanya. Tofauti ni Nguvu unayoongeza!
 
kwani wameshajidhihirisha wenyewe kuwa ni MAFISADI.
Hakuna haja ya kutafuta mchawi.,mchawi ni FISADI.
Na ikiwezekana tukifute kabisa hiki chama cha mafisadi.
 
kwakuwa CCM wamedhihirisha kwamba wao ni nyoka. tuchukue hatua madhubuti za kumuuwa nyoka huyu ili tuondokane nae. nyoka ni nyoka tuu hata akijivua gamba hawezi badilika na kuwa sii nyoka kwani sumu yake ni ile ile.

Umesema kweli mkuu dawa ni kukiponda kichwa cha nyoka na kukisaga saga kisha tukitenganishe na kiwiliwili maana nyoka huwa haaminiki hadi umkate kichwa ndipo utakuwa na uhakika kuwa amekufa. Baada ya kuvua gamba nyoka huyu atakuwa mkali(fisadi) kuliko mwanzo kwa hiyo dawa yake ni kumuua kabisa na kumchoma moto
 
Ni kweli Kujivua gamba ni lugha ya picha inayoomaanisha kuanza upya kwa jambo. Kama hivyo ndiyo basi CCM wameanza upya yale yote waliyokuwa wanayafanya kama vile ufisadi tena kwa nguvu na ari Kubwa. Kuanza Upya hakuna maana ya kubadilika. Kuvua gamba ina maana ya kuanza upya mambo yale yale uliyokuwa ukifanya. Tofauti ni Nguvu unayoongeza!

Bullet,
unalosema ni kweli, kwani hata nyoka mwenyewe akivua gamba si anaota gamba jipya na lisilo na tofauti na lile la kwanza, nyoka hawezi kuvua gamba akaota ngozi ya kuku, haiwezekani abadan
 
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.

Kutakuwa na maoni mengi, but this is purely wrong communication strategy. hawakufanya utafiti wa kutosha, au hawakufanya utafiti kabisa juu ya tafsili ya hiyo maneno.
 
kuvua gamba ni lugha ya picha inayomaanisha kuanza upya kwa jambo na wala haihitaji uwe mchungaji au msomi uliebobea kuelewa nini chamaanishwa labda kama mtu anataka kupotosha makusudi.

Kujivua gamba(Kuanza upya)_Tuangalie sifa za viumbe wenye tabia hii :_
KONOKONO-SNAIL...Kiumbe huyu gamba lake humsaidia kujilinda dhidi ya maadui vilevile kuzalisha vilainisho vitakavyomfanya aweze kujongea na ikitokea gamba kupasuka au kuvuliwa kabisa itampunguzia uwezo ake wa kukabiliana na mazingira na hivyo kumpunguzia uwezo wa kuishi.

KOBE-TORTOISE.....Kiumbe huyu Gamba lake humsaidia kujihifadhi,Kujilinda na maadui pia kumsaidia kutembea na ikitokea gamba lake kupasuka au kuondolewa hatakua na uwezo wa kupambana na mazingira husika na hivyo nae inaweza kumharakishia kifo.

SNAKE-NYOKA ...Kiumbe huyu hua na desturi ya kujivua gamba pale apatwapo na jeraha kubwa ilikumsaidia uponyaji wa jeraha lake kwa haraka au afikishapo umri mkubwa au pale anapo ona nguvu zake za awali zimepungua na baada ya kufanya hivyo hurudiwa na hali yake ya awali kwa maana ya Mbio zaidi,Ujanja zaidi na Sumu kali zaidi.

Swali langu ni hili _CCM inajifananisha na kiumbe gani kati ya hawa?
Kama ni KOBE au Konokono basi Imekula kwao ,

Au wao ni NYOKA :shetani:na wamedhamilia watumalize kabisa?
 
ccm = nyoka.

Mwanzo 3: 14-15
Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umefanya hayo umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke , na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa...

CCM = nyoka.

wamelaaniwa!!!
 
Kujivua gamba(Kuanza upya)_Tuangalie sifa za viumbe wenye tabia hii :_
KONOKONO-SNAIL...Kiumbe huyu gamba lake humsaidia kujilinda dhidi ya maadui vilevile kuzalisha vilainisho vitakavyomfanya aweze kujongea na ikitokea gamba kupasuka au kuvuliwa kabisa itampunguzia uwezo ake wa kukabiliana na mazingira na hivyo kumpunguzia uwezo wa kuishi.

KOBE-TORTOISE.....Kiumbe huyu Gamba lake humsaidia kujihifadhi,Kujilinda na maadui pia kumsaidia kutembea na ikitokea gamba lake kupasuka au kuondolewa hatakua na uwezo wa kupambana na mazingira husika na hivyo nae inaweza kumharakishia kifo.

SNAKE-NYOKA ...Kiumbe huyu hua na desturi ya kujivua gamba pale apatwapo na jeraha kubwa ilikumsaidia uponyaji wa jeraha lake kwa haraka au afikishapo umri mkubwa au pale anapo ona nguvu zake za awali zimepungua na baada ya kufanya hivyo hurudiwa na hali yake ya awali kwa maana ya Mbio zaidi,Ujanja zaidi na Sumu kali zaidi.

Swali langu ni hili _CCM inajifananisha na kiumbe gani kati ya hawa?
Kama ni KOBE au Konokono basi Imekula kwao ,

Au wao ni NYOKA :shetani:na wamedhamilia watumalize kabisa?

umesahau panzi na mende. nao hujivua magamba.
 
Anapima upepo kwa kubalance issues baada ya kuonekana anakipigia upatu kijani,ni ile ile design ya usanii ilyozoeleka.
 
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.

Nyoka kwa muktadha wa biblia anawakilisha shetani. Sifa yake kubwa ni uongo na ndiye aliyemdanganya Hawa kula tunda. Mimi naona aliyeshauri CCM kutumia mfano wa nyoka alikuwa sahihi na ana akili sana kwani walichofanya CCM hakitofautiani sana na hali halisi. Yaani ni waongo. Hata dhana ya kujivua gamba ni uongo tu.
 
Jamani CCM imewakosea nini? yaani nyie kila kitu kwa CCM ni kibaya? mbona watu wa JF hamna shukurani? Au ndio ule msemo wa tenda wema nenda zako wala usingoje shukurani unatimia?
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.
 
kuvua gamba ni lugha ya picha inayomaanisha kuanza upya kwa jambo na wala haihitaji uwe mchungaji au msomi uliebobea kuelewa nini chamaanishwa labda kama mtu anataka kupotosha makusudi.

Ukiwa na "small thinker" utaishia na maana hiyo uliyoitoa. Lakini ukiwa "great thinker" yumkini hutaishia hapo bali utatafakari maana pana zaidi ya CCM kutumia mfano wa nyoka kuvua gamba kuelezea hatua wanazochukua ndani ya chama. Aliyefikiria matendo ya nyoka kuelezea matendo CCM siyo mjinga.
 
ahoji pia kama kweli aliyeshauri kutumia kauli-mbiu hiyo, kama ana akili nzuri. how come CCM kujifananisha na nyoka?

source Mtanzania.

Huyo mzee wa upako na yeye avue joho aingie kwenye siasa. Mbona hakushangaa oparesheni sangara anashangaa nyoka kujivua gamba? ana lake jambo/ anatumika vibaya.
 
Back
Top Bottom