Mzee wa miaka 71 awaka! Mnataka nife bila kupata umeme?

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mzee Exavery Mgavilwa (71) maarufu kwa jina la Boy Safi ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ninga halmashauri ya Wilaya ya Njombe ameiangukia serikali akiomba kufikishiwa nishati ya umeme nyumbani kwake akidai kuwa hataki kufa bila kuona umeme ukiwaka kwenye nyumba yake.

Mzee Mgavilwa ameeleza hayo wakati akitoa kero zake kwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe Wakili Edwirn Swalle alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ambapo amesema mpaka sasa watoto wake wamekuwa wakihangaika bila mafanikio.

"Hatuna umeme kabisa, vijana wangu wamekuwa wakijaribu kupiga kelele na diwani lakini na yeye anajitetea anasema sio mimi, mnataka nife bila kupata umeme? Swalle nilikuchagua mwenyewe", amesema mzee Mgavilwa

wampelekee umeme mze wa no reforms no election
 
Back
Top Bottom