Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Timothy Apiyo ni mmoja wa viongozi nchini ambaye amefanya kazi wakati wa utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Andaiwa kuwa mmoja wa viongozi machachari waandamizi waliokuwapo katika serikali hiyo ambayo Waziri Mkuu wake alikuwa ni Hayati, Edward Moringe Sokine.
Alishika nyadhifa za Ukatibu Mkuu katika wizara mbalimbali na kutokana na uhodari na uchapaji wake kazi baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Ikulu), wadhifa ambao kwa sasa unajulikana kama Katibu Mkuu Kiongozi.
Apiyo, alizaliwa katika wilaya ya Rorya, Tarafa ya Suba, mkoa wa Mara, na alipata elimu yake ya msingi na sekondari wilayani hapo na mwaka 1959 nilijiunga na Chuo Kikuu cha East Afrika Makerere Uganda ambako alichukua digrii ya kilimo na baada ya kuhitimu alipangiwa kufanyakazi katika Chuo cha Kilimo cha Ukiliguru.
Mwaka 1960 alipata uhamisho kwenda wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kuwa Bwana Shamba wa Wilaya na mwishoni mwa mwaka huo alihamishwa tena kwenda Wilaya ya Ifakara mkoani Morogoro ambako alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga.
Agosti 1962 alipata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani katika Chuo Kikuu cha West Virginia ambako alichuwa digrii ya pili ya Sayansi ya Kilimo na kutunukiwa cheti mwaka 1963.
Mwaka 1964 alipangiwa kufanyakazi Wizara ya Kilimo na baadaye alipelekwa Shinyanga kuwa Ofisa Kilimo wa Mkoa na Desemba 1965 na kisha kwenda mkoa wa West Lake (Sasa Bukoba) na mwaka 1967 alihamishiwa wizarani akiwa Afisa Mipango Mwandamizi. Mwaka 1968 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango Kilimo katika Wizara ya Kilimo na mwaka uliofuata 1969 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nyumba, Ardhi na Maendeleo Mijini.
Novemba 1969 alirudishwa tena Wizara ya Kilimo kuwa Katibu Mkuu na Aprili 1972 alihamishwa na kwenda kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda na Aprili 1974 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Julai 1986 alistaafu kazi.
Alikuwa na cheo gani huyo mzee?
Duh! Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu. Utawala wa Rais wa Kwanza Mwl. Julius Kambarage Nyerere (RIP)
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.Last time nilisikia huyu mzee analalamika kutelekezwa na serikali
maisha yalikuwa magumu mno kwake...
Alikuwa na cheo gani huyo mzee?
asante kwa tarifa ila nimeshtuka maana macho na masikio dunia nzima sasa yapo africa ya kusini,
Last time nilisikia huyu mzee analalamika kutelekezwa na serikali
maisha yalikuwa magumu mno kwake...
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.
Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.
The Boss, hicho ni kipindi cha nyuma sana. Serikali miaka mingi imempatia gari na msaidizi wa kudumu na kumsaidia katika matibabu. Hata gharama za matibabu ni serikali imekuwa ikimpatia. Last year or so alipewa gari nyingine mpya Discovery 4.
Kama mapungufu yapo ni ya kawaida.
Ndugu zangu
Mzee Timoth Apiyo amefariki dunia usiku wa jana akiwa katika matibabu South Africa katika Hospitali ya Mill Park South Africa.
Serikali ikishirikiana kwa karibu na ubalozi wetu South Africa unafanya mipango ya kusafirisha mwili kuuleta Tanzania.
Msiba upo nyumbani kwake Sitaki Shari.
Poleni sana wafiwa; Clay; Slyvia pamoja na wanafamilia wote.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
Rest in Peace Mzee Apiyo. You lived your life kwa uadilifu wa juu.
Afadhali Nafasi imepatikana kwa maana vyumba siku hizi shida sana Dar, watu wakipungua wengine tunapata nafasi ya chumba!
Afadhali Nafasi imepatikana kwa maana vyumba siku hizi shida sana Dar, watu wakipungua wengine tunapata nafasi ya chumba!
Kabla ya kuchangia fuatilia historia ya mtu kuliko kukurupuka. T. Apiyo alikuwa katibu mkuu kipindi cha JK Nyerere na alishastaafu na alikuwa anaishi katika nyumba yake. Ambayo alishindwa hata kuimalizia vizuri pamoja na kuwa alikuwa katibu mkuu kwa kipindi cha miaka kibao. Lakini kutokana na uadilifu wako hakuweza kuvuta hata senti.