Ngojeni ni wape ushuhuda hapa na tumaini wengine mtaniunga mkono au wenyel aptop wanaweza kuangalia kile kipindi.
Katika msiba ADAM KUAMBIANA.
Kwa wale mlioangalia kipindi Cha Zamaradi Mketema wa Clouds TV.
Alionyesha kipande ambacho JB alilia mpaka akashindwa kusimama(sijui kama ni kweli ila naona alikuwa anaigiza )
Sasa mie nikajua kweli anauchungu sana,sasa jioni yake ya usiku ule Zamaradi alimualika JB katika kipindi cha Take One,sasa ikawekwa Clips ya Steve Nyerere alipokuwa anahutubia huku akilia,sasa bahati mbaya mtu wa Camera wa Studio alikata clips akarejesha Studio na kwa mshangao mkuba JB na mwezie walikuwa wanacheka,kisha wakapoteza,ikabidi Zamaradi akapotezea nakusema ahh unajua sio mambo ya kucheka Steve anaogea kama vile Nyerere.
Sasa pale ndio nilipopata picha,yaani imewekwa clips ya mwezio anaongea hadi analia na wewe unacheka,halafu wewe huyo huyo mchana wake ulijifanya unalia hadi unaishiwa nguvu kwenye msiba on the same day ya mahojiano.
Hawa Jamaa kazi kweli kweli,yaani mie siwafagilii kabisaa,mwanzo walikuwa wanawalaumu wasanii wa Bongofleva kwamba wanawatenga wakati wao kwa wao wanga,hawasaidiani mpaka litokee,na mbaya zaidi hao wasanii ndio ambao waliokuwa wanawashirikisha na kuwalipa pesa kidgooo na wao kula neema.Ila kwenye Maradhi kila mmoja mbio.
Na CD zenu tuta zi BAN huku mpaka mshike adabu,xhsj type