Mzee Punch - "The incognito"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Punch - "The incognito"!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by under_score, Jan 15, 2012.

 1. under_score

  under_score Senior Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari za jumapili Wakuu?

  Nakumbuka ingekuwa nimalize masomo yangu ya shahada ya kwanza (B.com) pale chuo kikuu cha Darisalama mnamo miaka ya late 90's hivi, yaani almost 15 years back, lakini sasa ilinibidi nikache zangu "UD" tu nrudi kijijini kwetu ibiri nikalime tumbaku!

  Sasa mnajua ilikuwaje wana ? Leo hii, yaani usiku wa jana kuamkia leo, nimeota marudio ya picha moja flani hivi la ukweli, ambalo imebidi nkutupieni hapa jamvini tu ili nipate ku'share na ma'experiences yenu kama vipi!

  Ilikua namna hii: Nakumbuka siku moja niko na mshkaji wangu wa kitambo iyo (R.I.P my friend) tunakatiza zetu Academic Bridge (sijui lile daraja linaitwaje siku hizi) kitu ngoma 9 hivi za usiku ka kawaida tunatoka zetu kupiga "msuli" kuelekea mabwenini kulala, enzi hizo nakumbuka mi nlikua nalala Hall-5 ghorofa ya 11 (siku hizi naskia Hall-5 ni la wanawake tupu, sa sjui ni kweli?) afu mshkaji wangu ye alikuwa Hall 2 ghorofa ya 8 hivi kama sikosei!

  Sasa wana picha lilianza kunoga tulipofika pale maeneo ya Rev. Square (siku hizi sijui patakua panaitwaje), kwa pembeni yake hivi kulia palikuwa na Cafeteria enzi hizo (sa sijui kama pashageuzwa ni darasa labda siku hizi) tukakuta ma "black-ninjas", mtu kama 7 hivi zimetengeneza kitu kama pyramid kuelekea juu kwenye roof ya hilo jengo la Cafeteria, ambapo kimsingi ndo ilikuwaga "Billboard" ya machapisho ya Mzee Punch wa enzi hizo!

  Mwanangu asikwambie mtu, kwa ile namna jamaa walivosambaratika kwa kasi ya ajabu kutoka pale mahali spati picha lake, manake mi nliona chenga tu, na kilichofuatia ni kwamba na sisi tuligawana njia tukala zetu kona mbaya kabisa kila mtu na njia yake kachala nlijikuta niko Mabibo hostel, na msela wangu akaibukia from Mwenge hostel iyo asubuhi yake, make duh!! enzi hizo hata simu za mikononi ilikuwa hakunaga mwana!

  Sasa niulize mwisho picha lilikuwaje, ile kufika tu Mabibo hostel kwenye room ya mshkaji wangu mngine ili nimgongee nipate japo hifadhi kwa masaa yale machache ya usiku yaliyobakia nakutana na ile "chata" ya danger (fuvu la kichwa cha mtu + ile mifupa miwili iliyopigwa cross kwa nyuma yake) imebandikwa mlangoni kwa jamaa, with words in RED: Mzee Punch is every where; Mzee Punch is incognito; when you see Mzee Punch you see Death, etc etc etc!

  Na sasa kitu ilonchanganya zaidi ni kwamba picha lilikuwa ni hilo hilo na kwa yule mchizi wangu alokimbilia Mwenge hostel alipofika kutaka kugonga mlango wa room ya jamaa, sasa swali huwa najiuliza mpaka kesho, who was that "Mzee" for real, ni kundi la wale maninja tulowaona, ama wale ni manyoka tu wa "Mzee", ama huyo Mzee alikuwa ni jini, ni Shetani ama li kitu'kitu gani haswa!! Kwanza alijuaje in-advance kwamba ni wapi tunakimbilia for us to find the warning remarks waiting for us, kila mmoja kwa wakati wake na kwa mahali alipokimbilia katika ile hali ya kuchanganyikiwa ....
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  yadi yadi yadi

  kwa kumbu kumbu yangu, mabibo hostel zimeanza miaka ya 2000.
   
 3. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mi mwenyewe nimeshangaa, jamaa kasimuliwa habari za "Mzee" basi kaamua kutunga story zake za uongo. Mi nimeondoka UD 1999 and that time we had no Mabibo wala Mwenge Hosteli.
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  Hujui hata kudanganya
   
 5. ndegeulaya

  ndegeulaya Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Teh teh! JF bwana kunakuwaga na raha kweli; sometimes I wonder if all members in JF are Great Thinkers for real ...! Kama huwezi kusoma si uangalie hata picha tu Mkuu ? Ama bado kuna JF Great Thinker unajiuliza nna maana gani nitoe na jibu ...!
   
 6. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mzee Punch wa ukweli alikuwa UDSM miaka ya sabini na themanini,kwenye 90's alijiishia maana alivuka mipaka akamtusi mzee Mwinyi ikabidi ashughulikiwe perpendiculary na ndo ukawa mwisho wake.
  Kwa waliosoma chuo kikuu enzi hizo watakiri 'mzee'alikuwa tishio.Freshers mkiingia tu kesho yake mnakuta bandiko juu ya mesi ya 'manzese'(zilikuwa mesi tatu 'harvard','manzese' na 'shimoni',shimoni ilikuwa spesho kwa mainjinia),utakuta bandiko limeandikwa 'ten commandments za mzee punch',hapo fresher utapewa do's na don'ts,mfano wasichana vimini marufuku,wavulana freshers marufuku kula 'harvard'hususani meza ya kwanza kushoto ukiingia,marufuku wasichana kuwa na mabwana wa mjini'wabenz' etc.
  Usiombee kupanchiwa ,utatamani ujitumbukize mto kagera,maskini nawakumbuka wahanga wa mzee Punch kama 'naked runner',murderous moll',abatekaya','the giraffe' etc yaani mzee akikupunch sharti akupe na jina.Mi naona warithi wa mzee punch ni haya magazeti ya udaku ya kina kiu na ijumaa.
  Those days,chuo kilikuwa chuo hasa na serikali ilikuwa ina invest a lot katika elimu kuanzia praimari hadi uni,leo hii mmmhhh!!!
   
 7. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Duh! mwaga data mkuu Bishanga, kwa maana hiyo basi "Mzee" alikuwa anakula mess ya Havard, meza ya kwanza kushoto ukiingia, kwa mujibu wa Commandments zake, sivyo? Na mbona nasikia Mzee Punch alikuwa anajiita "incognito", yaani kwa maana ingine hawezi kutambulika ama siyo maana yake hiyo mkuu??
   
 8. b

  blue eyez Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nakumbuka kaka yangu aliwahi kupanchiwa miaka ile ya 98 mimi nikiwa mwaka wa pili Sheria yeye mwaka wa tatu akapewa jina la "toto la majanini" roho yangu ilinumia sana!
   
 9. ndegeulaya

  ndegeulaya Member

  #9
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! Hiyo Part 2 yake ya 'basheija' hapo juu nadhani yenyewe sio ya JF Chit-Chat, wacha tusubirie Part 3 yake sasa!!
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mi naona punch kalikuwa ni kagenge ka mafioso flan hivi,na kwa kuwa kum punch mtu ilikuwa ina involve investment in terms of manilla paper,marker pens na gundi na kwa kuwa wanafunzi tulikuwa malofa ina maana genge hili lilikuwa na watu wa mjini(labda ma ex punch) waliokuwa wanawekeza kwenye uharamia huu.
  ila nikiri hawa jamaa walikuwa wanajua ung'eng'e,maana ukisikia mzee punch anaanza...'mzee warns....'ujue kazi ipo. wakati huo utamsikia anamtukana msichana na kusema....'mzee wonders if her department two was not tempered with'....'tafsiri mwenyewe hapo.
  hiyo meza ya harvard bana mi naona wengi wakaaji walikuja ni jamaa wa 4th year engineering maana wao walikuwa wanasoma miaka mingi kuliko wote main campus(muhimbili mitano).
   
 11. RR

  RR JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160

  Mnakatisha tamaa watunzi under-ground....lol
   
 12. mwakichi

  mwakichi JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Daah! shukrani sana mkuu Bishanga kwa kunijuza tales za Mzee Punch, ujue vijana wengi sisi tuliosoma enzi hizi za JK wengi wetu hatukuwahi kabisa ku'experience machapisho ya MzeePunch, by the way hii mambo ya Mzee ilikuwa ni hapo UDSM tu au mpaka na vyuo vingine kama IFM n.k ?
   
 13. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hueleweki!!
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  kipindi kile Tanzania ina chuo kikuu kimoja tu (UDSM) kikiwa na campus tatu mlimani(main),morogoro (kilimo,siku hizi SUA) na muhimbili(udaktari,siku hizi Muhas).Kote huko mzee Punch alikuwa anatamba though main campus ndo yalikuwa makazi yake zaidi.IFM ,cbe vilikuwa vinaandaa watu wa kuja kuchukua Bcomm baadae mlimani au kufanya CPA,mzee Punch alikuwa harushi makombora huko.Kipindi hicho mlimani chumba tunalala watu wawili wawili tu,imagine Hall six mchumba ule ulivyokuwa mkubwa.Kuna kitu kilikuwa kinaitwa kupigwa exile,yaani mate wako analeta mwanamke(au mwanamke analeta mwanaume hall three) na wewe unakwenda kulala
  hukooooo!!!!
  naamini humu jf kutakuwa na mamemba ambao washawahi kuwa ma Punch.Waje hapa watujuze kwa nini walikuwa wanadhalilisha wenzao.
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  aseme kabisa ni mtunzi, sio atuhakikishie ni ukweli

   
 16. ndegeulaya

  ndegeulaya Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ungejifikirisha kidogo at least kujua hilo bandiko mchapishaji kaliweka jukwaa gani nadhani usingepata shida sana kuelewa kama wewe kweli ni Great thinker mkuu!
   
 17. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  Kumbe SUA nayo ilikuwa part ya UDSM,kweli UDSM ni baba lao.
   
 18. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Upupu!!!!
  Kalale!
   
 19. under_score

  under_score Senior Member

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ha ha! ndegeulaya umenifurahisha kweli kwa hiyo post yako ya mwisho hapo juu, ama kweli wewe ni mmoja wa ma Great thinkers humu ndani, heshima mbele mkuu!
   
 20. b

  blue eyez Member

  #20
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu, hata mimi sasa naanza pata wasiwasi na watu fulani wa humu JF kwa kutokana na kile kiingereza chao chenye maneno magumu magumu mithili ya yale ya Mzee Punch wa enzi izo!
   
Loading...