Brother, kwa swali hilo, una ngozi nene ya kupokea maswali?Kwahiyo mzee Mwinyi alikuta hazina iko empty?
Ama kwa hakika ufisadi ulianza kitambo.....kwani Mtei alistaafu lini pale BoT?!!
Hahahaa.......!Brother, kwa swali hilo, una ngozi nene ya kupokea maswali?
Kosa ni kutajwa Nyerere kama mshauri kwenda kuomba?Kumbe uomba omba haukuwa bahati mbaya ni maagizo!
Makubwa haya.
Kuomba siyo dhambi.... Waswahili wanaomba hadi chumvi!Kumbe uomba omba haukuwa bahati mbaya ni maagizo!
Makubwa haya.
Viongozi Africa maajabu hayawezi kuisha, Mugabe ana pesa ya kuisaidia Tz? Au ni iliyokuwa Serikali ya Zimbabwe!
Kila misaada inayotolewa na Nchi za Africa inaenda kwa Majina ya Viongozi badala ya Nchi.
Tabia mbovu kweli hii.. Hasa kwa Tanzania sasa imeshamiri.
Samani?? Imekuwaje meza au kiti?Anasahau kuwa wakati huo Mugabe alikua anatumia pesa za Mabeberu wakiokua wamemkabidhi Nchi . Wakati huo Mugabe alikua na muda wa miaka 4 tu madarakani ,na uchumi wa Zimbabwe ulikua imara sana na haikua ni Juhudi zake Huyo Hayati Mugabe kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Mugabe Aliikuta Zimbabwe ikiwa na uchumi Mzuri sana ,akawa anachota mapesa na kufanya mambo ya Hovyo mpaka Leo ameiacha nchi hiyo ikiwa na pesa yenye samani sawa karatasi za kuchorea kama sio pampers.
Hata hivyo tunamshukuru kwa jambo hilo zuri kwa nchi yetu japo sisi tulitoa wapiganaji wetu kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo na wakapoteza maisha yao ambayo yanathamani kubwa kuliko kitu chochote.
Nina uhakika kwa asilimia mia kuwa Mugabe hakuwahi kuisaidia Tanzania hata senti tano. Mugabe kama Mugabe hakuwa na uwezo wowote wa kifedha kusaidia Tanzania. Mzee Mwinyi samahani sana, usidhalilishe taifa letu. Mtu hawezi kuisaidia nchi. Yeye kuidhinisha kutoa msaada wowote ni nchi imetoa na siyo mtu (Mugabe) katia mfukoni make, la hasha.
Hata USAID wanakuandikia kabisa ni msaada wa watu wa Marekani, lakini umeshindwa kuelewa hilo Mzee wangu? Pole sana mzee, mimi nakupinga japo sijawahi kuwa rais wa nchi. Tumia lugha stahiki, angalau basi sema serikali ya Zimbabwe iliamua kutusaidia, lakini siyo mtu aliyetusaidia. Mtu ananufaika na nchi, kamwe hawezi kuisaidia nchi. Na akipata mamlaka hufanya kwa niaba ya nchi na wananchi wote.