Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

Heshima sana wanajamvi,

Mzee Ruksa katika kitabu chake amekiri wazi Mchg Mtikila aliisumbua sana Serekali yake ya awamu ya pili.

Binafsi nakumbuka Mchg Mtikila akimwaga nondo zake wakati huo zilikuwa moto Mahakamani na nje ya Mahakama.

Pamoja na usumbufu wote Mchg Mtikila hakupigwa risasi wala kufuatwa fuatwa na wasiojulikana kwa minajili ya kusitisha uhai wake.

Mungu amzidishie maisha marefu Mzee Ruksa.

Wapo viongozi waliofuatwa usipomsifu uhai wako unakuwa mashakani, wale wote waliojaribu kumkosoa au kuonyesha mapungufu yake walikula risasi mchana kweupe au walipotezwa.
Mungu amwongezee adhabu kali ikiwemo moto wa milele mwanadamu yoyote anayepanga kutoa uhai wa mwanadamu mwenzake kwasababu za kisiasa na umaarufu wa kijinga.
Licha ya kuawa na wasiojulikana Mch Mtikila hakuwahi kusaliti nchi yake kama Lisu kwa Acacia.
 
Mtikila alianzisha hoja za serikali ya Tanganyika..
Lengo ilikuwa kumdhoofisha Mwinyi..

Kina Njelu kasaka wakaikubali..

Malecela alivyokuwa PM pengine Kwa tamaa ya madaraka akaikubali
Pengine aliona Mwinyi atarudi Zenji..yeye ata take over..

Leo tunagundua kumbe Mwinyi ni Mtanganyika...

Nyerere wakati anavunja G 55 alisema kuna watu hawataki Muungano Kwa sababu ya Wazanzibari wengi ni waislam..

Je bara hakuna waislam?

Nyerere ndo akamkomalia Malecela ajiuzulu na Kolimba ..

Leo hakuna anaejua ingekuwaje
 
Huwa nachekaga nikisikia mtu anasema Magufuli alikuwa dikteta uchwara aisee Magufuli alikuwa ni dikteta kamili na Kama angeendelea mpaka 2025 wote tungekubaliana na hili.
Sio kuwa wote tungekubaliana na hilo la kuwa Magufuli alikuwa Dikteta bali wengi tungekuwa hatupo maana angetuua.
Fikiria miaka mitano tuu kisha kuwa fyekafyeka maisha ya watu jee 7 au 8 sii angekuwa nunda kabisa!
Mungu ashukuriwe kwa kuyaona maafa haya ya Watanzania na kutupigania maana dalili zinaonyesha tulisha shindwa kujitetea kama kuku bandani na uchaguzi wa kitoweo
 
Umefikiri mbali sana.
 
Huwa nachekaga nikisikia mtu anasema Magufuli alikuwa dikteta uchwara aisee Magufuli alikuwa ni dikteta kamili na Kama angeendelea mpaka 2025 wote tungekubaliana na hili.
Mkuu alikuwa bado kufikia level ya dikteta kamili. Aise Kuna watu walikuwa waovu walipokuwa madarakani, mfno; Bokassa, Idd Amin. Enzi za utawala wa Amini, alifuta Bunge, badala yake akawa na Baraza la kijeshi lililoamua hatma ya Jambo. Brigedia Isack Maliyamungu au Isack Lugola, alikuwa mtu wa kutisha sana, ambaye kwa mjibu wa maandishi yaliyopo, alikuwa anaua hovyo hovyo watu.
 
Mungu amwongezee adhabu kali ikiwemo moto wa milele mwanadamu yoyote anayepanga kutoa uhai wa mwanadamu mwenzake kwasababu za kisiasa na umaarufu wa kijinga.
Nina mpango wa kwenda kukojolea kqburi lake hivi karibuni.
 
Heshima sana wanajamvi,

Mzee Ruksa katika kitabu chake amekiri wazi Mchg Mtikila aliisumbua sana Serekali yake ya awamu ya pili.

Binafsi nakumbuka Mchg Mtikila akimwaga nondo zake wakati huo zilikuwa moto Mahakamani na nje ya Mahakama.

Pamoja na usumbufu wote Mchg Mtikila hakupigwa risasi wala kufuatwa fuatwa na wasiojulikana kwa minajili ya kusitisha uhai wake.

Mungu amzidishie maisha marefu Mzee Ruksa.

Wapo viongozi waliofuatwa usipomsifu uhai wako unakuwa mashakani, wale wote waliojaribu kumkosoa au kuonyesha mapungufu yake walikula risasi mchana kweupe au walipotezwa.
Mungu amwongezee adhabu kali ikiwemo moto wa milele mwanadamu yoyote anayepanga kutoa uhai wa mwanadamu mwenzake kwasababu za kisiasa na umaarufu wa kijinga.
Hujui wewe nyamaza. Hujui mara ngapi amekoswa koswa kuuawa kwa sumu. Haya mambo muwe mnanyamaza nyie watoto wa 2000s Mtikila ungemuuliza angekuwa hbr tofauti na haya uyasemayo. Unamfaham Stan Katabalo? Unafahamu aliuawa vipi kwa issue ya kufuatilia Loliondo Gate? Muwe mnatuuliza sisi tuwaambie.
 
Mtikila alikuwa mchochezi aliye tumwa akatumika vilivyo.
Tabia kama hizo zisijirudie ktk tawala za sasa na zijazo.

kamwe asivumiliwe mtu au kikundi cha watu wenye nia ya kutugawa kwa misingi ya kiimani, rangi au kikabila.

Yunajifumza kuyoka ktk kitabu chake kuwa;

unaweza kuwa kiongozi mwadilifu lkn bado uadilifu wako ukachafuliwa kwa maksudi na watu wabaya na ukaonekana hufai mbele ya jamii, na kinyume chake kwa hila na hadaa viongozi wasio waadilifu wakaonekana kuwa waadilifu.
 
Angefanyaje? Angelivunja bunge??
Nakwanini asingelivunja?
Kinachowasumbua nikwamba akivunja bunge nae yumo ndio shida. Ingekua wanauwezo wa kuvunja bunge wao wakasalia madarakani ingekua mchezo wa viongozi wa Afrika.
Baraza la mawaziri lenyewe linawashinda kuvunja,itakua bunge?

Basata na Bashungwa haviguswi sasa tunaanzaje kufikiria vitu kama bunge?
Hapana chezea mwafrika
 
Ndio wale wale wasiojua demokrasia na kulewa madaraka, na kutokuwa na weledi katika uongozi wa juu.
Huyu mzee, tushukuru tu Mungu Nyerere alikuwepo. Angeweza kukaa madarakani mpaka kufa.

Hana anachokiamini.
 
Back
Top Bottom