Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

Mkuu alikuwa bado kufikia level ya dikteta kamili. Aise Kuna watu walikuwa waovu walipokuwa madarakani, mfno; Bokassa, Idd Amin. Enzi za utawala wa Amini, alifuta Bunge, badala yake akawa na Baraza la kijeshi lililoamua hatma ya Jambo. Brigedia Isack Maliyamungu au Isack Lugola, alikuwa mtu wa kutisha sana, ambaye kwa mjibu wa maandishi yaliyopo, alikuwa anaua hovyo hovyo watu.
Where is mali ya mungu now
 
Hahaha alimuuliza malecera,moja jumlisha moja ni ngapi?akajibiwa mbili,akamwambia sasa wewe hiyo serikali tatu unazitoa wapi?
Malecela naye alikuwa mweupe kichwani, ilipaswa naye ambandike swali, simenti ukichanganya na maji unapata nini? Najua kichwa maji nyerere angejibu unapata tofali, so naye angemuuliza mbona haijawa majisimenti? Kifupi swali la nyerere halikuwa na logic kabisa.
 
Rais Mwinyi anasema alijutia namna alivyoliachia bunge hadi likafikia hatua ya kupiga kura na kuwaunga mkono kundi la wabunge waliojulikana kama G55 waliodai Serikali ya Tanganyika.

Lakini hatimaye jambo hili lilienda kukwamishwa na vikao vikuu vya CCM na kutupiliwa mbali.

Kadhalika Mwinyi anaukumbuka ubaguzi uliojitokeza wakati wa uongozi wake wengine wakijiita wazawa na wengine wakidhihakiwa kuwa " maghabachori"

Hali hii ilipelekea serikali kumpa ulinzi mfanyabiashara Reginald Mengi.

Mzee Mwinyi anamtaja mchungaji Christopher Mtikila kama mwanasiasa wa upinzani aliyeisumbua sana Serikali yake.

Mungu Ibariki Tanzania.
Na hii hii tanganyika iliondoka nae asubuhi na mapema kwenye ajali ambao eri mtu kafa yeye tuu na tai yake shingoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtikila alikuwa na Mengi mazuri ila alikuwa na harufu ya Ubaguzi (kitu ambacho kikishaingia katika jamii kutoka ni kazi sana)..., Huyu ndio alileta mambo ya wazawa na wangambachori (Karne ya sasa kuleta usisi na uwao) ni fikra duni...
 
Back
Top Bottom