Mzee Mwinyi: Nilijilaumu kwa kuliachia Bunge hadi likapitisha hoja ya Serikali ya Tanganyika, Mtikila aliisumbua Serikali yangu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,480
141,194
Rais Mwinyi anasema alijutia namna alivyoliachia bunge hadi likafikia hatua ya kupiga kura na kuwaunga mkono kundi la wabunge waliojulikana kama G55 waliodai Serikali ya Tanganyika.

Lakini hatimaye jambo hili lilienda kukwamishwa na vikao vikuu vya CCM na kutupiliwa mbali.

Kadhalika Mwinyi anaukumbuka ubaguzi uliojitokeza wakati wa uongozi wake wengine wakijiita wazawa na wengine wakidhihakiwa kuwa " maghabachori"

Hali hii ilipelekea serikali kumpa ulinzi mfanyabiashara Reginald Mengi.

Mzee Mwinyi anamtaja mchungaji Christopher Mtikila kama mwanasiasa wa upinzani aliyeisumbua sana Serikali yake.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Heshima sana wanajamvi,

Mzee Ruksa katika kitabu chake amekiri wazi Mchg Mtikila aliisumbua sana Serekali yake ya awamu ya pili.

Binafsi nakumbuka Mchg Mtikila akimwaga nondo zake wakati huo zilikuwa moto Mahakamani na nje ya Mahakama.

Pamoja na usumbufu wote Mchg Mtikila hakupigwa risasi wala kufuatwa fuatwa na wasiojulikana kwa minajili ya kusitisha uhai wake.

Mungu amzidishie maisha marefu Mzee Ruksa.

Wapo viongozi waliofuatwa usipomsifu uhai wako unakuwa mashakani, wale wote waliojaribu kumkosoa au kuonyesha mapungufu yake walikula risasi mchana kweupe au walipotezwa.
Mungu amwongezee adhabu kali ikiwemo moto wa milele mwanadamu yoyote anayepanga kutoa uhai wa mwanadamu mwenzake kwasababu za kisiasa na umaarufu wa kijinga.
 
Sawa.
 
Back
Top Bottom