kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,916
- 17,329
Tumefanya bahati kumpata Rais Magufuli anayefahamu makosa tuliyofanya waafrika baada ya kupata uhuru miaka ya 1960s, miongoni mwa viongozi waliotufikisha hapa tulipo Mzee Mwinyi alikuwa miongoni mwao. Wako wengi tunaokunwa na utendaji wa Rais JPM lakini tuko kimya kwakuwa tunadhani hivyo ndivyo Rais wa watu anavyopaswa kuwa, lakini Mzee wetu Mwinyi ameona kumsifu JPM kimyakimya haitoshi.
Mzee Mwinyi alipata fursa ya kuyafanya haya anayoyafanya Rais JPM tena na zaidi kama angetaka kufanya hivyo. Watu wanashangaa kwanini sasa anakunwa, tena hadharani na hiki anachokifanya Rais wetu JPM. Kwa faida ya watanzania, taifa na Afrika kwa ujumla angepaswa atuambie ni kitu gani kiliwanyima viongozi wa afrika akiwepo yeye kufanya hiki anachokifanya Rais Magufuli leo kwenye awamu zao?
Hata sasa hivi nadhani Rais Magufuli kwakutumia usomi, uzoefu na weledi wake anafahamu ni kwanini Mzee Mwinyi anamsifu sana hivi, tena hadharani.
Watu wengi wanadhani uchaguzi wa Zanzibar 2020 pia unahusika.
Ni maoni yangu tu kama mtanzania wa kawaida kwenye nchi yake.