Mzee Mwinyi anataka nini kwa Rais Magufuli?

Mzee Mwinyi anataka nini kwa Rais Magufuli?

Anamfanyia JPM masaji ya mgongo kulinda uwaziri wa mwanae, the lousiest minister in the past 20 years.
 
Kura yangu kwa Professor,haya mambo ya kusafiria nyota za wazazi hatuyataki,alianza wa karume kaka na mdogo wote wakiutaka uraisi na sasa huyu
fanya kazi wewee acha porojo kura yako nini wakati mnapitaga kwa tume.

Kafanye kazi huko
 
Wewe pale ukiwa unamsifia hasa Mkeo / Demu wako wakati Sisi tunamjua kabisa kuwa ni ' mbaya ' huwa unataka nini Kwetu? Tuanzie hapa Kwanza tafadhali.
Kila mtu ana mtazamo wake na sababu zake, huwezi kulazimisha watu wote waone kama unavyoona wewe, kabila na kanda yako. ndio maana Rais Mstaafu Ali Mwinyi haoni taabu ku- admire waziwazi mchana kweupe, bila shaka na yeye ana mtizamo na sababu zake za msingi. Tuache kila mtu aone mwenyewe anachotaka kuona ili misingi ya demokrasia itimie.
 
Hata huku Bara mwaka 2015 ' Mapopoma ' wengi walijua ni ama Lowassa au Membe lakini ikawaje Mkuu? Nasubiri jibu lako!
Huenda mzee anataka kuzuia mambo kama hayo yasitokee 2020 tena
 
Kijana 2020 Mama Samia anapewa Zanzibar! Mwinyi upepo wake mbaya kule& Mbarawa mpemba now n zamu ya muunguja!
Hussein Mwinyi anaijua zaidi Tanganyika (Tz Bara) kuliko Zanzibar (Tz Visiwani). Hivyo anafaa zaidi Bara 2025 bila kipingamizi, maana yuko vizuri sana na ana exposure kubwa ya uongozi..
 
Angesifiwa na JK au BWM ningeamimini kwamba kuna jamba ila huyu kasha kua outdated miaka 93 sio mchezo
Ni outdated mkuu. Nakumbusha tu kwamba Mzee Mwinyi ni mtaalamu wa Kiswahili, tena cha UNGUJA MJINI
 
Ni aki
Tumefanya bahati kumpata Rais Magufuli anayefahamu makosa tuliyofanya waafrika baada ya kupata uhuru miaka ya 1960s, miongoni mwa viongozi waliotufikisha hapa tulipo Mzee Mwinyi alikuwa miongoni mwao. Wako wengi tunaokunwa na utendaji wa Rais JPM lakini tuko kimya kwakuwa tunadhani hivyo ndivyo Rais wa watu anavyopaswa kuwa, lakini Mzee wetu Mwinyi ameona kumsifu JPM kimyakimya haitoshi.

Mzee Mwinyi alipata fursa ya kuyafanya haya anayoyafanya Rais JPM tena na zaidi kama angetaka kufanya hivyo. Watu wanashangaa kwanini sasa anakunwa, tena hadharani na hiki anachokifanya Rais wetu JPM. Kwa faida ya watanzania, taifa na Afrika kwa ujumla angepaswa atuambie ni kitu gani kiliwanyima viongozi wa afrika akiwepo yeye kufanya hiki anachokifanya Rais Magufuli leo kwenye awamu zao?

Hata sasa hivi nadhani Rais Magufuli kwakutumia usomi, uzoefu na weledi wake anafahamu ni kwanini Mzee Mwinyi anamsifu sana hivi, tena hadharani.

Watu wengi wanadhani uchaguzi wa Zanzibar 2020 pia unahusika.

Ni maoni yangu tu kama mtanzania wa kawaida kwenye nchi yake.
Jitambuwe wewe,umesema viongozi wa nyuma hawakuweza kufanya mambo mazuri,ila huyu wa sasa amefanya mambo mazuri,na kwa bahati mbaya sana umeishia kusema anafanya mambo mazuri.Hizi ni akili za kitoto kwasababu wale wa nyuma walifanya hovyo kwa utashi wao na huyu anafanya vizuri kwa utashi wake.Sasa je hayo mazuri yatalindwa na mfumo gani wa kikatiba pindi yeye akiondoka madarakani?Ni kosa kubwa kusifia utashi binafsi wa kiongozi,bali tunahitaji dira ya kitaifa yenye kulindwa na katiba yenye meno.
 
Unaliza mwinyi kafanya nn?bila huyo pengne tv au hata jamii forum ungekuwa unaiskia kwenye tbc taifa kwenye radio ya mninga
Mwinyi mwenyewe anajua kuwa ali-under perform ..... ndiyo maana anamuhusudu JPM.

Yaani Rais mzima, aliyetumikia kwa miaka kumi, anakuja hadharani na kudai anamuhusudu Rais mwingine kwa kiasi kile tena kwa kazi amabyo hata yeye meenyewe aliifanya. Maana katamka maneno "Kuhusudu na kuadmire" zaidi ya mara tano ndni ya dakika 3. Seriously!!

Ina maana anayoyafanya JPM hayakuwahi kuingia akilini mwake hata siku moja ....!!?
 
Mzee Mwinyi alipata fursa ya kuyafanya haya anayoyafanya Rais JPM tena na zaidi kama angetaka kufanya hivyo. Watu wanashangaa kwanini sasa anakunwa, tena hadharani na hiki anachokifanya Rais wetu JPM. Kwa faida ya watanzania, taifa na Afrika kwa ujumla angepaswa atuambie ni kitu gani kiliwanyima viongozi wa afrika akiwepo yeye kufanya hiki anachokifanya Rais Magufuli leo kwenye awamu zao?

Nilikuwa naanda uzi kuhusu huyu Mzee lakini nilivyoona umeandika hapa na kufikiria umri wake nikaamua kuacha tu. Sisi baadhi ya watanzania tuna laana ya kutosahau mambo yaliyofanywa na tawala zilizopita, sema huwa tunaacha tu mambo yapite. Lakini huyu mzee anapotokea tu na kuanza kuongea akihisi sisi watanzania ni mazuzu huwa najikuta nachafukwa sana nyongo yangu. Yaani nachafukwa mno hadi mwili unasisimka na vinyweleo vinasimama.

Huyu Mzee na genge lake la wahuni ndiyo waasisi wa kwanza kabisa wa ufisadi hapa nchini. Yeye ndiyo aliyetuletea Siasa za Business as Usual na zile za Kila mtu atakula kwa Urefu wa kamba yake. Walipishana na hayati Baba wa Taifa kwasababu Raisi Mwinyi alikuwa haamini kabisa katika Ujamaa na kusema wazi bila aibu kwamba hautekelezeki. Walikwaruzana waziwazi na ikafika hadi kipindi Nyerere akawa anamrushia vijembe vya waziwazi hadi kupelekea Raisi Mwinyi na genge lake la wahuni kujaribu kufanya baadhi ya vitu viovu dhidi ya Mzee Nyerere lakini bahati nzuri sana havikufanikiwa.

Raisi Magufuli anafuata baadhi ya sera za kijamaa na hilo kaliweka wazi kabisaaa. Tena mbaya zaidi ni kwamba anafuata mambo mengi kutoka awamu ya kwanza ambayo Raisi Mwinyi alizikataa sera zake. Sasa juzi nikabaki najiuliza hivi kwanini huyu Mzee anasifia kitu ambacho hakuwahi kukiamini hata siku moja ?

Mimi nasema tu, ni hatari sana kwa Rais Magufuli kuzungukwa na wazee kama hawa...
Mzee ambaye yuko radhi kuvaa unafiki kwasababu ya maslahi ya familia yake halifahi taifa kabisaa.
Hata huyo Hussein Mwinyi naamini hana tofauti sana na Baba yake, kama alivyo January na Yusuph.


Hopeless kabisaaaa kuwa na Taifa ambalo lina viongozi wenye kutengeneza kigenge cha watoto wao waje kushika nyadhifa kubwa za nchi.
 
Back
Top Bottom