Mzee mwenye umri wa miaka 78 aanza kusoma darasa kwanza tarime

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Nyamhanga Suguta Gesaba (78) mkazi wa kitongoji cha Kibeyo Kijiji cha Getenga kata ya Mbogi Wilayani Tarime Mkoani Mara ameamua kujiunga na masomo ya shule ya msingi na kuanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Makerero.


Mzee huyo anasema lengo kuanza kusoma ni kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu ili kuendeleza biashara zake ndogo ndogo za kuuza ndizi.


Mzee Huyo amesema kuwa hakubahatika kwenda shule kipindi cha ujana wake hivyo alianza mwaka jana kwenda shule na akabahatika kufaulu na hivyo ameamua kujiunga darasa la kwanza ili kutimiza ndoto yake kwani elimu haina mwisho.

Walimu wa mwanafunzi huyo wanasema maendeleo yake shuleni ni mazuri.


IMG_20170206_122750.jpg
IMG_20170206_122843.jpg
IMG_20170206_123902.jpg


Chanzo: Malunde blog
 
Mwanafunzi ni mwanafunzi tu hata uwe na miaka mingapi au hata uwe unajua kiasi gani
Ukiitwa mwanafunzi maana yake kuwa hujui na unataka kuelimishwa/kufundishwa
 
Back
Top Bottom