Mzee Mshume Kiyate, hii ndiyo historia yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
1711459995349.png

Mzee Mshume Kiyate akimvisha Mwalimu Nyerere kitambi kumfariji baada ya maasi ya 1964
1711460132626.png

Aliyemshika Nyerere mkono kulia ni Mshume Kiyate, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi Uchaguzi wa Rais 1962.
1711460496765.png

View: https://youtu.be/SiZ7ibE5mPc
 
Nyerere aliwaacha mbali sana hawa wazee ndo maana ili ionekane kafanya kazi kubwa lazima uoneshe alishirikianaje na Nyerere
 
Nyerere aliwaacha mbali sana hawa wazee ndo maana ili ionekane kafanya kazi kubwa lazima uoneshe alishirikianaje na Nyerere
Mpaji...
Huijui historia ya TANU.

Nyerere hakuwa na wazee kama mwenyewe alivyoeleza.

Soma hapo chini uwaone vijana wenzake aliowakuta katika harakati:

KAULIZA MUULIZAJI: ‘’KWA NINI MAJINA YA WAASISI WA TANU 1954 YAPO KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA LAKINI WAASISI WA AFRICAN ASSOCIATION 1929 HAYAONEKANI POPOTE?’’

Kijana alichonitafutia ni historia ya Muungano wa Tanzania mwaka wa 1964.

Akanifahamisha kuwa amesoma kitabu cha historia ya muungano kilichoandikwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2022).

Katika kitabu hiki alikuta orodha ya majina ya waasisi wa TANU lakini hakuona majina ya waasisi wa African Association.

Ametafuta kwingi lakini hakuweza kuyapata majina hayo ya waasisi wa African Association.

Kauliza kwa nini majina ya waasisi hawa hayapo na kama nayajua majina yao.

Jibu langu kwake ni kuwa swali hili kalileta sipo alistahili kuwauliza CCM swali hili kwani wao ndiyo warithi wa historia ya TAA na TANU vyama vilivyotokana na African Association.

Nilimjibu hivyo na nikamueleza kuwa mimi nayajua majina ya waasisi wa African Association na mengine lakini itakuwaje ikiwa CCM wakayakataa majina hayo kuwa si ya waasisi wa African Association?

Kijana akasisitiza kuwa angependa kuyaona majina ambayo mimi ninayo yamsaidie katika utafiti wake wa historia ya muungano.

Kwa faida ya wanafunzi wa historia ya uhuru wa Tanganyika naweka hapo chini majina ya waasisi wa TANU na chini yake naweka majina ya waasisi wa African Association taarifa nyingine muhimu katika historia ya TANU:

Waasisi wa TANU 1954:

1. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
2. Germano Pacha – Jimbo la Magharibi
3. Joseph Kimalando – Jimbo la Kaskazini
4. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
5. C.O. Milinga – Jimbo la Mashariki
6. Abubakari Ilanga – Jimbo la Ziwa
7. L.B. Makaranga – Jimbo la Ziwa
8. Saadani A. Kandoro – Jimbo la Ziwa
9. Suleman M. Kitwana – Jimbo la Ziwa
10. Kisung’uta Gabara – Jimbo la Ziwa
11. Tewa Said Tewa – Jimbo la Mashariki
12. Dossa A. Aziz – Jimbo la Mashariki
13. Abdulwahid Sykes – Jimbo la Mashariki
14. Patrick Kunambi – Jimbo la Mashariki
15. Joseph K. Bantu – Jimbo la Mashariki
16. Ally Sykes – Jimbo la Mashariki
17. John Rupia – Jimbo la Mashariki

Waasisi wa African Association 1929:

1. Cecil Matola (President)
2. Kleist Sykes (Secretary)
3. Mzee bin Sudi
4. Ibrahim Hamisi
5. Zibe Kidasi
6. Suleiman Majisu
7. Ali Said Mpima
8. Rawson Watts
9. Raikes Kusi

TAA Political Subcommittee 1950:

1. Dr. Vedasto Kyaruzi (President)
2. Abdul Sykes (Secretary)
3. Mufti Sheikh Hassan bin Ameir
4. Sheikh Said Chaurembo
5. Hamza Mwapachu
6. Steven Mhando
7. John Rupia

TAA Executive Committee 1953:

1. J.K. Nyerere (President)
2. Abdulwahid Sykes (Vice-President)
3. J.P. Kasella Bantu (General Secretary)
4. Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz (Joint Minuting Secretary)
5. John Rupia (Treasurer)
6. Ally K. Sykes (Assistant Treasurer)
7. Committee Members: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko
 
Jina namba 9 upande wa waasisi wa TANU 1954 kwa usahihi ni Suleimani Kitwara. Mwenyeji wa Musoma.
 
Back
Top Bottom