Mzee Mkapa: Imani za kishirikina nyumbani Lupaso zilisababisha Mama, bibi na bibi yake mama kupigwa na kuteswa kwa tuhuma za kusababisha ukame

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,901
14,368
Kisa hiki kipo kwenye kitabu chake na kinasimuliwa na Profesa Mkandala

Kutokana na Familia ya Mkapa kuonekana inajiweza kidogo ilionewa wivu na chuki, Mwaka 1947 kulitokea ukame mkali watu wakamleta mganga wa kienyeji pale Kijijini kwao Lupaso, wakaamua Mama mzazi wa Mkapa, bibi yake na Bibi wa Mama yake wameroga mvua isinyeshe.

Mama wa Mstaafu Mkapa, Mama wa Mama yake na Bibi wa Mama yake walipigwa na kuteswa sana kwa tuhuma hizo za kuroga kuzuia mvua hadi Padri mzungu alipofanikwia kuwaokoa, Mama wa bibi yake aliaga Dunia muda mfupi baada ya tukio hilo.


mkapa.jpg

UchambuziMyLifeMyPurpose

Pole sana Mh Rais Mstaafu.
 
Kweli kabisa mkuu
Pole sana Mh. Rais Mstaafu, historia kama hizi huwa ndizo driving force kufikia our dreams, na kweli Title ya kitabu chako kinasadifu yote uliyopitia. Kila mtu anayo ya kusimulia.
 
Nimemkumbuka Saanane, nadhani hata baba yake ana mateso mengi moyoni ila anakosa pakuongelea. Akumbukwe Ben.
Maskini baba yake ameshaamua kuweka matanga ya mwanae na kuwasamehe wote, maana ni mwaka wa 3 huu unakwenda hata dalili za kwamba atamwona mwanawe akiwa uhai hazipo.

Pole sana Mzee wetu, na Ben utakukumbukwa na wana mageuzi na wapigania demokrasia ya kweli Tanzania na Africa nzima kama kijana shujaa!
 
Maskini baba yake ameshaamua kuweka matanga ya mwanae na kuwasamehe wote, maana ni mwaka wa 3 huu unakwenda hata dalili za kwamba atamwona mwanawe akiwa uhai hazipo. Pole sana Mzee wetu, na Ben utakukumbukwa na wana mageuzi na wapigania demokrasia ya kweli Tanzania na Africa nzima kama kijana shujaa.
Vipi mzee alishaweka matanga.
 
Out of the topic
Maskini baba yake ameshaamua kuweka matanga ya mwanae na kuwasamehe wote, maana ni mwaka wa 3 huu unakwenda hata dalili za kwamba atamwona mwanawe akiwa uhai hazipo. Pole sana Mzee wetu, na Ben utakukumbukwa na wana mageuzi na wapigania demokrasia ya kweli Tanzania na Africa nzima kama kijana shujaa!
 
Mafanikio yanasakwa kwa kila mbinu iwe chafu ama safi cha muhimu kuyafikia hizi ni stori za ujanani
 
Back
Top Bottom