Mzee 'Mapesa', John Memosa Cheyo "Ripoti Imenitoa Machozi!. Tumepata Rais Jasiri!. Tumuunge Mkono!".

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,688
119,326
Wanabodi
Mwenyekiti wa UDP, Mzee John Memosa Cheyo 'Mzee Mapesa', yuko live TBC kwenye Jambo Tanzania, akijadili ripoti pili ya makinikia, amesema "Ripoti Imemtoa Machozi!. Tumepata Rais Jasiri!. Nampongeza Sana, Watanzania wazalendo lazima Tumuunge Mkono!".

Amesema hata rais Magufuli yalimtoka machozi ya ndani na Nyerere kule aliko anabubujikwa na machozi ya furaha angalau Tanzania imepata rais wa kwanza Mzalendo baada yake.

Endelea kufuatilia

Paskali
 
Better late than never, karibia miongo miwili kitu kinafanyika wanaangalia tu.
I have more faith kwa vijana sio hawa wazee, wengi elimu za bure au tamaa za pesa.
Ngoja tuone hili la makinikia litaishia wapi, sio mwezi ujao linakuja jingine hili linafunikwa linapotea moja kwa moja watu wanasahau kama walivyosahau ya Bashite ambalo hadi leo linanikera.

Hii mikataba hamna haja ya kuifanya iwe ya siri, natengeneza website secured watupe tuiweke wazi kama wameshindwa kuiweka kwenye website zao official. Hata marekani ukiingia department of defense website kuna contracts za miaka zote zipo wazi mtu unaclick unasoma.
 
Wanabodi
Mwenyekiti wa UDP, Mzee John Memosa Cheyo 'Mzee Mapesa', yuko live TBC kwenye Jambo Tanzania, akijadili ripoti pili ya makinikia, amesema "Ripoti Imemtoa Machozi!. Tumepata Rais Jasiri!. Nampongeza Sana, Watanzania wazalendo lazima Tumuunge Mkono!".

Endelea kufuatilia

Paskali
Paskali, unadhani kuna mtu wa kwenda TBC kutoa mawazo yake huru? Cheyo???????!!!!!! Kila mmoja amefungwa na vitisho! Wakija nje nitawashughulikia!
 
Mimi naona hiyo mikataba ikirudishwa, na ile mingine ya kitaifa wabunge wapige kura ya wazi kama bunge la katiba ili wakifanya ujinga tunadeal nao
 
Kazi ya upinzani sio kupinga kila kitu, linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania tunapaswa kuwa wamoja. Hivyo amesisitiza Watanzania tutangulize uzalendo kwa kumuunga mkono rais wetu.

P.
 
Amesema uamuzi wa rais kupitia mikataba yote utatuletea misukosuko mikubwa, na matatizo makubwa kwa rais Magufuli. Atatikiswa, atafinywa finywa, atasumbuliwa, atatishwa na hata kufikishwa mahakamani kwa sababu wanaotuibia ni mataifa makubwa na yenye nguvu hivyo Watanzania wote tuwe wamoja katika hili, tuungane na rais watu katika kutetea rasilimali za taifa letu.

P.
 
Amesema katika kipindi chote akiwa Bungeni, akiwa Mwenyekiti wa PAC, ameipigania sana Vote 58: ya madini alipigania mikataba iletwe Bungeni, alikataliwa.

P.
 
Kazi ya upinzani sio kupinga kila kitu, linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania tunapaswa kuwa wamoja. Hivyo amesisitiza Watanzania tutangulize uzalendo kwa kumuunga mkono rais wetu.

P.
Ccm hapa ndio huwa wananifurahisha..hoja ya upinzani inapoletwa since day one inakatiliwa

Leo hii hoja ya zaidi ya miaka 10 iliyopita hoja ile ile iliyopingwa bungeni..leo hii inaonekana kuwa ni Lulu..ipo haja watz wote tukapimwa IQ yetu ya akili
 
Amepongeza uamuzi wa kupitia mikataba yote na kusema hili ni Pandora Box hivyo kutaibuka madudu ya ajabu.

P.
 
pascal acha kutuuzia sura humu ndani...tumuunge nani mkono kwa lipi alilofanya??
kuwahoji akina Daniel Yona nayo ni adhabu wakati alikuwa kitanzani akamtoa mwenyewe?
Hizi tamthilia uzuri wake zinasindikizwa na wasanii so no wonder wenye akili zao wanaiona tamthilia ya awamu ya tano
 
Cheyo amehitimiisha kwa kauli hii kwa Watanzania kwa kusisitiza wito wa tumuunge mkono rais wetu Magufuli kwa kumwambia "Mhe Rais Tuko Pamoja na Wewe"

Kipindi Kimemalizika.

Asanteni

Paskali
 
Ccm hapa ndio huwa wananifurahisha..hoja ya upinzani inapoletwa since day one inakatiliwa

Leo hii hoja ya zaidi ya miaka 10 iliyopita hoja ile ile iliyopingwa bungeni..leo hii inaonekana kuwa ni Lulu..ipo haja watz wote tukapimwa IQ yetu ya akili

Nyinyi mliiua hoja ya ufisadi na mkamkaribisha fisadi mkuu huko kwenu na kumpa nafasi ya kugombea urais
 
Back
Top Bottom