Uchaguzi 2020 John Cheyo: Mimi ndiye mwenyekiti wa UDP, Nitashawishi tumuunge mkono Rais Magufuli

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
" Mimi ndiyo mwenyekiti nitashawishi vikao vyote vya UDP kwamba @ccm_tanzania wakimteua @MagufuliJP kuwa mgombea Urais na sisi tutamuunga mkono lakini wasipomteua basi tutaangalia namna nyingine " - John Cheyo, Mwenyekiti wa UDP.

EastAfrikaRadio

Kuna Mtu Mmoja aliwahi Kuniambia kuwa Mzukulu ukifa ukiwa umewatendea Mabaya Watu Kaburi lako wanaweza hata Kulinyea Mimavi tele tu.

======

Dar es Salaam
CHAMA cha upinzani hapa nchini cha United Democratic Party, (UDP) leo Julai 2, 2020, kimefungua dirisha la uchukuaji fomu kwa wanachama wake wanaotaka kugombea Ubunge na Udiwani, huku kikitangaza kuwa hakitaweka mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa akufanyika Oktoba mwaka, badala yake kitamuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampitisha kuwa mgombea wake wa urais

Mwenyekiti wa Chama UDP John Cheyo (Mapesa) amesema kipaumbele cha Rais Magufuli kuwainua wanyonge na kuleta maendeleo nchini ndio sababu iliyowafanya kuumuunga mkono katika ngazi ya kiti cha Urais, badala ya kuweka mgombea ambaye atampunguzia kura bila sababu.

"Namsifu Magufuli kwa kuboresha uchumi wa nchi kwa kuboresha miundombinu ya usari na usafirishaji wa anga, reli, barabara, bandari na pia kuwabana watumiaji vibaya wa madaraka na arasilimali za nchi tena ameboresha huduma za kijamii kama afya na elimu, ndiyo maana tumeamua kumuunga mkono endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema Cheyo.

Chama cha UDP kimekuwa cha pili kuunga mkono Rais Magufuli baada ya kutanguliwa na Chama Cha TLP ambacho tayari kimeshatangaza pia kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.

Kuhusu kufundua dirisha la wagombea wa Ubunge na Udiwani kupitia UDP, Cheyo amesema baada ya dirisha hilo kufunguliwa leo, siku ya mwisho wa uchukuaji wa fomu hizo watatangaza kuendana na ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusema "Natoa Rai kwa wanachama wa UDP, kuja kuchukua fomu ili kuweza kupata nafasi ya kuingia katika baraza la maamuzi,".
 
Chadema imeunga mkono kwa style yake

Wagombea wake wa Urais wa 2010 na 2015 wapo na Jpm na wa 2015 kamdhamini kabisa
Mwacheni tu aunge juhudi, mwenzake Lyatonga kesha tangulia. Niwashauri na vyama vyao wavivunje kabisa au wanasaka ........
 
" Mimi ndiyo mwenyekiti nitashawishi vikao vyote vya UDP kwamba @ccm_tanzania wakimteua @MagufuliJP kuwa mgombea Urais na sisi tutamuunga mkono lakini wasipomteua basi tutaangalia namna nyingine " - John Cheyo, Mwenyekiti wa UDP.

EastAfrikaRadio

Kuna Mtu Mmoja aliwahi Kuniambia kuwa Mzukulu ukifa ukiwa umewatendea Mabaya Watu Kaburi lako wanaweza hata Kulinyea Mimavi tele tu.
The man is politically and healthy wise "Gasping for air".
 
Cheyo anavizia teuzi, namwambia hivi imekula kwake kwani membe na wenzake sita wamejiapiza kumchomoa jiwe ikulu kwa namna yoyote ile, kumbuka kikwete na nkapa ni miongoni hao sita wenzake na membe!
 
Chama cha United Democratic Party (UDP) kimetangaza rasmi kumuunga mkono mgombea ( 334 X 640 ).jpg

Chama mfu cha UDP leo kupitia Ndugu John Momose Cheyo ambaye bado haijafahamika kama ni mwenyekiti au la , kutokana na chama hicho kutofanya uchaguzi wowote katika kipindi cha zaidi ya miaka 20 , kimetangaza kumuunga mkono Dr Magufuli ikiwa chama chake cha ccm kitampitisha kuwa mgombea urais .

Bado haijajulikana kama wamekaa kikao kama chama au ni Cheyo binafsi kwa utashi wake ameamua .
 
Kwani UDP bado ipo hai! Siyo mbaya mzee wa mapesa akitafuta mahali pa kujishikiza wakati huu.
 
" Mimi ndiyo mwenyekiti nitashawishi vikao vyote vya UDP kwamba @ccm_tanzania wakimteua @MagufuliJP kuwa mgombea Urais na sisi tutamuunga mkono lakini wasipomteua basi tutaangalia namna nyingine " - John Cheyo, Mwenyekiti wa UDP.

EastAfrikaRadio

Kuna Mtu Mmoja aliwahi Kuniambia kuwa Mzukulu ukifa ukiwa umewatendea Mabaya Watu Kaburi lako wanaweza hata Kulinyea Mimavi tele tu.
who is he? Si akihamishe "kikoba" chake kijiunge na CCM
 
Mwacheni tu aunge juhudi, mwenzake Lyatonga kesha tangulia. Niwashauri na vyama vyao wavivunje kabisa au wanasaka ........

Bora Lyatonga huyu mwingine 'ungosha' wake unatia ukakasi bora hata angalikaa kimya.
 
Back
Top Bottom