Rais Magufuli: Mtu akipambana na Madawa Tumuunge mkono si kumchafua

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo hapa Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania Uganda Grace Aaron Mgovano.

Pia Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.

Vilevile Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya ambazo zinazidi kuangamiza nguvukazi ya Taifa.

“Niwaombe ndugu zangu tuungane katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, waandishi wa habari na wana mitandao tuweke mbele Utanzania wetu, akitokea mtu anapambana na dawa za kulevya tumuunge mkono badala ya kumchafua”

“Vita hii ni kubwa hatuwezi kwenda nayo kwa mzaha na Serikali itahakikisha inasimamia sheria namba 5 ya mwaka 2015 iliyohusu kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ambayo ilitungwa na Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda na sheria hiyo ikatiwa saini na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nawapongeza sana kwa kutunga sheria hii.”

Dkt. Magufuli amesema takwimu zinaonesha kuna watanzania 1,007 wamekamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya, na amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo kutojihusisha kuwatetea waliofungwa kwa makosa hayo na badala yake waache sheria za nchi husika zichukue mkondo wake.
 
wakuu wa mikoa wote wameanza kupambana vizuri katika vita hii ya madawa ya kulevya,ila kwa walio dar poleni sana mana jamaa hawezi kupambana kimya kimya hio ni hulka,mwizi ni mwizi tu ukimkimbiza kimya kimya au kwa kelele haiondoi mana ya mwizi.
Heko Rais wangu JPM
 
Tena mkuu wa mkoa wa DSM anapokea mpaka misaada ya watu wanaoshukiwa kuwa katika biashara hii! Heko!
9b35f0bcbbdb044a8a6daa2b86201622.jpg

05c66b998063b23c9690d3de65758749.jpg
 
Hahaaa, haya sasa mechi inaendelea, kati ya team mihadarati na Anti drugs. Mpaka sasa Anti drugs wana goal 3, mihadarati 0: ila naona mihadarati wanashumbulia kweli goal la Anti drugs pengine waweza funga goal.

Tuendelee kuweka maombi Anti drugs waibuke na ushindeo_Oo_O
 
wakuu wa mikoa wote wameanza kupambana vizuri katika vita hii ya madawa ya kulevya,ila kwa walio dar poleni sana mana jamaa hawezi kupambana kimya kimya hio ni hulka,mwizi ni mwizi tu ukimkimbiza kimya kimya au kwa kelele haiondoi mana ya mwizi.
Heko Rais wangu JPM

Ni kweli mkuu.
 
Vita in yet sote lakini mheshimiwa asiwakingie watumishi husika wanao vunja utaratibu Na Sheria katika zoezi hili. Imeashiria dhahiri kama alivyo Fanya makonda wanaojihusisha Na Bishara hii kujihami Na kupoteza ushahidi.
 
Ndo maana niliwaambia vijana bunge haliwezi kusababisha Makonda aondolewe. Hayo ni kwa kifupi zaidi, mengi watapewa kwenye party caucus, wataambiwa waache uchadema. Ndipo utaelewa kwamba baadhi ya vifungu kwenye katiba ni mapambo.
 
Kuanzia sasa tuanze kuhesabu siku mpaka pale madereva atakapofanya kitu kimuudhi mwenyekiti. Vijana wa kidato cha nne wametaga wakati wana fursa nyingi ambazo wenzao wa mikoani hawana, lakin mwenyekiti wala hajazungumzia maana hataki kuharibu taswira ya madereva. Nakuhakikishia utahesabu mpaka nywele na hiyo siku haitatokea.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo hapa Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania Uganda Grace Aaron Mgovano.

Pia Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.

Vilevile Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya ambazo zinazidi kuangamiza nguvukazi ya Taifa.

“Niwaombe ndugu zangu tuungane katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, waandishi wa habari na wana mitandao tuweke mbele Utanzania wetu, akitokea mtu anapambana na dawa za kulevya tumuunge mkono badala ya kumchafua”

“Vita hii ni kubwa hatuwezi kwenda nayo kwa mzaha na Serikali itahakikisha inasimamia sheria namba 5 ya mwaka 2015 iliyohusu kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ambayo ilitungwa na Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda na sheria hiyo ikatiwa saini na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nawapongeza sana kwa kutunga sheria hii.”

Dkt. Magufuli amesema takwimu zinaonesha kuna watanzania 1,007 wamekamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya, na amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo kutojihusisha kuwatetea waliofungwa kwa makosa hayo na badala yake waache sheria za nchi husika zichukue mkondo wake.
Noted
 
Back
Top Bottom