Mzee Malecela atangaza kutetea jimbo lake!

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
Mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, amevunja ukimya na kutangaza kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake.

Alisema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wilayani Chamwino juu ya watu ambao wamekuwa wakisema kuwa hafai kugombea tena kutokana na kuwa na umri mkubwa.

Malecela alisema kuwa wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea kutokana na maneno ya watu kuwa yeye hana sifa ya kuwa mgombea tena bila kujali kuwa wananchi wanataka nini.

Alisema hata kama hatagombea bado ataendelea kuheshimika kwani amewafanyia wananchi wake mambo makubwa na kutekeleza ilani ya chama kwa asilimia kubwa lakini hawezi kuacha wakati wakiwa bado wanamuhitaji aendelee kuwafanyia yale yalio salia.

Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao, alisema Mwanasiasa huyo mkongwe.

Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kwa nini haigi mfano wa wazee wenzake walioamua kuacha kugombea kama Paul Kimiti, Malecela alisema, Mimi ni Malecela na kimiti ni Kimiti kwa hiyo siwezi kuiga kitu ambacho hakiko moyoni mwangu mwenyewe wametangaza hivyo na mimi natangaza kuwa nagombea.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Unajua mie siwaelewi hawa viongozi wa Afrika??? Wanataka kufia katika kiti cha uongozi.

Nikimquote jamaa anadai "Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao, Hivi unadhani wananchi watasema hawamuhitaji wakati jamaa hawapishi wenzie wakaongoza???

Jamaa anakaa madarakani hadi anakongoroka utafikiri ni ufalme. Mabadiliko hayaletwi na kiongozi aliyekaa muda mrefu kwasababu hana benchmark ya kuibeat but instead anatawala kama vile amezaliwa na cheo hicho. Kiongozi mpya akija huwa anatazama mwenzie amefanya nini ili na yeye aweze kuyapiku malengo ya mwenzie aliyepita. Sasa malecela anapredecessor gani anayejicompare naye.

Jamaa anataka madaraka hadi siku atakapokufa !!!!!
 
Unajua mie siwaelewi hawa viongozi wa Afrika??? Wanataka kufia katika kiti cha uongozi.

Nikimquote jamaa anadai "Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao”, Hivi unadhani wananchi watasema hawamuhitaji wakati jamaa hawapishi wenzie wakaongoza???

hahaaaa, we subiri uone moto!!
 
hahaaaa, we subiri uone moto!!

Tehetehe nausubiri kwa hamu labda atumie na viagra mtu anafikia kuwa umri karibu twice the age ya akina dewji bado yupo nae si kituko hichi!!!! Nadhani hata mawazo nayo huwa ya kuzeeka pia.
 
Wakuu kama vipi kachukueni fomu mumpinge.Siasa za kusubiri mtu mpaka atoke mwenyewe zishapitwa na wakati.
 
Angalia ushauriwa De Novo hapo juu!

Kaka ishu sio kuchukua fomu au kutishwa ishu ni busara huyu mzee amekaa madarakani tangu mie mtoto hadi sasa wengine tuna wajukuu anapigana vikumbo bado katika viunga vya bunge tu.

Na nasikia jimboni kwake kaweka wanted kwa yeyote anayetaka kumpinga sasa unadhani utachukua fomu hapo kamanda.
 
Wakuu kama vipi kachukueni fomu mumpinge.Siasa za kusubiri mtu mpaka atoke mwenyewe zishapitwa na wakati.

Very good suggestion; nategemea vijana watajitokeza... ila wakirudi huko waje watujuze yaliyojiri ingawa yako predictable
 
Kaka unawatisha hivyo waachie wajaribu huwezi jua pengine wana ubavu naye ila mie nadhani atumie busara tu kuachia ngazi kwani ameshazeeka.
 
Kizee hiki nacho....hakioni aibu?shit what else do he want?kwanini asijipumzikie tu kwa heshima zote?I wish apate mpinzani mzuri ili ammwage..
 
Malecela%284%29.jpg

Mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela

Mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, amevunja ukimya na kutangaza kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake.

Alisema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wilayani Chamwino juu ya watu ambao wamekuwa wakisema kuwa hafai kugombea tena kutokana na kuwa na umri mkubwa.

Malecela alisema kuwa wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea kutokana na maneno ya watu kuwa yeye hana sifa ya kuwa mgombea tena bila kujali kuwa wananchi wanataka nini.

Alisema hata kama hatagombea bado ataendelea kuheshimika kwani amewafanyia wananchi wake mambo makubwa na kutekeleza ilani ya chama kwa asilimia kubwa lakini hawezi kuacha wakati wakiwa bado wanamuhitaji aendelee kuwafanyia yale yalio salia.

"Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao," alisema Mwanasiasa huyo mkongwe.

Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kwa nini haigi mfano wa wazee wenzake walioamua kuacha kugombea kama Paul Kimiti, Malecela alisema, "Mimi ni Malecela na kimiti ni Kimiti kwa hiyo siwezi kuiga kitu ambacho hakiko moyoni mwangu mwenyewe wametangaza hivyo na mimi natangaza kuwa nagombea."

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
  • Mzee wetu huyu ana tatizo gani kiasi kuwa hataki kuachia ngazi?
  • Amejuaje kuwa wananchi jimboni kwake bado wanamtaka au naye ana utaalam wa Sheikh Yahya?
  • Hivi ni mpaka afie kwenye kidonda ndio atajua kuwa kalewa madaraka?
 
Mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, amevunja ukimya na kutangaza kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake.

Alisema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wilayani Chamwino juu ya watu ambao wamekuwa wakisema kuwa hafai kugombea tena kutokana na kuwa na umri mkubwa.

Malecela alisema kuwa wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea kutokana na maneno ya watu kuwa yeye hana sifa ya kuwa mgombea tena bila kujali kuwa wananchi wanataka nini.

Alisema hata kama hatagombea bado ataendelea kuheshimika kwani amewafanyia wananchi wake mambo makubwa na kutekeleza ilani ya chama kwa asilimia kubwa lakini hawezi kuacha wakati wakiwa bado wanamuhitaji aendelee kuwafanyia yale yalio salia.

“Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao,” alisema Mwanasiasa huyo mkongwe.

Akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua kwa nini haigi mfano wa wazee wenzake walioamua kuacha kugombea kama Paul Kimiti, Malecela alisema, “Mimi ni Malecela na kimiti ni Kimiti kwa hiyo siwezi kuiga kitu ambacho hakiko moyoni mwangu mwenyewe wametangaza hivyo na mimi natangaza kuwa nagombea.”

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Unajua mie siwaelewi hawa viongozi wa Afrika??? Wanataka kufia katika kiti cha uongozi.

Nikimquote jamaa anadai "Ninyi wenyewe mashahidi mmewasikia wananchi wanavyosema kuwa bado wananihitaji kwa hiyo siwezi kuacha wakiwa bado wana mapenzi na mimi kiongozi wao”, Hivi unadhani wananchi watasema hawamuhitaji wakati jamaa hawapishi wenzie wakaongoza???

Jamaa anakaa madarakani hadi anakongoroka utafikiri ni ufalme. Mabadiliko hayaletwi na kiongozi aliyekaa muda mrefu kwasababu hana benchmark ya kuibeat but instead anatawala kama vile amezaliwa na cheo hicho. Kiongozi mpya akija huwa anatazama mwenzie amefanya nini ili na yeye aweze kuyapiku malengo ya mwenzie aliyepita. Sasa malecela anapredecessor gani anayejicompare naye.

Jamaa anataka madaraka hadi siku atakapokufa !!!!!

Nddugu yangu wewe ndiyo hueleweki, huu ni ubunge; chukua fomu kagombee umg'oe Malecela, siyo ati ang'atuke ati wewe unyemelee. Namsifu sana huyu mzee, yaani vijana wote mnaogopa na kutetemeshwa. You have the guts go and get the forms, go in a big way, and knock him out; that is the way an energetic young man should do. Hivi huku bongo kukoje? Fight for it, get it, siyo kungojea mkono udondoke kama "fisi".

Presidents are easier to munipulate results, ubunge? Cheza karata zako. Vijana wa Tanzania wavivu sana.
Mie nishatangaza kumng'oa Galinoma, wala simshutumu aachie ngazi, nitamtoa kwa kura; kwa points.

I still believe "when the going gets tough, the tough gets going" - Bill Ocean
 
  • Mzee wetu huyu ana tatizo gani kiasi kuwa hataki kuachia ngazi?
  • Amejuaje kuwa wananchi jimboni kwake bado wanamtaka au naye ana utaalam wa Sheikh Yahya?
  • Hivi ni mpaka afie kwenye kidonda ndio atajua kuwa kalewa madaraka?
I now believe why Tanzania imports "Human resources" we have absolete
 
Back
Top Bottom