Hivi kwani Mzee Makamba ana umri gani? Kwa mtazamo wangu alifanya kazi nzuri sana kama Katibu Mkuu wa CCM kuliko Mzee wetu Mukama wa sasa hivi. Tena ukisema kwa hoja zinazoenda na wakati, naweza bado nikamtetea Mzee Makamba kuliko Mzee Mukama.
Mimi naona hajaongea kumpinga JK, ametoa mtazamo wake wa siasa zilivyo. ni dhahiri kwamba kichini chini wana-CCM wote nchi nzima wanalalamika na hali ya nchi ilivyo na chama chao, lakini wanalinda nidhamu ya kumhehimu Mwenyekiti wao waliyemchagua wao wenyewe, Mpendwa wetu Jakaya Kikwete. Lakini ni dhahiri kwamba watakapolazimishwa kuchagua mtu, basi nidhamu itapotea. Kwani hata Mkapa hakumbeba Jakaya, kwahiyo siamini Jakaya ana mpango wa kumbeba mgombea yoyote yule.
Naamini ujumbe wa Mzee Makamba ni kwamba yoyote anayefikiria kugombea kupitia ticket ya CCM, assijipange kwa siasa za kutegemea kubebwa na Jk, bali ajenge hoja zake na watu wampime kwa mabaya na mazuri yake.
Kwa kumalizia, hivi kama tunajenga hoja ya Zitto kuwa Rais wa nchi hii mwaka 2015, tena kama private candidate, kwanini isiwe JANUARY MAKAMBA? Nawasilisha.
Kazi gani nzuri alofanya? Kwa kuiua CCM? Labda hiyo.... Wewe ni mmoja wa familia hiyo umejidhihirisha mwishoni eti JM..thee tehh eteh ndio maana mzee ameanza kutabiri ili atakaye teuliwa na CCM aambiwe waende Tanga akaoneshwe nguvu za giza na amuombe ampe kazi JM huyo unayemtaka awe rais.. kazi kweli kweli....teh theheh