Mzee Makamba aibua siri ya Urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Makamba aibua siri ya Urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Aug 9, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  *Aonya mgombea atakayebebwa na Kikwete

  Na Mwandishi Wetu

  ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza na kuzungumzia mustakabali wa taifa kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Makamba amekuwa kimya kwenye ulingo wa siasa, tangu alipoondolewa kwenye nafasi ya Ukatibu Mkuu ndani ya CCM alisema Watanzania waamini kuwa Mgombea urais 2015 atatoka kwa Mungu.

  Makamba alisema amesikia kelele nyingi kuhusu nani akayemrithi Rais Jakaya Kikwete lakini pamoja na hayo yote atakayeamua hatma ya mgombea urais ni Mungu peke yake.

  Mwanasiasa huyo machachari, anayesifika kwa kwa kutolea mifano maandiko ya kwenye vitabu vya biblia na quran, alikwenda mbali zaidi na kunukuu maandiko ya biblia akisema; " Si kila mtu aniitae bwana bwana atakayeurithi ufalme wa mbinguni' akiwa na maana kuwa si wote wanaoutaka urais watakuwa marais.

  Akitolea mfano, Makamba alisema hata wakati Kanisa la Kiinjili ya Kiluteri Tanzania (KKT) wanamchagua Askofu Mkuu wao Maaskofu wawili waliokuwa wakigombea nafasi hiyo, Steven Munga wa Dayosisi ya Lushoto na Askofu Owdenberg Mdegella wa Dayosisi ya Iringa baada ya kupigiwa kura kwa takribani mara tatu walishindwa kumpata mgombea.

  "Lakini aliibuka askofu mmoja akasema tuongeze jina la Alex Malasusa, jina la Malasusa lilipoongezwa tu walipopiga kura mara moja, Malasusa akapita, hivyo nataka kuwaambia kuwa mgombea urais 2015 atatoka kwa Mungu na atapatikana kwa staili kama aliyopatikana Malasusa…hivyo watu wasiwe na mashaka" alisema Makamba.

  Baadhi ya wanasiasa wanaotajwa kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki, Bernad Membe.

  Wengine ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, John Nchimbi.

  Alipoulizwa kati ya wanaotajwa kuwania kiti cha urais 2015 ni yupi ambaye anamuunga mkono, Makamba alisema ni mapema mno kuweka msimamo wake wazi.

  Hata hivyo alisema muda ukifika na mchakato wa kuchukua fomu za kuwania urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi utakapoanza na baada ya wagombea kuchukua fomu ndipo atakapotangaza mgombea anayemuunga mkono.

  Katika hilo, alisema mgombea atakayemuunga mkono yeye ana uhakika atapita na ndiye atakayeshinda urais 2015.

  Makamba ambaye ni mwanasiasa machachari mwenye maneno mengi, akizungumzia hilo alikwenda mbali zaidi na kutahadharisha kuwa mgombea atakayeungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete kugombea urais 2015 ataanguka.

  Alisema mgombea atakayebebwa na Rais Kikwete yatampata kama yaliyompata Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2002 alibebwa na Rais Daniel arap Moi awe mgombea wa KANU lakini matokeo yake chama kikamegeka na kusambaratika na Mwai Kibaki aliyekuwa akigombea kupitia chama cha Upinzani akaibuka mshindi kwa kura nyingi.

  Uhuru ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya alichaguliwa kuingia bungeni mwaka 2001, na kuteuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa chini ya utawala wa Rais Moi na pamoja na kwamba hakuwa na uzoefu mkubwa wa kisiasa Rais Moi alikuwa akitaka awe mrithi wake.

  Mbali na hilo Kuhusu CCM na harakati zake za siasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015, Makamba ambaye amepata kuwa kiongozi ndani ya CCM akianzia nafasi ya chini na kupanda hadi kushika nyadhifa za juu kabisa alisema ana uhakika chama hicho kitashinda.

  Alipinga akisema kuwa chama hicho hakina makundi kama ambavyo baadhi ya watu wanatafsiri.

  "Nimekaa CCM kwa muda mrefu sana…sijaona makundi yanayosemwa, ila kama ukisema pale ambapo wagombea wanachukua fomu za kuwania urais, hapo sawa makundi lazima yaibuke kwa sababu kila mmoja kuna mtu wake ambaye anaona anafaa kuwa rais" alisema Makamba.

  Kuhusu dhana ya ‘kujivua gamba' ndani ya CCM, Makamba alisema kauli hiyo imetafsiriwa vibaya na wale wanaoitekeleza.

  Alisema lengo la kujivua gamba halikuwa likiwalenga baadhi ya wanasiasa wachache ndani ya Chama cha Mapinduzi wanaotuhumiwa kwa ufisadi bali ililenga kuwaondoa watu walioonekana kukaa kwa muda mrefu katika safu za uongozi ndani ya chama na kuleta damu changa ili nao waje waongoze wakiwa na mbinu mpya.

  Alisema dhana hiyo imepotoshwa na wale wanaoitekeleza wanaitekeleza kwa malengo tofauti.


  Source: Gazeti la Fahamu
   
 2. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Makamba mtu wake ni EL.asitudanganye, Wakati JK Mtu wake ni MEMBE, Lakini wote ni mafisadi Tutakomaa hatutaki Raisi wenye harufu ya ufisadi au chama chenye harufu ya ufisadi!
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo siri iliyoibuliwa na Makamba ni kwamba Mungu ndiye anayeamua nani awe Rais?
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mzee mwenzangu Makamba uzee unaanza kumjia vibaya na anautumia vibaya. Hana hata aibu anadanganya mchana kweupe eti hajawahi kuona makundi wakati naye ni sehemu ya makundi. Makamba shame on you! Kinachokera kwa Makamba ni kuanza kumgeuka Kikwete wake akitafuta kupata pa kujishikiza akijua wazi kuwa CCM haina lake. Hata hivyo, Makamba tangu mwanzo ni kigeugeu anayeweza kufanya lolote hata kama la kumdhalilisha ilmradi mkono uende kinywani.
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Aisee Zanzibar hawana chao CCM! Kweli out of sight out of mind.
   
 6. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu dingi mwongo,amesahau alitokwa na povu aliposema mkuu wa kaya ni mtaji pekee wa ccm.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwani Mungu anapiga kura?
   
 8. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  EL kweli unatisha, ushaanza kumpiga mkwara m*were kwamba akiweka mtu wake ameisha!
   
 9. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mengi yasemwe lakini ninachojua mimi ccm ndio washindi 2015 .....
   
 10. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mdomo uliponza Kichwa! Aangalie kinachomtoka mdomoni. Jamaa anaweza akampiga chini mwanawe sasa hivi! Chezea ****** weye!
   
 11. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  huyu nae asitufanye watoto,anayemigia debe kila mtu anamjua!wanataka kumshirikisha mungu kwenye dhambi zao!kwanza kasababisha matatizo mkubwa ccm kwa kuweka watu anaowataka kuwa washindi wa kura za maoni ktk uchaguzi
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  His predictions are getting older
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Piga ua EL apewe hii nchi ila aonywe awaache wazee wapumzike na pia asilipize visasi kwa waliomsema sema kipindi chake cha mpito....wakiona wameweka wababe na watu wameshindwa kuamua,walete wapya ili Makamba apate unabii wake kutimia!!wataongezwa Magufuli na huyo waziri wa Utawala bora
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Makamba kaamua atoke vipi.
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mungu hachagui Rais ingekuwa ndiye anaechagua asingetupa hili janga!!
   
 16. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  "Mungu ametupa akili tuzitumie kama ipasavyo" kuokoa Taifa letu
   
 17. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee makamba ni mnafiki kupita maelezo hapo anasema atamtaja atakayeshinda muda ukifika iliajipendekeze kwaa atakayeona ana nguvu ya kushinda si ataje sasa kama anaweza kubhashiri kwa unajimu wake, hana lolote anawaleta anapotosha mind tuu ili watu wajue JK ana mtu wake kati ya wanaotaka kuomba urais CCM wakati si kweli karibia wote ni wale walewale tuu,mwakyembe,sita,membe,lowasaa,nchimbi na yeye makamba wote walikuwa wanamtandao wa Jk sasa utofauti unatoka wapi usanii tuu hapo.

  Rais bora wagombee kina magufuli ,mwandosya au kigoda watafanya kazi sio usanii tuu. na kina mzee makamba wanalijua hilo ndio maana hawawapi promo hawa...hao wanaotajwa kugombanani promo tuu hiyo wadanganyika fungukeni ukaelewa unavyosaniiwa
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani muambiwe mara ngapi msikie? Lowassa anautaka sana urais lakini HATAKUWA RAIS hata kama atakusanya vikongwe wote hawa i.e. Makamba, Kingunge, Bomani, Kisumo n.k. Yeye hana uwezo wa uchambuzi na ni lazima aelewe kwamba mazingira ya Kanu, Moi na Kenyatta ni toafuti na mazingira ya CCM, Kikwete na wagombea waliopo. Mbona chama hakikushindwa pale Mkapa alipomridhia Kikwete? Moi aliharibu pale alipozima jaribio la kidemokrasia la kupata mgombea wakati katika issue hii kanuni za Chama na mchakato wa uteuzi utazingatiwa. Hii mbinu ya Mzee Makamba, ambaye anajua kwamba mgombea wake hachaguliki na kudhani watamtisha Rais asitekeleze majukumu yake wakati wa uteuzi hazitafua dafu.

  Makamba hana hata aibu, mwezi huu wa Ramadhan, kukanusha kwamba hakuna makundi wakati tulio nje tunajua kwamba kuna makundi mawili ndani ya chama. Kuna wale ambao ni walafi, wabinafsi, wahujumu rasilimali za nchi na wadumaza maendeleo kwa upande mmoja, na wale watetea haki za wanyonge, wapinga ufisadi na wapigania haki na walinzi wa rasilimali zetu kwa upande mmoja. Yeye ni mnufaika wa kundi la kwanza na ndiye gamba namba moja. Sasa anaibuka na kujifanya ni nabii, aende zake akaendeshe hotel yake aliyoijenga kwa fedha za ufisadi na hata kuhamishia fenicha za CCM huko!
   
 19. K

  KGBtz Member

  #19
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2007
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani Mzee Makamba ana umri gani? Kwa mtazamo wangu alifanya kazi nzuri sana kama Katibu Mkuu wa CCM kuliko Mzee wetu Mukama wa sasa hivi. Tena ukisema kwa hoja zinazoenda na wakati, naweza bado nikamtetea Mzee Makamba kuliko Mzee Mukama.

  Mimi naona hajaongea kumpinga JK, ametoa mtazamo wake wa siasa zilivyo. ni dhahiri kwamba kichini chini wana-CCM wote nchi nzima wanalalamika na hali ya nchi ilivyo na chama chao, lakini wanalinda nidhamu ya kumhehimu Mwenyekiti wao waliyemchagua wao wenyewe, Mpendwa wetu Jakaya Kikwete. Lakini ni dhahiri kwamba watakapolazimishwa kuchagua mtu, basi nidhamu itapotea. Kwani hata Mkapa hakumbeba Jakaya, kwahiyo siamini Jakaya ana mpango wa kumbeba mgombea yoyote yule.

  Naamini ujumbe wa Mzee Makamba ni kwamba yoyote anayefikiria kugombea kupitia ticket ya CCM, assijipange kwa siasa za kutegemea kubebwa na Jk, bali ajenge hoja zake na watu wampime kwa mabaya na mazuri yake.

  Kwa kumalizia, hivi kama tunajenga hoja ya Zitto kuwa Rais wa nchi hii mwaka 2015, tena kama private candidate, kwanini isiwe JANUARY MAKAMBA? Nawasilisha.
   
 20. K

  KGBtz Member

  #20
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2007
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mhe Mbopo, salam aleikum. Hivi ni wewe tuliokusoma kwenye gazeti la RAI le?. Najua utasema ni gazeti la MAFISADI, kama ambavyo RAIAMWEMA lilivyo gazeti la WAADILIFU, kama ulivyoelezea makundi yako wewe ya CCM.

  Naona unaongea kama MAMLAKA kabisa. Lowassa anautaka sana urais lakini HATAKUWA RAIS .
  Hivi wewe ni MUNGU? Maana yake hata Rais Kikwete hana mamlaka ya kusema hivyo, basi na mimi najitwisha mamlaka hayo hayo, nasema BERNARD MEMBE HATAKUWA RAIS NA WALA HATA MKUU WA WILAYA KWENYE SERIKALI INAYOFUATA. Ameeeeen.
   
Loading...