Mzee Kikwete: Tunaumaliza mwaka 2022 wananchi wakiwa na furaha, nakupongeza Majizo kwa kuchukua hatua kila inapotokea changamoto!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Rais mstaafu mzee Kikwete leo amesherehekea Sherehe za kufungua Mwaka 2022 na kuukaribisha 2023 akiwa na Wananchi wenzake wa Msoga.

Kikwete amesema ni kawaida yao tangu akiwa Rais kufanya Sherehe kama hizi ambapo Ng'ombe huchinjwa na wanakijiji kula pilau pamoja na kusherehekea.

Kadhalika mzee Kikwete amemtambulisha mh Majizo ambaye ni mmiliki wa E FM radio na TV ambaye alikuwa MC.

Kikwete amempongeza Majizo kwa namna anavyoongoza Taasisi yake na Jinsi anavyochukua hatua kwa haraka zinapotokea Changamoto.

Kikwete amesema " usione vyaelea vimeundwa" na kwamba Maendeleo tunayoyaona na yatakayokuja ni Kazi ya Kiongozi wetu shupavu Dkt. Samia.

Source: TV E
 
Rais mstaafu mzee Kikwete leo amesherehekea Sherehe za kufungua Mwaka 2022 na kuukaribisha 2023 akiwa na Wananchi wenzake wa Msoga

Kikwete amesema ni kawaida yao tangu akiwa Rais kufanya Sherehe kama hizi ambapo Ng'ombe huchinjwa na wanakijiji kula pilau pamoja na kusherehekea

Kadhalika mzee Kikwete amemtambulisha mh Majizo ambaye ni mmiliki wa E fm radio and tv ambaye alikuwa MC

Kikwete amempongeza Majizo kwa namna anavyoongoza Taasisi yake na Jinsi anavyochukua hatua kwa haraka zinapotokea Changamoto

Kikwete amesema " usione vyaelea vimeundwa" na kwamba Maendeleo tunayoyaona na yatakayokuja ni Kazi ya Kiongozi wetu shupavu Dr Samia

Source: E tv
Huyu kamtambulisha wapi kwanani au anaenda kugombea ubunge uko.
 
Umekua mwaka mzuri kwake na familia yake na watu wote walio kwenye circle yake nao hao wakina majizo wake.
Waendelee kuwa na furaha mybe Mungu yupo upande wao sisi alisha tuacha!
Usikufuru.

Tuwe katika shida au taabu, furaha au majonzi, tupo katika ulinzi wa Mungu wetu. Mungu hamwachi mja wake anayemtegemea, japo katika macho ya wanadamu yawezekana tusione.
 
Aisee ,
Any way ni jambo jema kusherehekea mwaka na Ndugu na jamaa lakini pawe na Akiba ya maneno!

Dunia haijawahi kushuhudia nchi ikitawaliwa na kundi la aina Moja muda WOTE.

Hata Nchi zenye Demokrasia kama Marekani hua Zina pata watawala wenye misimamo Tofauti na wanachaguliwa na wanachi. CCM ni vyama vingi NDANI ya kimoja. Kwa Sasa ni Zamu ya Akina asali Lakini wapende wasipende automatically atakayekuja SIO mwenzao . Utawala ni Suala la kimungu. Hata Mugabe alipandikizwa na Mabeberu Wa Zimbabwe wakati Huo lakini baadae aliwageuka Wakati ulipofika akawa adui Yao Mkubwa.

Ukiona vya Elea kwenye nchi basi ujue ni mapenzi ya Mungu aliyewapa wanadamu uwezo Wa kuviunda.
 
Umekua mwaka mzuri kwake na familia yake na watu wote walio kwenye circle yake nao hao wakina Majizo wake.
Waendelee kuwa na furaha maybe Mungu yupo upande wao sisi alisha tuacha!
Wazee wa nongwa uwanjani! Si mchezo, kazi ipo!!

Angekuwa mtu wa kujali, kikwete angefika akiwa hoi kabisa......ila mwamba hana time na haters kabisa, yaani hawampotezei hata sekunde yake.
 
Kikwete amempongeza Majizo kwa namna anavyoongoza Taasisi yake na Jinsi anavyochukua hatua kwa haraka zinapotokea Changamoto.
Jinsi alivyochukua hatua haraka kwa Hsndo? Hatari hii jamani.

Hivi Majizo = Kikwete =. EFM ???
Nauliza tu.
 
Back
Top Bottom