Miaka kumi, watoto wakikaa chini, hospitali mhimbili mashine zote hoi, safari za nje nyingi kuliko uchumi wetu, wachache walitajirika, pengine wewe ukiwa mmojawapo na wengi masikini wa kutupa. Bei za nyumba zilikuwa feki nyumba mpaka dollers millioni 3 kwa uchumi gani? WALIOWEZA kununuwa ni wauza unga ama wapiga tenda, mwenye pesa ndiye mushindi, masikini hana sauti. Mafisadi wakiiba mchana bila ya kuogopa, Wauza unga Kikwete aliogopa kuwataja, watumishi feki, wanafunzi feki, uchumi feki, mizigo ikipitishwa mchana bila ya kodi. Leo mahakama zetu bado zina mawazo ya zamani, mahakimu wote walioshitakiwa kwa rushwa wote waneshinda kesi, hiyo ndiyo ilikuwa serikali ya Kikwete. Pengine Kikwete aje akuokowe wewe lakini siyo nchi, utawala wake kwa kuwa Hakuna deal tena umekwana, KWA Watanzania wengi, uongozi wake ndiyo umetufikisha hapa tulipo. Mikataba mibovu, watu wavivu kwa uongozi wake, akichoka anashika NDEGE Marekani au Australia. Rais Magufuli kaokoa jahazi lilikuwa linazama. Musema kweli ni mpenzi wa MUNGU. Baba akipiga suit na watoto wakivaa mitumba, hiyo ndiyo ilikuwa serikali ya Kikwete.