Namuomba Radhi Mzee Jakaya Kikwete

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne binafsi nakuomba Radhi leo kwa yote nilikuwazia au hata kukusema kiukweli at that time nilikuwa na Moto wa ujana na sikujuwa uzee wako ni hekima.

Nikiwa kama Raia wakawaida kabisa niliwahi kukuandikia baruwa na nikalalamika sana juu ya upole wako na democrasia ilio pitiliza.

Mungu sio athumani umemaliza muda wako nikaona utawala Ambao kiukweli ulinipa visible niliitaka Ola mara vaible nikaja gunduwa nacheza mziki gerezani na ninaye mfurahia anaumia kumbe na mimi kesho zamu yangu. Kiukweli fumbo hili limenifanya kuja hapa nakukuomba Radhi kweli nisamehe naomba Radhi Kwa niaba yangu na watanzania wengine walio waza kama mimi.

Kumbe yapo maisha badala ya vitu kumbe furaha yetu haipo katika vitu au majengo ila furaha yetu ipo katika upendo, Amani na Uhuru katika Taifa letu.

Naiangalia Libya nchi ambayo watu wake walipata kila kitu ila wakazibwa midomo jambo lililo tokea linatisha Sana. Naweza nakukumbuka Kuwa leo tunawakumbuka viongoz wetu sio Kwa vitu ila upendo na Amani walituachia. Wewe ni moja ya viongozi hakika ulitupa vaible ya democrasia na hakika hatuwezi kukusahau kamwe.

Nitawasimulia wanangu yote nimeyaona na hakika yapo mema mengi nimejifunza najuwa ipo siku Taifa hili litakuwa na Kikwete day siku ambayo watu watacheza na kufurahi kuhadhimisha miaka kumi ya utawala wako.

Naweza Sana nakumbuka sana mambo maneno yako ambayo mpaka leo yananisumbuwa kichwa.

Maneno mazito ya Kwanza uliyatoa kwenye hotuba ya Kwanza katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nani nanukuu. "Tusifanye mambo ambayo watoto wetu watachukua fimbo nakuyachapa Makaburi yetu nakuuliza hawa walikuwa na akili?" Mwisho wakunukuu.

Nukuu ya mwisho na inayonifanya kuamini ulikuwa nabii ipo katika Bunge la katiba Nani na nukuu. "Hii katiba ina MPA nguvu kubwa Rais hata mimi sijazitumia ila atakuja MTU hii itawasumbuwa "kipindi kile tulikudharau nakukukejeli ila Nabii hakubaliki nyumbani Mbio umezimaliza na sisi tutakuwa mashuhuda wako.

Mola akupe maisha marefu tujifunze kwako. Amen
 
Yanayofanyika sasa ni marekebisho ya uharibifu uliofanyika awamu iliyopita, kati ya uharibifu huo ni uovu kuvalishwa vazi la uhalali, akili ya watu ilihalalisha mambo mabaya kuwa mazuri. Wizi, madawa ya kulevya, zinaa, matusi, ubinafsi, utegemezi nk kama una akili inayofahamu tulikotoka, tulipo sasa na tunakokwenda huwezi kumbuka zama za uovu ukalinganisha na sasa..fanya kazi!
 
Back
Top Bottom