Mzee Kikwete, leo ndiyo leo; msituangushe

Mzee Kikwete, leo ndiyo leo; msituangushe

Mh. Rais mstaafu Jakaya Kikwette tunayo matumaini makubwa kwenu kuwa ule muda ambao taifa hili limeusubiri mno hatimaye umewadia.

Ni wazi kuwa kila mtu katika nchi hii angalipendelea tuishi sote kwa usawa na haki. Utashi wa viongozi wa juu katika kufanikisha hayo ni jambo la muhimu sana.

Kufanya maamuzi magumu yatakayorejesha imani ya wananchi kwa nchi yao itakuwa jambo la msingi mno kwa sasa labda kuliko jambo lolote lile.

Pana watu wakiwamo watia nia wengi waliojaribu kuutaka urais na kura kuwa hazikutosha hali nafasi ni moja wakiwamo akina:

1. Asha Rose Migiro
2. Mzee Mwandosya
3. Bernard Membe
4. Mizengo Pinda
5. Frederick Sumaye
6. Edward Lowassa
7. Abdulhaman Kinana
8. Philip Mangula
9. Anna Mghwira
10. Dkt. Slaa
11. Dkt. Nchimbi
12. Nk nk

Watu ambao hawakuwamo ndani ya establishment ya sasa au wale waliokuwa na maoni tofauti kuhusiana na establishment ya sasa kwa hakika wangetufaa sana.

JK tupeni raha kwa kuandaa mustakabala mwema utakaotuletea mwanzo mpya.
Aisee mbona unataka kuturudisha kwenye matapishi!! Mbona unawaza pumba kiasi hicho mkulungwa
 
umenikumbusha kauli ya Kingunge Gombale Mwiru aliyoitoa alipoulizwa kuwa "kwanini Serikali inabana Uhuru wa vyombo vya habari?", alijibu kuwa "Uhuru wako(mwanahabari) unaishia pale ambapo uhuru wa mwenzio unaanzia".


In some cases vyombo vya hbari ndiye adui mkuu wajamii
Sio wa jamii ni wa madikteta.
Hayupo dikteta apendae kukosolewa wote ufanana tabia madikteta upenda waandishi kama kina majura mulaga msiba kuimbiwa kwaya asubui jioni.
Kiongozi smart ni rafiki wa vyombo vya habari kwake ni SAwa na kioo, kupitia uhuru wa habari ujikosoa na kuwa bora zaidi,vyombo vya habari utoa kasoro,uibua uozo kupitia kasoro hizo marekebisho ufanyika kuelekea uongozi bora.
 
Makongoro Nyerere anafaa zaidi

Huyu hakuwa karibu na JPM, mtanzania bara na mwana CCM.

Ila kuna mmoja alikuwa nccr zamani baba wa taifa alisema hafai. Ndiyo huyu?
 
Tunataka mwanzo mpya. Utakaotambua nchi ni yetu sote. Utakaotambua tuna janga la Corona. Utakaotambua katiba mpya ni agenda yetu muhimu.

Mwanzo utakaotambua maendeleo ya watu nayo ni muhimu tena zaidi ya maendeleo ya vitu.
Kwan ww mpaka sasa hujatambua kuna korona! Hv mijitu mieusi kama ww kawaloga??
 
Huo ni mfano wa outsiders ndani ya CCM usiyekuwa ya sasa.

Tunahitaji mabadiliko kamili.

Wote hao wanaweza kuwa bora kuliko:

1. Majaliwa
2. Ndugai
3. Simbachawene
4. Chenge
5. Mwigulu
6. Kabisa

Na wa namna hiyo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Hivi hakuna uwezekano akawa ni ndugai? Au wadhifa alionao unamzuia? Tuanzie hapo kwanza maana watu tunamtupia sana jicho bashiru.
 
Na samia asipofanya mnayoyataka mtamchukia..
Bado unataka data za corona?
Mabandiko yangu yote umeyaona? Uzi huu je uliona?


Chatto wazima lakini?
 
Kikwete aliwahi kuuliza "Nimechomeka wapi?"

Hii ni baada ya kuambiwa hachomoi kwenye huu utawala.

Sasa naona kachomoa sasa, umuhimu wake umerudi kwa kasi sana.
 
Na samia asipofanya mnayoyataka mtamchukia..
Bado unataka data za corona?

Ulisikia tunapenda mtu?

Jali maisha ya watu tutakupenda sana.

Wewe baradhuli maisha ya watu huna time nayo. Wa kufa afe wa kuishi aishi. Hatutaki maisha hayo ya bahati nasibu.

Hiyo ndiyo habari yenyewe!
 
Ulisikia tunapenda mtu?

Hali maisha ya watu tutakupenda sana.

Wewe baradhuli maisha ya watu huna time nayo. Wa kufa afe wa kuishi aishi. Hatutaki maisha hayo ya bahati nasibu.

Hiyo ndiyo habari yenyewe!
Ndo maaana nasema MAISHA BILA UNAFIKI HAYAENDI
 
Hivi Afrika huwa kuna kura kutotutosha,nadhani afrika ni Rais aliyopo anataka nani amrithi.
 
Wewe ni Mchawi na Mnafiki ,adui wa Taifa. Yaani unataka Kikwete akuchagulie kiongozi? Wewe una akili kweli? Kama unampenda sana kikwete si ukanywe naye Kahawa? Mafisadi mnaanza kufurahi mkijua mnarudi kuibia wananchi.

Komeo la chuma yaani Magufuli siyo?

Chatto Inc nakusoma. Peleka salamu nyumbani wenye nchi yao wamekuja juu. Walikwazika na mambo mengi mliyokuwa mnawapelekesha wanataka mwanzo mpya.

Kutesa kwa zamu au vipi mkuu?
 
Magufuli hakuletwa na mkwere, huyu mkwere alimtaka Membe!! Jiwe alilijua hilo na ndio maana alimpiga spana asimuinfluence katika maamuzi yake! Acha uongo wako.
Ila aliletwa na mstaafu
 
Ndo maaana nasema MAISHA BILA UNAFIKI HAYAENDI

Kama hatupendi mtu unafiki unatoka wapi?

Wanafiki umewasahau?

Wengine hujawaona wanavaa barakoa sasa baada ya mwenzetu kumkuta ya kumkuta.
 
Mkuu tufanye je VP atakuwa mtanzania bara na kutokea CCM. Hawezi VP kutoka mbinguni.

Vijana ndiyo kama hao. Wazee ndiyo wale. Wapo waliokuwa karibu sana na jiwe na wapo waliokuwa nje. Pia wapo waliowahi kutofautiana naye kimawazo hadharani.

Humo ndimo tunamwomba mzee mkwere kutotuangusha.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Ndiyo Polepole awe VP? mmm haya sawa endelea kumuombea ili nyota yake iendelee kung'aa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom