Mzee John Malecela: Mafisadi wote watakaojaribu kuivuruga CCM watashughulikiwa. Miradi yote aliyoacha Dkt. Magufuli ikamilishwe

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Akiongea na kituo cha runinga cha Azam, leo asubuhi mjini Dodoma, mzee John Malecela amemshukuru aliekuwa raisi marehemu John Magufuli kwa kazi nzito ya kujenga upya mji wa Dodoma.

Mzee John Malecela ambae aliwahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania na balozi nchini Uingereza amemtakia kheri Raisi Samia Suluhu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliulizwa kuhusu maono ya marehemu JPM kama CCM itaweza kuyabeba na kuyandeleza yale yote ambayo ameyaacha.

Mzee Malecela akajibu kwamba marehemu John Magufuli alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM aliahidi kukiimarisha chama cha mapinduzi na kukifanya kuwa chama chenye nguvu nchini.

Akaendelea kwa kusema nguvu ya CCM ilijidhihirisha kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.

Mwisho akatoa onyo kwamba ikiwa kuna mafisadi ambao wana mpango wa kuja kukivuruga chama cha mapinduzi basi anaahidi kuwa watashughulikiwa ipasavyo.

Hayo ni maoni makini ya mmoja wa wazee na waasisi wa taifa hili yaani kwa kiingereza twasema "part of establishement".

Lakini tuchukulie kuwa hilo ni onyo kwa kila mtanzania ambae ana mawazo mengine mbadala ya mawazo ya CCM na dira ya maendeleo 2015-2025.

Wakati huohuo CCM mchana huu wapo kwenye kikao kizito kinachokaliwa na mzee Phillip Mangula.

Katibu mwenezi Humphrey Polepole anatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu yalojiri kwenye kikao hicho.
 
Hahaaa!!!yaani mama Samia ana kaazi jamani sipati picha,dhima alopewa ni kubwaa mnoo lakini naona bado akifanya masihara atapelekeshwaa!!!Yaani huyu mama amuombe sana Mungu tena mnooo!!!ampe hekima na busara maana mbele ni kugumu sana
Mama yetu anakazi nzito sana, kwakweli tumuombe Mungu sana amvushe katika hili, pia ampe hekima na busara ya kuingiliana na watu wote na kuiongoza nchi vyema!

Amina!
 
Ati aliahidi kukifanya CCM kuwa chenye nguvu, kwa kununua wapinzan, kwa wizi wa kura ulokithiri.

Vitabu vya dini vinasema husihibe na kama walituvurugia uchaguz kwa kuiba kura mimi naomba moto wa milele umuanzie mwizi yeyote wa kura pale pale kaburini, shenzi kabisa.
 
Hahaaa!!!yaani mama Samia ana kaazi jamani sipati picha,dhima alopewa ni kubwaa mnoo lakini naona bado akifanya masihara atapelekeshwaa!!!Yaani huyu mama amuombe sana Mungu tena mnooo!!!ampe hekima na busara maana mbele ni kugumu sana
Magufuli licha ya watu kumuona anakasoro fuani fulani lakini Magufuli alikuwa anajuwa kusimamia kile anachotaka kuona kifanyike
Mambo ya mikataba, usimamizi wa miradi ,manunuzi.

Je, mh Samia ataweza kuwa kama JPM?

Au zaidi ya JPM!

Ila tunamtakia kila la kheri aweze fanikiwa

Ova
 
Back
Top Bottom