Huyu jamaa kumbe ni Prof. sasa? Una maanisha Hassan Katalambula? Nakumbuka kuwasiliana naye miaka ya 90 wakati Tanzanet imeanzishwa na kuanza kukutanisha Watanzania dunia nzima.
Katalambula uandishi wake hadi leo nashindwa kujua kama alisoma sana vitabu vya James Hadley Chase au alikuwa akiangalia sana film za kijasusi za USA. Kwa kweli jamaa aliweza sana kutunga kitabu ambacho kingeliweza sana kutokea kwenye mazingira yetu kwa wakati ule. Tofauti na Musiba ambaye aliingiza sana vikorombwezo ambavyo labda kwa leo ndiyo ungelisema vinawezekana na kuwa jambo la kawaida ila si kwa miaka ile.
Nina imani kuna siku atakuja FILM Director mzuri na kutengeneza film yenye hadhi ya KATALMBULA.
Kama jamaa angeliwezeshwa, nisingelishangaa kuwa angelikuwa kachukuliwa Hollywood au Bollywood kuandika film.