I believe Pili Pilipili was and to me is the best Play, yaani ukiisoma ile kitu huwezi weka chini hadi last page, tumepoteza shujaa wengi wa waliobakia ni wale wa kukopi na kupesti hadithi toka kwenye mtandao..... sorry kwa wanaomfahamu vizuri hivi ndie huy huyu alieandika na ile riwaya ya SIRI ya SIFURI???
FARAJ KATALAMBULA KUZIKWA MKOANI TABORA
From: g sengo
Aliyekuwa mtunzi mahiri wa vitabu vya hadithi na riwaya nchini marehemu Faraj Katalambula (kulia) anatazamiwa kuzikwa kesho Isevya mkoani Tabora majira ya saa kumi jioni.
Faraj Katalambula alifariki juzi saa kumi na mbili jioni katika hospitali ya rufaa Muhimbili. Faraj Katalambula ambaye ni mmoja wa watunzi wa vitabu mahiri kupata kutokea atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu kilichosomwa sana cha ' Simu ya Kifo'. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa John Katalambula mwanae marehemu.
Ewe Mwenyezi Mungu ilaze Mahali Pema Peponi roho ya marehemu, Amen.
NB: Nimeambiwa kuwa atazikwa leo huko Isevya, TABORA. R.I.P. Faraj Katalambula.
pole wafiwa
waandishi ndo wanakwenda hivyo...
Pumzika kwa amani F. H. H. Katalambula, nakumbuka sana Riwaya zako; "Simu ya Kifo" and "Buriani" pia na Jarida la Picha "Film Tanzania" na wahusika wake Lawalawa na Mzee Frijala.