Uchaguzi 2020 Mzee Dkt. Slaa popote ulipo

Kwako wewe familia ya Mwalimu Nyerere ni nani na nani?

Mimi binafsi nimewahi kuishi Butiama Mwitongo kwenye nyumba ya Joseph Nyerete. Ninafahamu jinsi familia ya Baba wa Taifa inavyoishi.

Madaraka ndiye amepewa jukumu la kuishi na Mama Maria Nyerere. Ndiyo maana wakati wote Madaraka amekuwa na Mama yake kwenye makazi ya Mwalimu Nyerere. Ukikaribishwa nyumbani na Madaraka maana yake umekaribishwa kwenye nyumba ya Baba wa Taifa, na kwenye nyumba ya Mama Maria Nyerere.

Sielewi hata hoja yako ni nini? Kwa akili yako, unaamini familia ya Mwalimu Nyerere haiwezi kumkaribisha Lisu? Hivi mnaijua ile familia? Mwalimu Nyerere ni mtu aliyechukia ubaguzi kwa dhati toka moyoni mwake, siyo kama maigizo yanayofanywa na huyu Rais wetu. Mara maendeleo hayana vyama, mara mkichagua wapinzani sitawapelekea maendeleo!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndiyo umeniandikia 'Upuuzi' gani huu 'mrefu' hivi?
 
Punguza mihemuko! utakufa na mi sheli bure!! ukweli ni kwamba Lisu ameshamzidi Baba jesca kimbinu!! umeona leo Baba jesca amefuta vitambulisho vya wamachinga!

Sasa kama sio kuzidiwa ninini??

Hoja yako nii ni 'dhaifu' sana hebu jibiidishe Kwanza katika kutafuta 'Maarifa' zaidi na pia 'Kuunoa' vyema 'Ubongo' wako ili nawe una na IQ Kubwa.
 
Alidanganywa na sifa za kutoka kwa watu kama akina Bashite. Hata mtu unaposifiwa, inabidi uangalie mtu anayekusifia. Ukisifiwa na kichaa halafu na wewe ukaamini umefanya maajabu kwa sababu umesifiwa na kichaa, kuna siku utajutia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku kupenda sifa kuliko pitiliza ni dalili ya psychosis jamani. Haiwezekani kabisa wanaume na suti zao wengine na mashahada yao kabatini kila wakiamka wanaimba Pongezi kwa Mheshimiwa Rais wa Awamu ya tano.
 
Tundu Lissu 'amekaribishwa' na Mmoja wa Watoto wa Hayati Mwalimu Nyerere aitwae Madaraka na hakukaribishwa na Familia yake. Msipotoshe!!!
Akalibishwe na mtoto au mzazi kwani kosa liko wapi?
Nyumbani kwa baba wa taifa kwani ni mali ya ccm?
Akili fupi kabisa...
Unapenda kuchochea utengano kuliko umoja..
Awe lissu au wewe au mimi na mtanzania yoyote yule tunahaki ya kukalibishwa kwa baba wa taifa au kwa mtanzania mwenzetu yoyote yule...
 
Dr. Slaa anasuburi tarehe 28 kwa hofu kubwa manake hajui itakuwaje CDM ikishinda, mboga yake ama ugali vyote vyaweza kumwagika siku hiyo.
Siasa hazina urafiki au uadui wa kudumu. Dr Slaa ni msomi mzuri, Rais ajae anaweza kumpatia sehemu itakayomuezesha kutumia ule ubongo kwa faida ya wengi.
 
Dkt. Slaa nakusalimu kwa jina la Bwana wetu Yesu kristo. Naami uko mzima na unaendelea vizuri na uwakilishi wa nchi yetu huko uliko,

Bila shaka unajua na unafatilia jinsi kampeni zinavyoendelea huku!!

Natamani Sana kusikia au kusoma maoni yako kuhusu kampeni zinavyoenda huku! Ujengaji wako wa hoja ndio ulionishawishi hadi nikawa mpenzi wa siasa!

Natamani Sana kusikia maoni yako, kuhusu kijana wako Tundu Lisu!

Unasemaje kuhusu familia ya Mwl kumkaribisha Tundu Lisu nyumbani kwao?? unalisemeaje hili?

Tafadhali mzee wangu, sema japo kidogo! tusahau ya mwaka 2015! Hata mimi sikufurahi jinsi ilivyotokea!

Kwani wewe tayari ulishakuwa funguo za kufungulia kufuli.
Butiama panaruhusiwa kwenda kwa kila Mtanzania Na wasio watanzania, bila kujali chama, hata Lowasa aliwahi kwenda huko! akapokelewa vizuri, akala chakula hapo hapo.
 
Akalibishwe na mtoto au mzazi kwani kosa liko wapi?
Nyumbani kwa baba wa taifa kwani ni mali ya ccm?
Akili fupi kabisa...
Unapenda kuchochea utengano kuliko umoja..
Awe lissu au wewe au mimi na mtanzania yoyote yule tunahaki ya kukalibishwa kwa baba wa taifa au kwa mtanzania mwenzetu yoyote yule...

Another Fool!
 
Back
Top Bottom