Mzee anayetrend huko mitandaoni ni nani?

Mzee anayetrend huko mitandaoni ni nani?

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
11,718
Reaction score
27,812
Mwenye kumfahamu

USSR
Screenshot_20241113-111650.jpg
Screenshot_20241113-111629.jpg


======
Zimekuwapo Picha na video zikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonesha mzee akiwa anasaidiwa kutembea huku kila mtu akieleza lake lakini wengi wamekuwa wakizungumzia kuhusu umri wa mtu huyo huku wengine wakisema kuwa ana miaka 300.

Video mojawapo ilizua gumzo katika mtandao wa X zamani ikujulikana kama Twitter ambapo mtu mmoja aliweka video ya mtu huyo na kuandika kuwa

“This Indian Man has just been found in a cave. It’s alleged he’s 188 years old. Insane” akiwa na maana kuwa mwanaume wa kihindi amekutwa kwenye mapango huku akikadiriwa kuwa na miaka 188.

Ukarasa wa instagram wa redio ya TimesFm walichapisha pia video kama hiyo huku wakidai kuwa

“Wakati ukijiaminisha kwamba umeshaona maajabu mengi. Kupitia sayansi ya Mmarekani au Mjapan. Utakuwa unajidanganya. Hapa kutana na binadamu mwenye umri mrefu zaidi katika dunia hii ya sayansi na tekinologia. Mwamba huyu hapa amemeza miaka 300 hadi sasa na anadunda kama kawa. Anatokea katika taifa la India. Sayansi ya Mungu inaendelea kukitunza kiumbe hiki kikiwa bado hai”

Mtu huyo anayeonekana katika video hizo ni mkazi na raia wa India anayetambulika kwa jina la Siyaram Baba. Makala mbalimbali zimemuelezea Siyaram Baba kama miongoni mwa watu ama kiongozi wa Kiimani katika jamii yake.

Tovuti ya mathrubhumi imeandika kuwa Siyaram amejitolea maisha yake ili kutumikia imani yake na kutoa mafundisho kuhusu imani hiyo. Amekuwa akitumia muda mwingi pia kusoma maandiko ya imani yake, bila hata kutumia miwani licha ya umri mkubwa alionao. Amekuwa akiishi maisha ya kawaida tu, huku akifanya kazi zake nyingi peke yake licha ya umri wake kuwa mkubwa. Watu wengi wamekuwa wakienda kwake kupata ushauri na baraka kutokana na kuisimamia imani.

Suala la miaka aliyonayo Siyaram limekuwa changamoto kwani kila mtu amekuwa akitaja miaka tofauti, mathalani tovuti ya TimesNow wameandika kuwa umri halisi wa Siyaram haufahamiki ila inakadiriwa kuwa ana miaka zaidi ya mia moja.

Chapisho lililowekwa kwenye mtandao wa X lililodai kuwa Siyaram ana miaka 188 lilipingwa vikali na watu mbalimbali kwa kusema kuwa mtu huyo hajafikisha miaka 188, huku mtandao wa X wao wenyewe kupitiaX communitywameeleza kuwa taarifa hiyo si sahihi na inakadiriwa kuwa Siyaram anakadiriwa kuwa na miaka 109 ama 110.
 
huyo ni mzee mwenye umri mkubwa kwa taarifa zilizopo........duniani alikuwa akiishi pembezoni na mji kwa kujitenga ndo watu wakamuibua india
 
Back
Top Bottom