Mzazi: Epuka haya katika malezi ya mtoto wako

Majs

Senior Member
Dec 21, 2012
190
500
Nimeyakusanya maradhi ya malezi katika ulimi kwenye "Maneno Aina Kumi" yanavunja moyo watoto na yanawahamasisha kupotea, nayo ni kama yafuatayo:

  1. KUTUKANA: Kwa kumpa mtoto sifa za wanyama (punda/mbwa/ng'ombe/mbuzi/ewe mnyama/......) au kuitusi siku aliozaliwa.
  2. KUMDHARAU: Kwa kumkejeli kwa sifa hasi (negative) mfano: Wewe (muovu/muongo/ mbaya/ unatisha /mnono /kiguru /mwizi).... na dharau ni kama kaa la moto inachoma moyo.
  3. KULINGANISHA: Na hii inaharibu utu wa mtoto (personality), kwa sababu kila mtoto ana uwezo wake na vipawa vyake tofauti na mwengine, na kuwalinganisha kunamfanya ahisi ana kasoro, na kunaua kujiamini (self confidence) kwake, na kunamfanya amchukie anayelinganishwa naye. Katika ujuzi niliyopata katika kutatua matatizo ya malezi, niligundua kuwa kitu ambacho sana kinasaidia kupotea kwa watoto ni (utumizi mbaya wa matamshi na maneno). Na kutoka siku mbili nilikaa na kijana aliyetoroka nyumbani kwao nimsikilize tatizo lake la kimalezi na wazazi wake na mwisho wake ilikuwa ni (maneno mabaya) ambayo anayasikia kutoka kwao! Na msichana alinilalamikia kupotea kwake hali akiwa nafsi yake hairidhiki, lakini alitaka kulipiza kisasi kwa wazazi wake (kwa maneno yao mabaya).
  4. MAPENZI YA MASHARTI: Kama kushurutisha mapenzi yako kwake kwa kitendo maalumu, mfano (mimi sikupendi kwasababu umefanya kadha / nitakupenda ukila kadha au ukifaulu au ukidurusu),, mapenzi ya masharti yanamfanya mtoto ajihisi hapendwi na hatakiwi. Na akikua anajihisi kama hayumo kwenye familia kwasababu alikua akichukiwa alipokua mdogo, na hii ndio sababu watoto humpenda babu na bibi sana kwasababu mapenzi yao si ya masharti.
  5. UFAHAMU WA MAKOSA: Mfano (mwanamume halii / nyamaza wewe bado mdogo / mtoto huyu amenitia wazimu, mimi simuezi / ALLAH akulipe na akuchome na moto).
  6. KUKEJELI: Mfano (wewe huelew i / nyamaza ewe shetani / huna faida yoyote)
  7. UTISHIAJI WA MAKOSA: ( nitakuvunja kichwa chako / nitakunywa damu yako / nitakuchinja)
  8. KATAZO LISILOKINAISHA: Kama kukariri La! La! La! (Hapana!!! Hapana!!! Hakuna!!!! Haiwezekani!!!) daima unakataa matakwa yake na huelezi sababu!
  9. KUMUAPIZA: Mfano ( Mungu akutwae/natamani ufe / maluuni (umelaaniwa).
  10. KUMFEDHEHISHA: Na ni kwa kutoa siri zake na mambo yake ya kibinafsi (ya ndani).! Haya mambo kumi kamili..... Na nimefanya utafiti unaosema kuwa mtoto katika umri wa 'teenage' anakuwa ameshasikia kutoka kwa wazazi wake maneno 16000 mabaya.. Fikiria mtoto hajafikia miaka minane na katika kamusi yake ana zaidi ya maneno mavunjifu 5000, kwahiyo athari yake kwake itakua zaidi ya silaha hatari na yatavunja maisha yake na utu wake....,,,, Insha a Allah tujitahidi na hayo yote yaliyotajwa ijapokuwa saa nyingine mzazi huwezi kujizia kwa ghamu ya mtoto kwa matendo yake. MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.
Makala ya Dr.Jaasim yameandaliwa na Amour Al Habsi

Mtoto.gif
 

bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,191
2,000
mtoto umleayvo ndivyo akuavyo, ukimlea kimayaimayai......kiubishi....n.k.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom