Malezi ya mtoto baada ya kuachana yana changamoto zake

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
174
618
Heloe JF,

Kuna kitu napitia kizito kidogo, Mimi ni binti wa makamu nilibahatika kupata mtoto, lakini kuna maugomvi ya hapa na pale yalisababisha kuachana na baba mtoto, mtoto alichukuliwa na ndugu zake upande wa kiume.

Sasa karibu shule zinafungwa nazani baba ake atamchukua kwaajili ya likizo, baba ake tayari ana maisha mengine,ana watoto wawili kwa sasa na anaishi na mke wake, sasa na Mimi nahitaji kumuona mtoto.

Siwezi safiri kwenda kumuona mtoto kwasababu ya majukumu ya kazi yaani uko alikochukuliwa(ndugu upande wa kiume), kama mnavyojua kazi za serikali izi na Mimi mwanaume niliyenaye yupo kikazi mkoa Fulani.

Sasa uyu baba mtoto kaniambia tukutane mkoa Fulani ili na Mimi niweze kumuona mtoto Nina miaka kama miwili sijamuona uwa nawasiliananae kwenye simu tu.
 
Wacha wee... unaendelea au bado?
Anyway, nenda kakutane nae ukiwa umeongozana na huyu "bebi" wako mpya maana hamchelewagi kukumbushia.
La sivo ukijipeleka mwenyewe mtoto utamuona lakn ukirudi huyu jamaa mpya amesepa na kijiji
 
Kamuone mtoto kuhusu maswala ya kulala wapi gesti na hotel zipo nyingi utatafuta wewe ukalale au mlale wote yeye mtoto na wewe
Angalizo huyo jamaa anataka akumbushie ukilegea unajiharibia mahusiano yako mapya ukikataa pia kumuona tena mtoto Mara nyingne itakuwa mtihani
 
Back
Top Bottom