Nilianza kuwa na adabu Ile siku niliyoona engine ya Benz ikiwa imebebwa kwenye mkokoteni inaenda kuuzwa kama skrepa.
Niliogopa pale msiba wa yule tajiri kaburi lake kuchimbwa na wale vijana wanaoitwa wezi na masela wa mtaani.
Nilipata mashaka pale dereva mzuri mwenye mbwembwe alipokufa kwa ajali kwenye Kona aliyoizoea.
Nilijifunza pale binti mdogo alipoolewa na mzee ili arithi mali, ajabu akatangulia kufa yeye..
Niliogopa pale hakimu aliyedhurumu haki za watu, na yeye alipata kesi isiyo na dhamana..
Maisha yakikupa ukubwa, chagua kuwa mnyenyekevu🙏