Dada, uamuzi unao mwenyewe huu ushauri wa humu JF, unaweza kukujenga au kukuharibia zaidi. Fikiria afya yako, maana hujui huyo nyumba ndogo kama ni mwaminifu kwa mmeo tu or not, lakini pia fikiria watoto. Mtu asikudanganye, kuna tofauti kubwa sana kati ya watoto waliolelewa na mzazi mmoja na wale wa wazazi wawili.
Na zaidi ya yote kumbuka kwamba mkiachana inaweza kutokea kwamba baba akataka kubaki na watoto wake, na wakalazimika kulelewa na mama wa kambo. Au hata wewe unaweza kuja kushawishika kuolewa na mme mwingine na watoto wako wakalelewa na baba wa kambo ambaye kwa hakika hujui atakuwa ni mkarimu kiasi gani kwa watoto wako. Angalia Mkanda wa suicide mission. Pengine utajua ni kwa kiasi gani kutengana kwa wazazi kunavyoweza kuathiri watoto, na mkajikuta mna watoto machokoraa!
Muombe Mungu sana ambadilishe mmeo, na zaidi ya yote, omba Mungu awajalie afya njema. Wanaosema usijali suala la watoto inawezekana hawajui ukweli juu ya athari ya watoto kulelewa na single parenti au mzazi wa kambo. Kwa maana ya kwamba whether watoto watabaki na wewe au na mmeo, bado kuna uwezekano kwamba mmojawapo kati yenu akaamua kuoa au kuolewa tena. Sasa katika mazingira hayo fate ya watoto ni lazima ifikiriwe. Nimeona wanandoa wengi wanaoishi nyumba moja lakini hawalali kitanda kimoja, nia ikiwa ni kulinda mustakabali wa watoto.