In detail report kuhusu myus.com:
hawa ni kama host couriers ambao wanakufadhili kwa kukupa anuani marekani,anuani ambayo sasa unaweza kununua bidhaa kwa muuzaji (seller) yeyote wa ebay,amazon na hata official sites kama apple,dell na nyinginezo. unapokuja kwenye kujaza anuani ya manunuzi na usafirishaji(shipment address/address) unajaza anuani ambayo umepatiwa na myus.com.. kitakacho fanyika ni mzigo wako unakwenda kwenye address ambayo ulipewa na myus.com na wenyewe watakujulisha kwa njia ya email au simu na kukuuliza ni kwa njia gani ungependa mzigo wako ukufikie,wenyewe wataingia gharama kukusafirishia mzigo wako na watakukata automaticaly kwenye account yako(hadi uverify lakini) na mzigo wako utakufikia saafi kabisa..hivyo hawa jamaa ni salama na wako certified na wana fanya hii huduma kwa muda mrefu sasa
vyakuzingatia ni hivi:
-utajaza fomu ya registration ambayo utaandika anuani yako na sehemu halisi uliyopo,hakikisha una kadi ambayo imewezeshwa kufanya malipo ya mtandaoni(e-banking,online purchases almost bank zote zinafanya kasoro NMB)
-utakatwa kiasi cha dola 10$,kama registration fee
-tunza password yako na suite namba ambayo ni kama username yako(muhimu sana)
-KUMBUKA kuwa anuani yako ya manunuzi sasa itakuwa ni hii ya myus.com na sio hii ya bongo hivyo nenda kwenye profile yako ya ebay au mtandao wowote unaofanyia manunuzi na uibadili address yako kuwa hii ya myus.com
-kumbuka kuangalia email yako na simu yako kama umeshanunua kitu kwa kutumia myus kwasababu watakutafuta uverify shiping method ya kuja kwako
-sasa unaweza kununua chochote kokote duniani kwakuwa tayari una address ambayo inaeleweka na ina julikana ilipo
my fellow Geeks nawashauri msiogope haya mabo wala msisite kwasababu kuna waoga wachache wanafanya mabo yaonekane ni magumu kwa wote kaajili ya woga wao,jaribu na jaribu,uliza ukishindwa na usisahau kuwa MAKINI MNO. usikurupuke maana haya mambo yanataka uchunguzi kidogo.
kwa upande wangu nimeagiza earphone original kutoka applestore( sio ebay nazungumzia mtandao official wa apple) na wamecomfirm mzigo utafika kesho jioni kwenye address yangu ya myus.nitazidi uwapa data ndugu zangu.,
leteni maswali (though sipo online muda wote)
tembeleeni hii website ya MYUS.COM kabla hamjauliza maswali wakuu.jionee kwanza ukikwama leta hoja tulijadili wote.sote ni wageni kwa haya mambo
joe out...