My experience baada ya kumaliza chuo kikuu

My experience baada ya kumaliza chuo kikuu

Hi wana jamii forums
Niseme tu it's an honor kupata jukwaa kama hili la kushare life experience.
Kipindi chote nasoma chuo,jijini dizim nilipanga toka niko first year kuwa nikimaliza tu,I will go back to where I came from.

So baada ya kukabidhi kitabu changu (dissertation )nilifunga mabegi yangu tayari kwa safari. Mizigo iliyokuwa mikubwa nilipeleka kwa mama yangu mdogo aishiye Tabata;tukakaa, tukapika tukala then nikamweleza azma yangu ya kurudi nyumbani.Nakumbuka aliniuliza mbona mapema sana?Nilimjibu nisipoondoka sasa ;sintaondoka wacha nende,isitoshe bibi na babu wamenimisi sana nami nimewamisi,wacha nikawasalimu then ntarudi.Ilikuwa Ijumaa.

Nilikuwa nshakata tiketi kabisa ya basi,alfajiri na mapema nikafika ubungo nikapanda basi kwenda kaskazini. Nikiri mimi si wa kaskazini ila maisha yalifanya wazee wangu wakafika kaskazini na kujenga mji.Saa 12 jion nilikuwa kaskazini.Nikapokelewa kwa furaha na bashasha na ndugu na majirani.

Mwezi mmoja baadae nilikuwa busy kila nikiamka nazunguka kwenye maofisi mjini pale nikipeleka cv na kuomba kazi.Wakati huo huo kuna ofisi moja ya kanda nikaenda kuomba kujitolea kwa mambo nilosomea. Mama yule ,Mungu ambariki sana alinambia sawa naweza jitolea ila hana fungu la kunilipa chochote.Nikamwambia mama usijali uzuri natokea nyumbani,haina shida nahitaji kujifunza kazi tu.Walinirusuhu nifanye asubuhi hadi saa 6 mchana then wakawa wananiruhusu nirudi nyumbani.Basi ikawa baada ya saa 6 naenda shinda stendi nikiangalia kama kuna fursa gani nifanye.kila mara nilikuwa najiambia sikusoma nitaabike stendi huku,this is not my place.But nilikuwa nakaa pale stendi toka 6 mchana hadi 12 jioni then narudi nyumbani.

Baada ya mwezi sehemu nilizopeleka barua wakaniita walihitaji mtaalamu,kwa mshahara wa laki 5,jijini Arusha nikakubali.kwani sikuwa na jinsi. Nikaenda nikafanya kazi kama miezi 3,then wakawa na project mwanza wakanipeleka,wakanilipia chakula ,hotel,malazi na mshahara wangu wa mwezi.Nakumbuka nilikaa mwanza miezi 3.Mungu huyu,nilipiga hela sana,si wajua tena mwanza kina ngosha wahana hiana. Nilinenepa hataree.

Project ilipoisha nikarud arusha,nimekaa kama mwezi utumishi wakaita watu kwenye interview,nilikuemo,nikafika na kufanya usaili.Mwaka ulofuata nikaingia serikalini rasmi,yes private kulikuwa na hela sema job security ilikuwa ndogo. But nawashukuru coz they got me wakati sina mbele wala nyuma.

So for any graduate out there usikate tamaa. Saa yako yaja.It's just the matter of time.haimaanishi maisha tumeyapatia,no but tunapata mkate wa kulisha family na siku zinasonga.Jipe moyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna kitu wewe unakimbia private kisa eti "job security" kwanini usitegeneze security mwenyewe kwa huo mshahara.....mimi naona wewe ni kijana alie dekezwa na single maza na baba wakambo.....utakufa masikini na hiyo job security yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii story yako unamaanisha watu wakimaliza chuo waende kwao mapema..na wakakae stendi? Story yako ni nzuri sana Ila hukupaswa kuzunguka kote huko!! Habari ya sijui "Mimi sio MTU wa kaskazini, Mara wazazi walijenga, Mara nikaenda stendi" haikuwa na ulazima kikubwa ungewaeleza wahitimu wa vyuo kuwa wapambane baada ya kumaliza na wawe wavumilivu watafanikisha ndoto zao kama wewe...hiyo pekee ingetosha!
 
huu uzi ni saws na majivuno hauna jipya, tena umeficha mambo sijui kwa ajili gsni, yaan kila ulipoomba ulipata direct! ni saws, Umekutana na ganda la ndizi halafu unawashauri wenzako wavumilie kuburuza miguu, Uzi wako hauna uhalisia, au huenda ni Uzi Wa miaka ya 90 lakini Leo ndo umeupost humu. Huu Uzi ni yaleyale ya GPA ya 32 ya Injiniaringiiii!!!!!!!!
Mkuu acha kejeli
Mtu kaamua ku share na sisi emu muache mi sijaona majivuno ya mleta mada
Afu kuhangaika na maisha sio mpaka ichukue miaka 20 hata mwaka mmoja tu unatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si ndo hapo
Huo muda nilokaa mtaani nilipigika hatare
Nilikuwa nakosa hata nauli ya kwenda napojitolea

Sent using Jamii Forums mobile app
Good morning Iron Butterfly... Nmetafakar leo alfajiri neno "Iron" umelitumia kujieleza kua wee nimwanamke uwezae kusimma pekee, maisha yako unayaendesha mwenyewe, awepo mwanaume nyuma asiwepo bado yataenda.

Neno "Butterfly" umelitumia kujieleza namna ulivyo mzuri, mtamu mtamu , sura na umbo vyote vzuri .


[emoji4]
 
Back
Top Bottom