My confession: Hornet is Positive

Status
Not open for further replies.

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
26,119
49,492
Habari zenu wote?

Siku kadhaa nyuma nimejikuta kwenye wakati mgumu mno. Hivi karibuni niliwiwa kwenda kupima kama sehemu ya kuifahamu afya yangu,

Majibu yangu hayakuwa ya kufurahisha, nilichanganyikiwa na nikajichukia mno. Nikajutia nyakati zote za kukutana bila kinga na kujikuta nimechukia sex mnoo.

Ila baada ya kumweleza rafiki yangu alinipa moyo na nipo naendelea kuishi kwa matumaini.

My take ;
Usimpime mtu kwa macho.
Tutumie vipimo tutumie kinga.

#lets stay positive.
 
Dah we mrembo mjanja sana. Unanifukuza kijanja sio? Mi siogopi wala nini, mtongozo uko palepale.

HIV sio ugonjwa
HIV sio kifo
HIV ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Usiingiwe na hofu ukikutwa HIV+
Ishi kwa matumaini... kula vizuri, pumzika vya kutosha, mazoezi ya wastani, fuata ushauriwa wataalam wa afya.. Hakika utaushuhudia uzee wako ukiwa na afya yako njema kabisa

Tuko pamoja mrembo wangu,hakuna unyanyapaa wala nini.
 
Dah we mrembo mjanja sana. Unanifukuza kijanja sio? Mi siogopi wala nini, mtongozo uko palepale.

HIV sio ugonjwa
HIV sio kifo
HIV ni upungufu wa kinga mwilini. Usiingiwe na hofu ukikutwa HIV+
Ishi kwa matumaini... kula vizuri, pumzika vya kutosha, mazoezi ya wastani... Hakika utaushuhudia uzee wako ukiwa na afya yako

Tuko pamoja mrembo wangu,hakuna unyanyapaa wala nini.
Nashukuru pia nimefanikiwa kwa kiasi Fulani kuhandle yoga na hofu ndani yangu.

shukrani
 
Hongera sana

Kwanza kwa kuijua hali yako lakini pia kwa kujikubali.

Ni heri sasa utajua namna ya kutunza afya yako vizuri.

Hali hiyo haitishi kama zamani, kuwa na furaha vile vile, hakuna jipya kabisa
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom