mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,966
Wakuu,nikiwa natimiza miaka kadhaa siku ya leo,nina furaha kubwa maishani mwangu.Pamoja na malezi ya watu wangu wa karibu,Watu wote wa Jf,wake kwa waume mmeyabadilisha maisha yangu.Ni mizigo mingi nimetua hapa na kupata ufumbuzi.Ni masahibu mengi nimepata lakini hapa limekuwa jokovu la faraja.Nawashukuru nyote na ninawapenda sana.Mungu awabariki nyoote na kuwajalia kila hitaji muwekalo mbele yake.Ujumbe wangu kwenu ni kuwa:MUNGU ATABAKI KUWA MUNGU.