Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala katika JamiiForums

Status
Not open for further replies.
Lugha chafu na matusi vimetamalaki katika mijadala mbalimbali hasa ya kisiasa. Naomba idhibitiwe maana inalivunjia heshima jukwaa letu tukufu.
 
Shukran sana kwa mwongozo huu. Angalau ni muhimu kukumbushana.

Until then ...
 
Asanteni MODS kwa kutukumbusha maadili yanayotakiwa katika ukumbi huu wa JF. Mojawapo wa vitu ambavyo sikuvifurahia ni ile Na.12 kuhusu mtu anayeingiza vitu nje ya mada inayojadiliwa. Mnasema mnamezea tu pamoja na kuona kasoro hiyo. Hii si sahihi. Inafanya watu waache kuchangia mada hata kama walikuwa na hoja nzuri. Pendekezo langu ni kwamba bandiko ambalo liko nje ya mada ya uzi lifutwe moja kwa moja.

Mchangiaji huyo anaweza kuanzisha uzi wake akajadili mada yake. Siyo kumchafulia mwenzako ambaye anazungumzia vitu tofauti. Mfano amabao umekuwa ukijitokeza mara nyingi ni mtu atakuwa anazungumzia kitu fulani, kama ugonjwa wa korona au treni ya SGR. Mchangiaji mwingine, ambaye hana hoja ya kuchangia hapo, anakuja na swali 'Vipi zile trilioni 1.5?'

Au mtu ameanzisha mjadala kuhusu 'interchange' ya Ubungo. Mwingine anadakia 'Vipi zile milioni 40 kila kijiji? Kama una dukuduku na hoja hizo, anzisha uzi wako uweke hoja zako ambazo watu watazijadili. MODS futeni michango kama hiyo mara moja na kama mchangiaji akirudia tena apewe 'ban'. Hii ndiyo itabakiza jukwaa hili kuwa 'Forum of Gret Thinkers' na majadiliano kuwa ya maana.

Kitu kingine ambacho sikubaliani nacho ni Na.15 kuhusu saini na avata zinazotumika. Ni sawa kutuacha huru tuchague jina au sahihi au avata gani tutumie. Kuna nyingine mnaweza kuingilia kati kama mnaona hazifai. Mfano wa saini moja ambayo hainifurahishi ni ile ya mchangiaji mmoja inayosema "Miafrika ndivyo tulivyo".

Mada aliyokuwa akiijadili mchangiaji inaweza kuwa nzuri sana na haina chochote kuhusu bara letu la Afrika. Kwa nini tujidhalilishe bila sababu? Hata kama kuna mwenzetu amefanya kitu cha ajabu, usitujumlishe Waafrika wote kwamba hiyo ndiyo kawaida yetu. Huenda tupo wengi ambao hatukubaliani na hayo aliyoyafanya mwenzetu huyo. MODS wawe huru kuchukua hatua wakiona vitu vyenye utata kama hivi.
 
Nahisi kama nimeandikiwa mimi, kwaio hizo ndio sheria na masharti?
 
Boss; Kama unafahamu jukwaa hili limekuwa na watumiaji kulingana na mapenzi yao kwa maana wapo wanaopenda jukwaa la siasa, wapo wamichezoni, wapo wa habari na Tupo sisi wamatangazo yaani matumizi yangu ni matangazo kuliko nyuzi zingine si mfatiliaji sana.

Sasa; katika haya matangazo uko post mara moja ads itaonekana kisha itatokomea kwenda huko katika kurasa za mbali kiasi kwamba wapitiaji wengine watakosa kuona hiyo ads na hawanan muda wa kupekua page za mbele Swali? je nifanye nini ili ads yangu irudi juu na ionekane tena pasi na kukiuka amri ya kurudia rudia.

Shukrani!
 
Na sisi raia tunaruhusiwa kuwashughulikia hawa walinda maudhui (ma-mods) kwa namna gani? Wengi wamezidisha uonevu eti unaandika "Jiwe" yeye anakulazimisha huo ni mhimili wa Rais, tuna Rais anaitwa Jiwe hapa nchini?
wanajaribu ku legalise hayo majina indirectly...
 
JamiiForums is a User-Generated Content...

No moderator, admin or anyone should interfere with a content that a user has generated. Utaratibu wa kuchukua posti ya mtu (kuanzia heading mpaka yaliyomo) na kuibadilisha, na kisha kuiacha kana kwamba huyo user ndivyo alivyoandika, ni intellectual dishonesty, na inaingilia moral-rights za mtu.

JamiiForums admins should either, delete a content, or move it to a post in the same sub-forum it was posted. But not changing the original text and insinuate it was originally posted as such.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom