Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala katika JamiiForums

Status
Not open for further replies.
Hapo No7 kwenye kuwapuuza wanachama wasumbufu umeongelea kuhusu ignore. Naomba mpafanyie maboresho kidogo ukim-ignore mtu usipate notifications zake kabisa.

Mfano, kuna mtu nimem-ignore nikajua tatizo limeisha ila aki-like post zangu napata notifications.
 
Mkuu Maxence Melo kuna uwezekano wa kufuta hii ID, nataka kubaki na ID yangu yenye jina halisi (ninayo).
Kwa sasa sioni sababu ya kuwa na ID mbili kwa sababu hata ban nina miaka mitano sijapewa.
 
Aidha, epuka kutumia herufi kubwa (CAPS), hati mkolezo au hati mlalo katika andiko lote.
Sir na-enjoy kufanya haya kuliko mnavyoweza kufikiri msitupangie to that extent sasa.
.
Kuhusu adabu kwakweli adabu JF members tuna zero na nusu 😊 vikero kero vingi automatically heshima inaponyoka.
 
Hapo No7 kwenye kuwapuuza wanachama wasumbufu umeongelea kuhusu ignore. Naomba mpafanyie maboresho kidogo ukim-ignore mtu usipate notifications zake kabisa.

Mfano, kuna mtu nimem-ignore nikajua tatizo limeisha ila aki-like post zangu napata notifications.
Tafadhali soma hapa: Ignore list on JamiiForums: Maboresho ya mwaka 2020

Ni kuwa tunachofanya ni kuwashirikisha, mkitaka jambo tunalifanyia kazi ingawa inaweza ikachukua muda kidogo.

BTW, kama unatumia browser utaona kuwa kuna options zaidi zimeongezwa kwenye editor mfano X[SUP]2[/SUP] + Y[SUP]2[/SUP]
 
Mkuu max hili bandiko ungeliweka kila jukwaa kwa leo maana kuna watu hupitia jukwaa moja au mawili na pengine hapa huwa hawapiti kabisa ,mwingine unakuta anapenda kuongia mmu tu kwa miezi na zaidi

Ishu ya kupata notification za mtu uliyemignore nalo mlifanyie kazi tusipate kabisa
 
Asante sana mzee; mimi naijua sana miongozo hii kwani ni ya kawaida sana katika majadiliano ya kistaarabu. Ila kuna watu wanafanya hapa kama kijiwe cha wao kuondolea frustration zao kwa kutoa matusi na kuandama wachangiaji wa yale ambayo hayawafurahisi badala ya kujifunza kwa nini hawakubaliani.

Mijadala yote duniani hufungwa kwa consesus fulani lakini mijadala inayofanikiwa ni pale kila upande wa mjadala unajitahidi sana kufahamu upande wa pili na kujua tofauti zao ziko wapi.
 
Sijajua kwenye avatar iwapo mtu atachukua avatar well known ya member mwingine inakuaje?..
Au zile I'd zinazochanganya..
Mfano mtu ajiite [SUB]maxence mmelo ..mnafanyaje?[/SUB]
 
Na sisi raia tunaruhusiwa kuwashughulikia hawa walinda maudhui (ma-mods) kwa namna gani? Wengi wamezidisha uonevu eti unaandika "Jiwe" yeye anakulazimisha huo ni mhimili wa Rais, tuna Rais anaitwa Jiwe hapa nchini?
 
Sijajua kwenye avatar iwapo mtu atachukua avatar well known ya member mwingine inakuaje?
Ukimwona tuarifu, tutaangalia aina ya avatar na nani alianza kuitumia. Then wa mwisho ataelezwa kistaarabu kuwa achague avatar tofauti (kama wote ni active members

Au zile I'd zinazochanganya..
Mfano mtu ajiite [SUB]maxence mmelo ..mnafanyaje?[/SUB]
Ndo maana kuna mfumo wa kupitia waliojisajili; ni nadra sana kukuta mkanganyiko wa majina. Mkibaini watu wa aina hiyo tuarifu tufanye maamuzi haraka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom