Mwongozo wa kuvunja laana

Mwongozo wa kuvunja laana

Ni Neema ya Bwana Yesu ujifunze somo hili ili ikiwa wewe ni muhanga wa laana uweze kujinasua kutoka katika laana na ukaishi maisha yaliyo katika mapenzi ya Mungu yaani Baraka za Mungu

Laana ni nini?
LAANA ni kinyume cha Baraka ZA MUNGU.

VYANZO VYA LAANA ni hivi :
1. Laana za ukoo
Hizi ni laana zinazowapiga watu wa ukoo wenye kuamini na kuabudu mizimu kutokana na maovu ya koo zao zilizotangulia , hizi zinapita hadi kizazi cha tatu na nne na. Kuendelea

2. Laana tunazojiletea kwa matendo yetu wenyewe
(I) Ushirikina
Pale mwanadamu anapo amini na kuenda kwa wachawi au waganga wa kienyeji anafanya agano na shetani, na kutoa sadaka ya damu yake kwa kuchanjwa chale aua ya mnyama, ananunua mapepo,unaweka imani juu yao na kuzini nayo ambayo mwisho yanakutesa, na unajiweka wakfu kwa mashetani

(II) Uhusiano na dini za uongo
zimpingazo Yesu au kutafuta maarifa kwa njia ya mapepo, kama kuamini nyota, kusoma mikono,kuabudu sanamu.

(III) Kumwaga damu isiyo na hatia kama vile kuua, kutoa mimba na kuua kwa ushirikina (mwanzo

(IV) Uzinzi na uasherati.
Hii ni kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa au kabla ya ndoa.

Waebrania 13:4 ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu

Pia ndoa za jinsia moja(ushoga /usagaji) au mnyama.
Walawi 18:22-23
Usilale na mwanaume mfano wa kulala na mwanamke, ni machukizo, wala usilale na mnyama yeyote ili kujitia unajisi kwake, wala mwanamke asisimame mbele yake ili kulala naye ni uchafuko.

(V) Maneno ya kinywa chako.
Mithali 18: 20-21) Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake , pia atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake.

Pia Mithali 6:2 Basi umetengwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako.

HATUA ZA KUVUNJA LAANA
1. Mkiri Yesu Kristo kuwa ndiye Bwana na Mwokozi wako.

Warumi10:9-10) kwasababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwa kuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka, kwa maana kwa moyo mtu huamini na kupata haki na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu.

2. Tubu dhambi zako zote na kupokea msamaha kutoka kwa Mungu kupitia damu ya Yesu Kristo.

3. Wasamehe wote waliokukosea Marko 11:25.

4. Ukatae uhusiano wa shetani juu yako kwa kufuta kwa damu ya yesu Matendo 19:18-20.

5. Futa jina lako katika maagano ya giza na kuvunja laana zote kwa kunyunyiza damu ya Yesu Kristo wa Nazareth 2 kor 5:17.

6. Kemea kwa jina la yesu pepo linalotumia lango la laana kukuadhibu.

7. Fungua milango ya baraka kwa Damu ya Yesu kupitia jina Yesu Gal 3:13-17.

8. Anza kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwa kufuata mapenzi yake yatakayokufanya umjue yeye sana.

Biblia ina sema " Mjue sana Mungu ili uwe na amani maishani mwako, ndipo mema yatakapo kujia" kumbuka mema ni baraka za Mungu kwako.

NB: Kwa kuifanya nyumba yako kuwa madhabahu ya Bwana utashinda hakika pasipo kuwategemea mitume na manabii wa michongo, Mtumainini Mungu pekee.

Jina la Bwana Yesu litukuzwe,
Utukufu kwa MUNGU.
Watu wanaoongoza kwa kuamini kwamba;
1. wanarogwa sana
2. Wana laana sana
3. Mapepo yanawafuata sana

etc
NI WALOKOLE
 
Kwann hatuifagilii mizimu shida ni kwamba mizimu haitaki maendeleo,hofu watu wakiendelea wataacha kuabudu mizimu.
Ukiwa na maendeleo utawapeleka watoto shule bora watapata elimu na connection wakipat maisha bora hawawezi tambika mizimu wakitegemea Elimu zao.Mizimu inaendana na umasikini.Elimu ni adui wa mizimu SAwa na dini.
Waafrika wengi wapo jinsi walivyo kwa sababu maisha yao yapo connected na mizimu na mizimu ndio inazuia maendeleo.

Nimekuelewa
 
Leo nilikua naongea na msukuma mmoja akaniambia sisi wasukuma ni matajiri kwasabu hatuachi mila!
Tuna dini lakini lazima tufuate mila dini haiwezi kunifanya niache mila na mila hainifanyi niache dini

Kwamba naweza kuoa wanawake sita na nikajenga kanisa nyumban tukawa tunaabudu tu kwasabu Mungu ni wa upendo na ndiyo maana unakosa unaungama unaendelea!
 
Utajiri na mila wapi na wapi
 
Huyo siyo msukuma, kakudanganya tu ama wewe ndo umeelezea kwa kujaza chumvi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom