Mwongozo wa kununua Audi A4/A3, BMW 3 series/1 series na VW Golf/Polo

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Nimejaribu kupick European Cars ambazo watu wanazinunua sana.

Kwa bahati mbaya sina story nyingi za kununua Mercedez Benz, japo nilitamani ningeweka maelezo ya C class na E class sababu ndio gari za M/Benz watu wanazinunua sana.

Gari ambazo nimezilenga hapa ni gari ambazo zimezalishwa kati ya miaka ya mwanzoni wa 2000 mpaka 2010.

Kwa sababu hapo ndio yalifanyika mabadiliko makubwa kwenye engines za hizo gari na hapohapo ndio matatizo makubwa pia yalizaliwa.

Hivyo kitu kikubwa nitakachokizungumzia hapa kinahusu machaguo ya engine sababu hapo mauzamauza mengi yanazaliwa.

Tuendelee...

BMW 3 series/BMW 1 series

Hapa nitazungumzia E90 kwa 3 series na E87 kwa 5 series lakini pia ushauri huo unaweza kuutumia kwenye BMW X3 E83.

1. Kama unanunua BMW 3 series/1 series ambayo ina Cc2000 au chini ya hapo achana na Petrol. Tafuta Diesel ya M47 ukiikosa hiyo ndio uje kwenye N47.

2. Engine za petrol below 2000Cc kwenye hayo magari ambazo ni N43, N45 na N45 hazitakupa reliability ambayo kama ambayo utaipata kwenye hizo engine za diesel.

3. Kama unataka engine ya petrol ambayo haina makandokando na kwa bei ya uchumi wa kati nenda na N52B25 kwa Cc2500 au N52B30 kwa Cc3000. Hizi ni moja kati ya reliable engines za petrol kutoka BMW.

4. Achana na engine zinaitwa N53 au N54, Kama unataka kupata stroke basi nunua N54. Hiyo ni moja ya worst engines ambazo BMW amewahi kutengeneza. Kwa kifupi usinunue Direct Injection engine ya BMW yoyote iliyotengenezwa between 2000 to 2010.

5. Kama unataka engine ya petrol yenye nguvu na reliable na unajiweza kimfuko go for N55. Hii engine ilitengenezwa baada ya madudu yaliyotokea kwenye N53 na N54.

6. Kama unataka engine ya diesel yenye nguvu go for M57, Moja kati ya popular engine ya BMW na moja kati ya reliable engines BMW kuwahi kuzalisha. Ukiikosa hiyo go for N57.

Kama umewahi kuwa na ndoto za kumiliki Super Cars na hela haitoshi basi tafuta BMW yenye M57 halafu itune mpaka stage 3. Acceleration utakayoipata hapo ni ya level ya level za Super cars.

Gari za Audi na VW.

Kwa upande wa Audi na VW nako hakuna utofauti mkubwa sana kama ilivyokuwa kwa BMW.

The good thing about Audi ni kwamba matatizo yake yanaweza kurekebishwa japo utaingia gharama kubwa. Yaani walitoa engine ambayo ina parts mbovu lakini kwenye kuja kutengeneza spare parts wakafanya maboresho.

Nitaongelea sana Audi A4(matoleo ya B7(2004-2009) pamoja na matoleo ya mwanzo ya B8[2008-2011]). Audi A4 B6 sitaizungumzia kabisa japo kuna toleo moja la 2.0L FSI ni la kuwa nalo makini. Hayo maneno ya 2.0 FSI huwa yaanaandikwa nyuma ya gari kwenye Audi na VW.

A3(Toleo la 8p[2003-2011]

pamoja VW Golf MK5 na MK6

VW polo matoleo ya hiyo miaka hiyo ambayo ni mk4 na mk5 naomba nisiyaongeleee kabisa kwa sababu wao wana engine line ya tofauti na audi a3, a4 na VW golf. Kama mtu anafikiria kununua VW polo mk4 au mk5 kila la heri kwake.

Nitazungumzia sana series mbili za engine.

EA113 engines ambazo zilizalishwa sana between 2003 mpaka 2006

EA888 engines ambazo zilizalishwa sana between 2007 mpaka leo hii (Hapa nitabase kwenye first Gen, 2nd Gen na 3rd Gen).

Hayo matoleo mawili niliyotaja hapo juu yamebase kwenye 1.8L na 2.0L FSI, TSI na TFSI (Kwa kifupi hizo ni Direct injection[wao wameita Stratified Injection] kama ilivyo D4 kwenye toyota lakini pia hizo zinazoanza na T maana yake zinakuwa na Turbo).

Hii EA113 naomba niizungumzie kiujumla na matoleo mengine ya Audi na VW ambayo yanatumia Stratified injection lakini ni below 1.8L mfano 1.4FSI/TSI, 1.6FSI na 1.2TSI/TFSI.

Kiujumla kuna isssues kubwa mbili au tatu kwenye hizo engines. Na issues hizo hutokea between 60,000Km mpaka 100,000Km

1. Kufeli kwa kwa timing chain tensioner hivyo kupelekea chain stretch na baadae gari inahama timing, engine ndio inakufa kwa mtindo huo. Ingawa kama mtu unalifatilia gari lako vizuri chain ikisha stretch huwa inapiga kelele.

2. Consumption kubwa ya Oil gari ikishafikia Km ambazo nimezitaja pale juu huwa inakunywa sana oil. yaani kwa 1000Km lita nzima ya Oil inaweza kuisha. So kama mtu hafatilii atakuja tu kushtuka taa ya Oil hii hapa.

3. Carbon Build up kwenye valves. Hii huwa ipo across engines zote za direct injection. Lakini kwa sehemu kubwa huwa inachangiwa pia na quality ya mafuta na Oils zinayotumika.

4. Yapo matatizo mengine japo haya sasa ni kwenye kwenye engine mojamoja mfano, kufa kwa ignition coils, kuharibika kwa westgate za turbo thermostat housing kuchoka hivyo kupelekea leak ya coolant n.k.

Labda tu kiujumla niseme hivi, Ukipata gari ya VW au Audi yoyote kwa miaka hiyo ya 2000 mpaka 2011 ambayo haina hizi Tech za FSI, TFSI/TSI basi nunua kwa maana nyingi hazisumbui, ndio maana VW polo nimeitoa kwenye mjadala.

Kwa upande wa engine za Diesel za Audi ukipata 1.4 TDI,1.6 TDI, 1.9 TDI au 3.0TDI ni engines nzuri sana. Ziko more reliable ukilinganisha na 2.0 TDI, 2.5 TDI na 2.7 TDI. Kama hii 1.9 TDI toleo la mwaka 1998 mpaka 2006 ukipata yenye engine code ya ALH ni moja kati ya best engine VW amewahi tengeneza. In short inaweza ndio ikawa most reliable na durable engine kutoka VW group.

Okay tuje kwenye EA888, hapa tunazungumzia 1.8L na 2.0L TSI/TFSI na FSI engines ambazo zilianza kuzalishwa 2007.

Engine hizi zina matoleo matatu and kiukweli mtu unapaswa kuwa makini sana kwenye kuchagua.

EA888 toleo la kwanza. 2006/2007

Kwa 1.8L mifano ya Engine Codes BYT na BZB kwenye VW au CABA, CABB na CABD

Kwa 2.0L mifano ya Engine Codes CAWA, CAWB, CBFA, CCTA na CCTB.

Matatizo makubwa kwenye hili toleo ilikuwa na Kuharibika kwa kufeli kwa tensioner ya timing chain, kufeli waterpump, PCV, Carbon build up n.k.

Harakaharaka baada ya kuona hiyo engine ina hayo majanga wakaamua kuredesign hiyo first generation ili kuweza kuondoa hizo changamoto.

EA888 toleo la pili. 2008

Hii Second generation ni the worst engine VW group wamewahi kutengeneza.

Kwa 1.8L mifano ya engine codes ni CDAA, CDHA na CDHB.

Kwa 2.0L mifano ya engine codes ni CCZA, CCZB, CCZC na CCZD.

Kwenye toleo la pili kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kupunguza friction kwenye cylinders, hivyo wakaja na design mpya ya piston, rods pamoja na rings na hapo ndio ilipoturn out na kuwa worse.

Hizo piston mpya zilipelekea engine ikawa inaburn sana Oil. Kama nilivyosema mwanzo kwamba ndani ya 1000Km, one litre inaweza kutembea.

Hii engine iliwaharibia sana reputation yao sababu ukiachana tu na hiyo ishu ya kuburn Oil bado kulikuwa na msururu wa matatizo mengine kwenye hii gari. Pia haikuharibu tu reputation ya hiyo ea888 2nd gen. bali iliharibu reputation ya matoleo yote ya ea888 hasa 1.8L

EA888 Toleo la tatu 2009

Hapa VW group walifanya mabadiliko makubwa sana, na wakatoa kitu ambacho kinakupa best performance lakini pia kipo very reliable.

Kwa 1.8L mifano ya engine codes ni CJEB, CJEE, CJED, CJSA, CJSB, CPKA na CPRA.

Kwa 2.0L mifano ya engine codes ni CULA, CULB, CULC, CPLA na CPPA.

Hii engine inakuja na Dual injectors kwa kila cylinder. Injector moja kwenye port[MPI] na nyingine direct kwenye combustion chamber.

Walisort out issues zote zilizokuwa kwenye Gen One na Gen Two. Hata hiyo ishu ya Tensioner ambayo ni common kwenye engine nyingi za Audi. Kwenye hii gen 3 ni less prone tofauti na gen 1 na 2. Pia hii ishu ya kuburn oil kwenye hii engine wameimaliza.

Pia kitu kizuri zaidi ni kwamba kwa upande wa Audi matatizo yake mengi yanarebishika na spea zinakuwa duarable siyo kama zile zilizokuja na gari.

Kwa mfano kusolve tatizo la kuburn oil in a long term kwenye 2nd gen ya engine ya EA888 utahitaji kubadili Piston zote 4, mikono yake pamoja na rings zake uweke zile za engine ya Gen 1. Sababu Gen 1 na Gen 3 hazina hayo matatizo ya Oil Burning.

I think nimegusa sehemu kubwa kwenye Audi na VW. Pia kifupi tu niseme gari yoyote ya Audi au VW yenye FSI/TSI/TFSI na ni ya before 2010 ni gari ya kuwa nayo makini sana. Between 2009 na 2012 mwanzoni kuna gari zina matoleo mapya ya engine na zingine zina matoleo ya zamani napo panahitaji umakini sana.

Kama mtu ana swali karibu.
 
H
Nimejaribu kupick European Cars ambazo watu wanazinunua sana.

Kwa bahati mbaya sina story nyingi za kununua Mercedez Benz, japo nilitamani ningeweka maelezo ya C class na E class sababu ndio gari za M/Benz watu wanazinunua sana.

Gari ambazo nimezilenga hapa ni gari ambazo zimezalishwa kati ya miaka ya mwanzoni wa 2000 mpaka 2010.

Kwa sababu hapo ndio yalifanyika mabadiliko makubwa kwenye engines za hizo gari na hapohapo ndio matatizo makubwa pia yalizaliwa.

Hivyo kitu kikubwa nitakachokizungumzia hapa kinahusu machaguo ya engine sababu hapo mauzamauza mengi yanazaliwa.

Tuendelee...

BMW 3 series/BMW 1 series

Hapa nitazungumzia E90 kwa 3 series na E87 kwa 5 series lakini pia ushauri huo unaweza kuutumia kwenye BMW X3 E83.

1. Kama unanunua BMW 3 series/1 series ambayo ina Cc2000 au chini ya hapo achana na Petrol. Tafuta Diesel ya M47 ukiikosa hiyo ndio uje kwenye N47.

2. Engine za petrol below 2000Cc kwenye hayo magari ambazo ni N43, N45 na N45 hazitakupa reliability ambayo kama ambayo utaipata kwenye hizo engine za diesel.

3. Kama unataka engine ya petrol ambayo haina makandokando na kwa bei ya uchumi wa kati nenda na N52B25 kwa Cc2500 au N52B30 kwa Cc3000. Hizi ni moja kati ya reliable engines za petrol kutoka BMW.

4. Achana na engine zinaitwa N53 au N54, Kama unataka kupata stroke basi nunua N54. Hiyo ni moja ya worst engines ambazo BMW amewahi kutengeneza. Kwa kifupi usinunue Direct Injection engine ya BMW yoyote iliyotengenezwa between 2000 to 2010.

5. Kama unataka engine ya petrol yenye nguvu na reliable na unajiweza kimfuko go for N55. Hii engine ilitengenezwa baada ya madudu yaliyotokea kwenye N53 na N54.

6. Kama unataka engine ya diesel yenye nguvu go for M57, Moja kati ya popular engine ya BMW na moja kati ya reliable engines BMW kuwahi kuzalisha. Ukiikosa hiyo go for N57.

Kama umewahi kuwa na ndoto za kumiliki Super Cars na hela haitoshi basi tafuta BMW yenye M57 halafu itune mpaka stage 3. Acceleration utakayoipata hapo ni ya level ya level za Super cars.

Kwa leo tuishie hapo. Mwongozo wa Audi na VW nitauleta kesho jioni. Maana huko maelezo ni mengi sababu ya machaguo mengi ya engines.
Hahahahah nakusihi hakikisha kuna walau ka RunX ka kukutoa jangwani
 
Sawa Mkuu,Ninangojea part nyingine.
 
BMW first na second generation E21 na E30 zilikuwa na Injini ipi maana South Africa ndio gari zinazotumika kufanya drag racing na stunting na michezo kedekede. Wakina Lefale Ntinja,Magesh Ndaba na Stacey Lee haya matoleo ya Sasa hawataki Kutumia Kwenye michezo ingawa Kuna M Power na M Competition na wanamudu kuwa nazo.

Ukiacha VW Polo na Golf matoleo ya Sasa kuogopwa hizo BMW "Gusheshe" au "Sheshe" Zina Heshima sana kuzidi hata matoleo ya M.
 
Hizo stock zilikuwa na M20 kwenye six cylinders..! Hizo M20 hazina nguvu..

Hao drifters wanabadilisha engine.. Nyingi zimefungwa S50 kutoka E46 M3 au M50.. Ndio zina power nzuri..!
Sifa ya E30 ni ile chassis yake.. Imekuwa designed vizuri sana..!

Sasa E30 M3 hii gari ni gharama sana.. Na ni collector's car.. Mwaka jana kuna moja iliuzwa 250,000usd..!
Kwahiyo hizi zinatunzwa kweli kweli..
Engine yake ni 4 cylinders..S14 Ila ni moto..
Ukiipata Evo iii..!
Hizi zina heshima zaidi ya hizo Gusheshe..!
 
SAY NO TO TURBO

Hahahah kwanini Boss.

Katika engine zote nilizotaja hapo.

Engine yenye yenye turbo na ambayo ni pasua kichwa ni N54 tu.

Nadhani walishindwa kumanage heat ambayo inazalishwa kwa sababu ya mfumo wa Direct injection(sababu ya kurun lean) plus joto linalotokana na Turbo.

N53 haina turbo ila na yenyewe ina majanga kama yote sababu ni Direct injection.

N55 ina turbo na ni direct injection na ina single turbo japo ni twin scroll ila inaproduce power kubwa kuliko N54 ambayo ni Twin turbo.

Kwa engine za Diesel zenye turbo sijasikia kama kuna makandokando sana.
 
hii ina engine ipi mkuu je ni M50i?!!
BK635060_7f743f.jpg
Screenshot_20220212-224506.jpg
 
Hii inakuja engine ya N63 4.4L V8 twin turbo.

X7 zimeanza 2017 ikiwa tayari hiyo engine ya N63 imeshafanyiwa technical updates zaidi ya mara 4.

Kwa sasa ni reliable engine siyo kama ilivyokuwa kwa miaka 2006 mpaka 2010 kwenye original version ambapo I'm sure hata BMW wenyewe wanalijutia kitu walichokuwa wamewapelekea wateja wao.

Hizo engine wakati zinatoka miaka ya 2006/07 twin turbo ziliwekwa kwenye lile Bonde la V (bonde la kati kwenye V engines) halafu hawakuweka namna nzuri ya kudispate heat.

Gari ikawa inaua tu coil packs, ukifika muda wa kubadili spark plug inabidi ubadili na ignition coils.

Yakaja matatizo mengine kama kufeli kwa timing chain na kufa kwa injector nozzle. Simply mwanzoni wakati inaanza mauzauza yalikuwa mengi.
 
ok kwa hiyo hii ipo vzr
 
Huko nakuja.

Japo ukiweza kujipinda chukua kuanzia 2012 najua bei itakuwa imechangamka.
Nitaanza na Tiguan ya 2006 - 2009
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom