Mwongozo Chadema baada ya uchaguzi mdogo


Kama ulisoma paragraph ya kwanza katika mada yangu utagundua nimeongelea hicho unachokisema kwa kifupi sana kama ifuatavyo:
Uchaguzi mdogo wa madiwani ulikamilishwa na wapiga kura nchini Jumapili October 28, Chadema kimepata funzo kubwa lenye kutoa tafsiri kadhaa zenye kuleta matumaini kwa wenye moyo mkuu au kufifisha kwa wenye moyo mchache.
Wewe ni mmoja kati ya wenye moyo mkuu wa kutambua hayo, wengine wamekata tamaa na kusema wameshauri uongozi hawasikii sasa bai. Hayo sikubaliani nayo, siasa ni sayansi lazima kusoma upepo unavyokwenda na pia huhitaji muda kupata mang'amuzi katika nyanja hizi.

Mambo ambayo tunayaona kama yameweza kusababisha ndiyo tunayojadili hapa ili viongozi wahusika wayafanyie kazi. Kunyang'anya viti vilivyoshikwa na chama tawala si lelemama.
 
Daftari la wapiga kura ni moja kati ya sababu kuu! fikiri vizuri, Mangine umeongea sawa ila kunasehem umepotoka kiasi.

Viti ambavyo Chadema wameshinda hakukuwa na matatizo ya daftari la wapiga kura kama vituo ambavyo wameangukia pua? Nadhani sehemu walizoshinda Chadema walisimamisha wagombea wanaokubalika
 

Eneo hilo la kuandaa wagombea wenye sifa ambao watakubalika kwa wapiga kura ndilo linalotakiwa kupewa kipaumbele na kufanya kampeni kali ya vijijini nyumba kwa nyuma na mtaa kwa mtaa pia kukiwa na mabalozi wa nyumba kumi ili kuweza kuhakiki vema wanachama.
 
Sitaki kuamini kama maneno haya yameandikwa na Candid scope.

Ni aibu kubwa sana kuandika vitu bila kufanya utafiti wa kina.

*Nitarudi kufafanua zaidi

Nathibitisha kwamba ni mimi Candid nimeandika, niko wazi, sina kigugumizi katika kuonyesha ukweli kwa nia njema ya kujenga mageuzi ya kweli. Mficha maradhi mwisho humwumbua. Bora tuwe transparent.
 

Jamani njaa inaweza kusababisha matatizo mengi, walao kidogo kinasidia kuwajengea uvumilivu kwamba ipo siku mambo yatakamilika. Amini posho ni muhumu. Huenda wanapata, sijafanya utafiti wa kutosha kama wanapata au la. Hilo ni pendekezo langu kama hawapati basi kuwepo na utaratibu fulani utakaosadia nao kupata angalo kidogo cha kupangusa jasho wanalotaabikia.
 
Mleta mada acha kuishi kwa hisia bali kwa uhalisia.

*Ni ujinga mkubwa kubeza mafanikio madogo ya CHADEMA kupitia matokeo ya chaguzi hizi za udiwani bila kuangalia kwanza mwenendo mzima wa uendeshaji wa uchaguzi ulivyokuwa.

Hatujafikia kiwango cha kuanika matusi hapa, naoni ni mbalimbali, lete unayoona yanafaa kwani mimi nimeleta ya kwangu, na katika kujadiliana tutafikia mwafaka kwamba tuyapange vipi kwa kutangulizana kadiri ya umuhimu wa kwanza. Labda penye shaka kwa ustaarabu ulio nao ungeniuliza nitolee ufafanuzi na usiporidhika hapo unaweza kunieleza utelezi wangu.
 
Mkuu Candid Scope umeupackage ushauri wako kwa uongozi wa CDM kidiplomasia zaidi.
Fujo na kupimana ubavu na vyombo vya dola hakukiasidii chama chenu CDM.

Ushauri huu ungezingatiwa pengine Daudi Mwangosi angekuwa hai leo.
 
Ni aibu kubwa sana kuandika vitu bila kufanya utafiti wa kina.

*Nitarudi kufafanua zaidi......

Hata mimi imenistua sana......Its like this, let me expose them maana shetani hapendi mwanga anapenda giza zaidi..M4C imeleta damage kubwa sana kwenye magamba na hawana ubavu wakuendelea kutumia nguvu kubwa iliyodhahiri kuisitisha..Na inawezekana kabisa hata haya matokeo ya udiwani si ya kweli...Kwanini?

Walikuwa wanajua what they are after kwamba kisiasa kuonyesha jamii na CDM wenyewe hiyo M4C haijawa na impact kubwa kama wanavyodhani..Na kwakua hakuna data base ya huhakika Tz kutokana na mfumo mbaya wa governance..(Hata local government nyingi hazina socio-economic profile zao kujua who is who and where are they na ili kutengeneza hili si kazi ya siku moja na inahitaji resources) so wakajua inahitaji akili sana na intelligence syatem kwa CDM kung'amua hili then wamepanga usanii wao waki system na nje wanakuja kama washauri kumbe ndiyo wale wale...

Kwanini nasema haya kwasababu haiingii akili kwa true member wa CDM kuja na vitu public vya kuibomoa zaidi kuliko kuijenga..Tena hizo advice zi reflect kabisa matukio halisi....Ingekuwa inafanywa na watu in-experienced ningeelewa lakini wale wenye akili zao timamu na wenye uwezo wa ziada..CDM kumbukeni maneno ya Wasira......M4C ndiyo dawa pekee ya kuwafikishia elimu ya uraia watu wengi hasa wale ambao siyo elite maana wengi wako emotional na siyo rational..Then on top sasa mjitahidi kutafuta jinsi ya kuwa-retain kwa incentive based mechanisms ambayo wala si garama sana kama tutajipanga vizuri..Ni coordination tu inayohitajika wala si financial facility kubwa just a seed money.[/QUOTE]

Pole sana, mimi si member wa Chadema, ila tu ni mpenzi wa Chadema. Si mwanachama wa Chadema ila napenda movement zao na hata sera zao. Uwazi wazo na nguvu ya hoja waliyo nayo bungeni na uraiani. Samahani kama ulifikiri mimi ni mwanachama la hasha ila ni mpenzi chama.

Sipendi kuwa mwanachama wa chama cho chote cha siasa kwa sababu ya kutouruhusu utashi wangu kuwa na ushabiki wa rangi badala ya ukweli wa hali halisi. Ndio maana umeniona hata wabunge na wengine kutoka CCM wanaofanya vizuri naandika mada zao hapa na kuwapa sifa stahiki. Hapa JF walinipopoa mawe sana nilipoanza kuleta hoja za utendaji mzuri wa Filikunjombe na kupata tafsiri nyingi, lakini leo wengi wamekuja kutambua ukweli huo ingawa huyo mtu sijamtia hata machoni mwangu.

Siasa za vyama si uadui, kinachoshindaniwa ni njia ambayo kila chama inaona nibora zaidi katika kuongoza taifa kwa mafanikio. Chama chenye kuvutia wananchi wengi kwa sera zao ndicho kinachopewa jukumu. Sina chuki na CCM kwani wana sera nzuri sana ila viongozi ni ovyoooo! Utekelezaji wa sera ni ovyoooooo! Uozo na ubovu wa uongozi wa CCM vinatia kichefuchefu. Ndio maana wanafalsafa wanasema:
'Hachukiwi mtu ila matendo yake!'

JF tunatakiwa kuwa na upeo wa kuchambua mambo si kushabikia kama timu ya mpira. Kuchambua uwezo na udhaifu wa viongozi wa kisiasa ni haki yetu na ni njia ya kuwajenga. Hata nionane nao ana kwa ana nitafanya hivyo na watanielewa vema kuliko unavyonielewa wewe na baadhi ya wengine wanaopinga maoni yangu hapa.

Mambo ya zidumu fikra za mwenyekiti ndio hata akiteleza ni kupigia makofi tu na matokea ndio haya tunayolalamikia CCM kwa sababu pamoja na Kikwete kuvurunda huku Chama bado hakuna wa kumnyoshea kidole kama ANC walivyomwadabisha aliyemfuata Mandela.


Tunatakiwa tuwe great thinker, na katu siko tayari kufunika yale ambayo yanaweza kuhatarisha uhai wa chama tunachokitegemea kuwa mkombozi wetu wa kwali.
 
Reactions: Ame

Wengi walifikiri CDM imeshafika, hivyo walitarajia ushindi wa kishindo tu kuanzia sasa. Wameshindwa hata kuiona hatua iliyopigwa hapo. Hatuna budi kuuona ukweli kwamba watanzania wengi bado sana kuamka toka kwenye mitizamo finyu ya maisha ya leo leo na kushabikia vihongo vya hapa na pale badala ya kupigania mabadiliko ya kweli katika maisha yao. Tatizo la kasi ndogo hii si CDM; ni sisi wote tusiochukua hatua za dhati.
 

Sijasema mikutano na maandamano yasiwepo kabisa, kuna nafasi kadhaa hayawezi kuepukika. Lakini dhana ya kwamba chama kitajengwa kwa maandamano na mikuano tunatakiwa kuwa wapana wa kuelewe na kusoma mambo yanavyokwelda.

Kwenye mkutano wanaokuja ni mashabiki ambao tumeshuhudia muda mrefu kuanzia kipindi cha Mzee wa Kiraracha, nilikuwa Tabora alivyojaza uwanja mkubwa wa Michezo wa Ali Hasan Mwinyi huwezi kuamini na kilichotokea wakati wa uchaguzi palepale Tabora. Mikutano ni propaganda za kisiasa, lakini si njia mahsusi ya kujenga msingi wa wanachama wenye kukipigia kura. Ndio maana tunapendekeza njia ambazo CCM wamejizatiti ndizo Chadema waende huko kuvunja ngome yao kwa kuanzisha balozi wa nyumba kumi wenye kulinda matawi ya chama na wanachama. Huko utokeapo uchaguzi ni source ya hakika kujua kuna wanachama hai wangapi.

Mikutano tu ikiisha kila mmoja anarudi home nini kinaendelea mitaani?
 
Mimi nashindwa kushauri kitu kwa sababu naona kama vile uongozi haushauriki au hawapiti mitaa hii siku hizi kukusanya maoni ya wadau.

Kwa maoni yako inapendwa zaidi au inachokwa zaidi????
 

Nakubaliana na wewe kuhusu
  • CHADEMA kuachana na maandamano yasiyo ya lazima badala yake ifanyike mikutano ya hadhara kwa lengo la kueneza sera na kupata wanachama wapya. Viongozi wasitumie muda mwingi kulaumu CCM tu; pia wawaeleze wananchi ni kinapaswa kufanywa ili kuachana na udhaifu wa CCM
  • CHADEMA kuwa na radio na TV kwa ajili ya kueneza sera za chama
  • Watumishi wa chama kulipwa mshahara au posho ili kujenga morali ya utendaji. Si vibaya kumlipa Dr. Slaa milioni saba kama chama kina uwezo; Nafikiri kwa sasa CHADEMA isitumie fedha nyingi kuwalipa viongozi wa juu tu badala yake viongozi wa juu walipwe mshahara unaowawezesha kuendesha maisha yao e.g. 2,000,000/= zinatosha; fedha zingine zitumike kuwalipa posho viongozi wa chini. Tusidanganyane eti watumishi wa ngazi za chini watatenda siku zote kwa kujitolea.
  • Viongozi na makada wa chama waandaliwe kwa kupatiwa mafunzo ya uongozi. Chama kianzishe chuo cha uongozi. Wapo wanachama wengi wanaoweza kufanya kazi katika chuo hicho.
 

Hivi wewe, umeshafanya tafiti za kina za HUJUMA ZA CCM KWENYE CHAGUZI NA UKAZIJUA KISAWASAWA NA KIUNDANI NA IMPACT ZAKE KWA CDM? au umefanikiwa tuu kuchambua kasoro za CDM???
 
Twende kihesabbu kidogo
Ruzuku 233,000,000/=
Pos
ho ya makatibu wa mikoa iwe 400,000/=x30=12,000,000/=
makatbu wa wilaya iwe 250,000/=x140=35,000,000/=
makatibu wa majimbo iwe 200,000/=x239=47,800,000/=
makatibu wa kata iwe 50,000/=xkata2800=140,000,000/=
jumla bila wa matawi ni shilingi 234,800,000/=

Hivyo matawi bado hayajapigiwa hesabu na itambuliwe kuwa hata ukimpa katibu wa mkoa laki nne bado hawezi kujaza mafuta mwezi mzima pikipiki yake kweda kijiji cha wilayani km 200 na hatazaidi.

Wala laki mbili tu ya katibu wa jimbo huwezi kusemani kikubwa kiasi cha kumfanya azunguke jimbo zima mwezi mzima. Elfu hamsin sijui kama kweli ingekutia hamasa mwanajamvi kama katibu kat uache shughuli zako za kukupatia mkate wako ili uhamasishe chama kila sku katani kwako kama si moyo wa kujitolea tu.

Lakini kwa hesabu hiyo chama kitakuwa kinadaiwa 1,800,000/= kila mwezi! bila kujumuisha posho za watendaji makao makuu, kulipia mapango ya ofisi mbalimbali, kununua magari hayo muonayo ya M4C, pikipiki zilizoagizwa, operesheni mbalimbal, kesi, uchapaji kadi nk

Mkikaaga kwenye laptop huwa hamjui hali halisi kiasi kwamba hamjui kuwa watu wengine wakiwa partime hata hizo hekaheka zinazotisha CCM hamtaziona.

Kwa nini kama watu mna uchungu hamjitolei walau kumlipa posho ya katibu wa mkoa mmoja ili kujenga moyo wa wengine kujitolea,. Maneno tuuu
 
Kuvuja kwa pakacha,,,,, CDM ipunguze ukabila
 
Je umefanya utafiti ukagundua kuwa vyama vya upinzani visivyofanya maandamano kama CUF UDP NCCR au TLP vimefanya vizuri kuliko CHADEMA ya maandamano? Pumba Kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…