Mwl. niko Ughaibuni kuongeza Elimu, niliyoyaona..

Mwl. niko Ughaibuni kuongeza Elimu, niliyoyaona..

Hutaosha vibabu miguu tu....utatemewa mikohozi na vizee vikorofi, vitakupiga kucha za hatari, utanyonya dushelele zao, uharo, matapishi n.k...hapo kibabu kinarun 97 yrs kimevuta mifegi mpaka koo likafunga[emoji23] [emoji23]

Mi nilipewa huo mchapo nikastagnant!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mm mtoto wa baba jesca nawapiga makofi na kichambo cha kiswahili
 
Ooops!..Mbona matibabu naambiwa ni very quality and cheapest?
Bima ndo kila kitu..lakini kweli huduma ni nzuri mradhi uwe covered.. sema wenzetu huwa ni wagumu sana kuandika dawa, yaani utaambiwa mazoezi na vyakula vya kula...
 
Tofauti ya kwa nini ulaya wanaendelea na sisi tunabaki nyuma ni hicho unachokifanya mkuu.

Hapa nyumbani, wewe mwalimu na elimu yako yote hiyo, unaweza kuokota makopo mitaani kweli?

Kwanza utaonekana umechizika, lakini pia sisi wamatumbi tukienda shule tu basi kuna kazi nyingine hatuzitaki au tuonekane tunazifanya.

Sijui siku hizi lakini nilipokuwa chuoni hata siku moja sikufikiria kuomba kazi ya kuuza chakula hotelini. Au msichana kwenda kuuza baa. Wakati huko majuu hizo ndizo kazi za wanachuo.

Halafu hao wanachuo wanaofanya kazi kama yako mkuu wanasevu na wakati wa kiangazi wanakuja tembea kama watalii TZ.

Angalia sasa tunavyowapapatikia na kuwasujudia kama miungu. Watu ni kuwasifia tu: "Hao wazungu bwana, wamejaa kishenzi hao." Shubaaaaamit.

Halafu tukitawaliwa au kuitwa SHITHOLE countries, tunalalamika.
Umenigusa na ukweli wako, nadhani wengine watasoma na kuelewa ulichoandika..Asante kwa elimu yako ya kimaisha..
 
Tofauti ya kwa nini ulaya wanaendelea na sisi tunabaki nyuma ni hicho unachokifanya mkuu. Hapa nyumbani, wewe mwalimu na elimu yako yote hiyo, unaweza kuokota makopo mitaani kweli?
Kwanza utaonekana umechizika, lakini pia sisi wamatumbi tukienda shule tu basi kuna kazi nyingine hatuzitaki au tuonekane tunazifanya. Sijui siku hizi lakini nilipokuwa chuoni hata siku moja sikufikiria kuomba kazi ya kuuza chakula hotelini. Au msichana kwenda kuuza baa. Wakati huko majuu hizo ndizo kazi za wanachuo. Halafu hao wanachuo wanaofanya kazi kama yako mkuu wanasevu na wakati wa kiangazi wanakuja tembea kama watalii TZ. Angalia sasa tunavyowapapatikia na kuwasujudia kama miungu. Watu ni kuwasifia tu: "Hao wazungu bwana, wamejaa kishenzi hao." Shubaaaaamit.
Halafu tukitawaliwa au kuitwa SHITHOLE countries, tunalalamika.
Hapo tu mkuu, hapo tu, ndio maana tuko maskini!
Mkuu wale huku wanafuata Madini yetu tu...
Siyo madini tu mkuu, tuna rasilimali na maliasili za kufa mtu hapa, akili zetu naona zimedumaa kutokujuwa tutazitumia kivipi tupate maendeleo na utajiri..
Umesikia ya mtaji wa laki na nusu, sasa wengine wanakuja bila hata hiyo, ila siku wakiondoka kurudi kwao ni matajiri wa kufa mtu...
Waafrika tuna matatizo nafikiri...
 
Bima ndo kila kitu..lakini kweli huduma ni nzuri mradhi uwe covered.. sema wenzetu huwa ni wagumu sana kuandika dawa, yaani utaambiwa mazoezi na vyakula vya kula...
kuna rafiki zangu kibao washaenda hospitali anaambiwa kanywe maji ya kutosha na mazoezi. Pharmacy nano huwezi nunua dawa bila prescription toka kwa daktari, utaishia kununua panadol
 
kwenye nyanja zote, kule bwana watu wanapenda space, unaweza kuwa na jirani asitake hata kujua jina lako, japo milango yenu inafuatana. Yeye akiwa na mbwa wake tosha.. huku kwetu unaweza kutoka ukaingia lets say bar, mkakutana na washkaji tu mkapiga story kibao mkacheka na kuenjoy hadi mnaondoka hata majina hamjaulizana na maisha yanaenda..kule wanasema you are just a stranger, i dont talk to a stranger.. mvua ikinyesha kama huna mwavuli huwezi kuingia kwenye kibaraza cha mtu kujificha..itapigwa simu polisi fasta unasikia you are invading a private property.. yaani ni full ubinafsi kule.. kwenda kwa mtu lazma utoe taarifa si unasema mshkaji nilikuwa napita hapa nikaona nikupe hi..hakuna hilo.. ndo maana nikasema unaweza kuwa mpweke sana si sawa na huku
hahaha dah, mkuu nimecheka sana , kuna sehemu nipo watu wamenishangaa....
 
Kwa mazingira ya kazi mkuu sidhani kama waweza dumu pale zaidi ya miezi 3 au 6, ila nakomaa sababu ya malengo...
Ila wenzetu wanapiga kazi mkuu! Acha kabisa, hakuna cha mweupe au mweusi, mwarabu au mhindi, wote job job tu..
pambana ukija bongo uwekeze
 
kwenye nyanja zote, kule bwana watu wanapenda space, unaweza kuwa na jirani asitake hata kujua jina lako, japo milango yenu inafuatana. Yeye akiwa na mbwa wake tosha.. huku kwetu unaweza kutoka ukaingia lets say bar, mkakutana na washkaji tu mkapiga story kibao mkacheka na kuenjoy hadi mnaondoka hata majina hamjaulizana na maisha yanaenda..kule wanasema you are just a stranger, i dont talk to a stranger.. mvua ikinyesha kama huna mwavuli huwezi kuingia kwenye kibaraza cha mtu kujificha..itapigwa simu polisi fasta unasikia you are invading a private property.. yaani ni full ubinafsi kule.. kwenda kwa mtu lazma utoe taarifa si unasema mshkaji nilikuwa napita hapa nikaona nikupe hi..hakuna hilo.. ndo maana nikasema unaweza kuwa mpweke sana si sawa na huku
Hayo ndiyo maisha ya KIBEPARI PURE !
- Mtu anajenga JUMBA, anajiwekea BONGE LA GETI LA UMEME. Hakuna kujikinga MVUA kwa MTU wala KUOMBA MAJI YA KUNYWA !
 
Mbona mnapenda sana kujitangaza....mimi nimeishi Ethiopia miaka miwili tena mjini Tigris lakini sikutangaza. Nawashangaa sana.
 
kuna rafiki zangu kibao washaenda hospitali anaambiwa kanywe maji ya kutosha na mazoezi. Pharmacy nano huwezi nunua dawa bila prescription toka kwa daktari, utaishia kununua panadol
Kwanini wanagoma kutoa dawa sasa?
 
Mbona mnapenda sana kujitangaza....mimi nimeishi Ethiopia miaka miwili tena mjini Tigris lakini sikutangaza. Nawashangaa sana.
Hahahaha...🙂🙂🙂🙂
Haina tatizo mkuu, hata kama umeenda Ukerewe, wewe weka nondo tujifunze, ila tunamshukuru kwa kutufumua macho...Duniani kuna watu wanaishi bana acha tu, safi sana kwa kweli..
 
Baya lisilokudhuru ni sawa na zuri lisilo na faida piga kazi mkuu ikiwezekana achana na mambomengine komaa kazini.
 
Hahahahaha....Nguo siyo issue mkuu, swala ni cheti changu na kandinga (usimwambie mtu, taratibu)..Gari kwanza nyumba baadaye..
Umenichekesha mkuu me natamani niipate hiyo kazi yako niifanye angalau mwaka 1 alafu nirudi home namtaji hata wamilioni 30 inatosha
 
Back
Top Bottom