Mwl. Kambarage Nyerere alitayarishwa!

Mwl. Kambarage Nyerere alitayarishwa!

Hiki ndiyo kilele cha kutokufikiri. Hiyo shule ya Tabora alisoma peke yake? Ulitaka Waingereza wasijjenge shule kwa ajili ya kuwaelimisha Waafrika? Hata leo serikali zote duniani zinaendelea kujenga shule na vyuo ili kusomesha vijana watakaoongoza nchi zao siku za usoni.

Tabora haifanani kwa vyovyote vile na Eton College.

Nyerere alipotoka Tabora Boys alikwenda Makerere ambayo ilikuwa ni College ya University of London na siyo Scotland(Edinburgh).

Inaelekea haujanielewa vizuri, Waingereza walijenga shule nyingi tu, ila hii ya Tabora ilikuwa ni Shule maalumu na ilijengwa kwa kufwata Model ya Eton College ya huko kwao, hilo wala usijaribu kulipinga, unaposema haifanani unamanisha nini?
Unaelewa maana ya "model"? Maana yake ni kwamba lengo la kuanzishwa kwa hiyo Shule (Tabora) ni kama lile lile la Eton College ambalo lilikuwa au kupika au kulea Viongozi wa wajao wa Taifa hilo ndilo lengo haswa.
Na hilo liko kila mahali na kama unabisha nenda Nyaraka za Taifa (National archives) pale Upanga na kasome historia yetu kila kitu kimeorodheshwa na kinatunzwa!

Sasa unataka kubisha Mlm.Nyerere hakusoma Scotland au? Au unataka kubisha kwamba alikutana na mambo ya ujamaa Scotland au? Au unataka kubisha kwamba Waingereza ndio walimpeleka kusoma Scotland? au unafikiri ni wazee wa Mkoa DSM ndio walimchangia kumpeleka Scotland?
 
Stori za kijiweni hizi! Utazijua tu facts zake ubabaishaji mtupu. Tumia muda kusoma na sio stori za gahawan
 
Taaaabora schooool kichwaaaa cha Tanzaniaaaaa..hapa alisomeshwaa baba yetu wa taifaaaa..taabora schoolx2 kichwaa cha Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas....hahahahhaha mguu pande! Mguu sawa! Hima himaaaaaa hima himaaaaa!
 
Aise mkuu kwa uwongo hujambo!nyerere hakusomea degree scotland wala ujamaa hakusomea.ujamaa aluichukua uchna kwa mao.
google Julius Kambarage Nyerere na soma na soma part ya early life and education - wacha uvivu:smile-big:
 
Hata kuzaliwa ukoo wa kichifu (Chifu Burito) aliandaliwa.

Hata kufa na kuzikwa Butiama iliandaliwa na Waingereza!

Katika muendelezo wangu wa kutafuta kiini cha matatizo yetu hapa Nyumbani, nimekuja kugundua kwamba Raisi wa kwanza wa Tanzania au sijui Tanganyika Mlm Kambarage Nyerere alitayarishwa na Wazungu (Waingereza) tangu enzi akiwa kijana ili aje kupewa na kukabidhiwa Nchi!

Sasa ni kwa nini nimefikia hapo, ni kwamba nimefwatilia nyendo za Mlm Nyerere nikaona kwamba alisoma Tabora Boys, Shule ambayo ilijengwa na Waingereza kwa lengo la kukuza kizazi cha Waafrika watakaoachiwa nchi pindi muda wao wa kuondoka utakapofika, yaani Watawala wetu, Tabora Boys ilianzishwa kwa kufwata Mfano wa Eton college ya huko Uingereza ambayo mpaka leo Viongozi wa nchi hiyo wengi wao wanatokea hapo!

Baada ya kutoka hapo Bw.Nyerere alipelekwa moja kwa moja Scotland kusoma kwa udhamini wa Waingereza na alipokuwa huko ndipo alipokumbana ya mambo ya Ujamaa, ambayo baadae alikuja kuyapandikiza kwenye Nchi yetu!

Baada ya kutoka huko na baada ya Waingereza kuona sasa alishaiva ndipo wakamrudisha na kumkabidhi Nchi, kinyume na propaganda tunazolishwa kwamba Bw.Nyerere alileta Uhuru, ukweli ni kwamba alitayarishwa ali aje apewe kwa malengo ya kulinda na kutetea maslahi ya Wazungu (Waingereza) kazi ambayo aliifanya vizuri sana na mpaka leo watawaala wetu wanaiendeleza...
 
Kuzaliwa Kichifu au kuzikwa Butiama sio ishu wengi tu wamezaliwa machifu na pia walikufa na kuzikwa Butiama. Hivyo sielewi unachomaanisha!

Sio swala la kujivua au kuvaa Nguo bali ni Swala la Ukweli! Je Mlm.Nyerere alifia wapi? Muhimbili Makao makuu ya Ujamaa ama London makao makuu ya Ubepari?

muda na nguvu unazotumia kumjadili marehemu ni vema ukatumia kufanya maendeleo..asante
 
Inaelekea haujanielewa vizuri, Waingereza walijenga shule nyingi tu, ila hii ya Tabora ilikuwa ni Shule maalumu na ilijengwa kwa kufwata Model ya Eton College ya huko kwao, hilo wala usijaribu kulipinga, unaposema haifanani unamanisha nini?
Unaelewa maana ya "model"? Maana yake ni kwamba lengo la kuanzishwa kwa hiyo Shule (Tabora) ni kama lile lile la Eton College ambalo lilikuwa au kupika au kulea Viongozi wa wajao wa Taifa hilo ndilo lengo haswa.
Na hilo liko kila mahali na kama unabisha nenda Nyaraka za Taifa (National archives) pale Upanga na kasome historia yetu kila kitu kimeorodheshwa na kinatunzwa!

Sasa unataka kubisha Mlm.Nyerere hakusoma Scotland au? Au unataka kubisha kwamba alikutana na mambo ya ujamaa Scotland au? Au unataka kubisha kwamba Waingereza ndio walimpeleka kusoma Scotland? au unafikiri ni wazee wa Mkoa DSM ndio walimchangia kumpeleka Scotland?

Tabora ilijengwa kama shule ya kuelimisha watoto wa machifu.Wale wanafunzi wa Tabora Boys walikuwa wanapewa huduma nzuri sana ikiwa ni pamoja na kufagiliwa vyumba vyao, kutandikikiwa vitanda, nk. Hata hivyo walikuwa wanacharazwa viboko. Sidhani kuwa wanafunzi wa Eton walikuwa wanapigwa viboko.

Nyerere baada ya kumaliza Tabora Boys alikwenda Makerere kusoma Diploma ya Ualimu ambako alifanya vizuri sana na kuchagua kufundisha St. Marys Girls nayo ya Tabora. Colonial Office walimpa Scholarship ya kwenda kusomea degree ya Biology, somo alilosomea kule Makerere lakini alikataa akachagua kusomea Uchumi, Jiographia na Filosofia.

Ninachokataa mimi ni kuwa Nyerere alitayarishwa na Wakoloni kuja kutawala Tanganyika. Nyerere alikuwa ni kati ya watu wengi ambao walisoma Mwisenge, hatalfu Tabora Boys, halafu Makerere, halafu Edinburgh. Tofauti ni kuwa yeye alitamani kuwa kiongozi wa juu Tanganyika. Ni yeye mwenyewe na siyo wakoloni.

Prof. Mukandara , Prof. Shivji na wengine wengi walisoma shule mbalimbali kabla ya kuwa maprofesa pale mlimani. Walipomaliza UDSM waliombwa kubakia pale wafundishe taaluma fulani. Wangeweza kukataa. walikubali kwa vile walipenda. Hawakulazimishwa. Hatuwezi kusema leo hii kuwa Shivji alitayarishwa na serikali kuwa professa wa Chuo Kikuu cha DSM.
 
Katika muendelezo wangu wa kutafuta kiini cha matatizo yetu hapa Nyumbani, nimekuja kugundua kwamba Raisi wa kwanza wa Tanzania au sijui Tanganyika Mlm Kambarage Nyerere alitayarishwa na Wazungu (Waingereza) tangu enzi akiwa kijana ili aje kupewa na kukabidhiwa Nchi!

Sasa ni kwa nini nimefikia hapo, ni kwamba nimefwatilia nyendo za Mlm Nyerere nikaona kwamba alisoma Tabora Boys, Shule ambayo ilijengwa na Waingereza kwa lengo la kukuza kizazi cha Waafrika watakaoachiwa nchi pindi muda wao wa kuondoka utakapofika, yaani Watawala wetu, Tabora Boys ilianzishwa kwa kufwata Mfano wa Eton college ya huko Uingereza ambayo mpaka leo Viongozi wa nchi hiyo wengi wao wanatokea hapo!

Baada ya kutoka hapo Bw.Nyerere alipelekwa moja kwa moja Scotland kusoma kwa udhamini wa Waingereza na alipokuwa huko ndipo alipokumbana ya mambo ya Ujamaa, ambayo baadae alikuja kuyapandikiza kwenye Nchi yetu!

Baada ya kutoka huko na baada ya Waingereza kuona sasa alishaiva ndipo wakamrudisha na kumkabidhi Nchi, kinyume na propaganda tunazolishwa kwamba Bw.Nyerere alileta Uhuru, ukweli ni kwamba alitayarishwa ali aje apewe kwa malengo ya kulinda na kutetea maslahi ya Wazungu (Waingereza) kazi ambayo aliifanya vizuri sana na mpaka leo watawaala wetu wanaiendeleza...
Jina lenyewe Kijakazi!!!!!!!!! Hv lina maana gani kwa kiswahili fasaha jamani? Mm nafikiri watu wa jina lako wanafikiri kitumwa tumwa vile! Unisamehe bure maana hata uandishi wako ni magumashi kweli. Haya endelea na utafiti wako tena.
 
Bado unachemka tuu! Tabora school ilijengwa na Waingereza kwa ajili ya kuelimisha Watawala au Viongozi wajao, na wala SIO Machifu tu, ilikuwa ni kwa yoyote yule ambaye alitimiza masharti ambayo wao (Waingereza) waliyaweka ya kupata nafasi ya kusoma pale, hivyo kama Ulikuwa mtoto wa Chifu na ukatimiza masharti walikuchukua Na Mlm.Nyerere ilitokea tu akawa Mtoto wa Chifu!

Wakoloni waliona kitu kwake na ndio maana walimpenda (labda) na kuamua kumuendeleza zaidi, kwa mategemeo kwamba wangemuhitaji baadae, na SI zaidi ya Hapo!
Kumbuka kwamba Waingereza tangu mwaka 1920 walikuwa wanajua kwamba mwisho wa siku ni lazima Waichie Nchi yetu, swala tu lilikuwa ni lini, waiache vipi na wamuacchie nani?

Hivyo kazi ya kutafuta mrithi ilianza muda tu na yeye Mlm.Nyerere, kutokana na juhudi zake yeye mwenyewe wakamuona, wakampenda, wakaanza kazi ya kumkuza na kumuandaa ili aje aendeleze ukoloni ila kwa namna nyingine, kitu ambacho leo hii tunakiona na hata tumekibatiza jina ukoloni mweusi!

Gomberg_map.jpg
Post war new world order... Zanzibar ilikuwa iwe base ya kijeshi....
 
Jina lenyewe Kijakazi!!!!!!!!! Hv lina maana gani kwa kiswahili fasaha jamani? Mm nafikiri watu wa jina lako wanafikiri kitumwa tumwa vile! Unisamehe bure maana hata uandishi wako ni magumashi kweli. Haya endelea na utafiti wako tena.

Asante kwa ushauri! Bado naendelea kujifunza na kusoma ili nielewe tunakotoka, tuliko na tunakokwenda!

Kwa kifupi natafuta kiini cha matatizo yetu, ni kwa nini tuna hya matatizo yasiyoisha? Ni kwa nini Maisha ya Tembo ni muhimu kuliko ndugu zetu? Ni kwa nini Mzungu anauziwa Shamba na Ndugu zetu wanafukuzwa kama wanyama tena kwa Polisi?
Ni kwa nini Raisi wa Nchi anagawa Rasilimali zetu kwa Wazungu? Ni nini kinamsukuma kufanya yote haya?

Ni kwanini Waziri wa Nishati anasema Watz tunaweza tu Bishara ya kuuza juice lakini sio Madini? Kwamba madini ni ya Wazungu tu, ni nini hasa kinamshusha Mtu chini kiasi Hicho?
Chimbuko ni nini?
 
Katika muendelezo wangu wa kutafuta kiini cha matatizo yetu hapa Nyumbani, nimekuja kugundua kwamba Raisi wa kwanza wa Tanzania au sijui Tanganyika Mlm Kambarage Nyerere alitayarishwa na Wazungu (Waingereza) tangu enzi akiwa kijana ili aje kupewa na kukabidhiwa Nchi!

Sasa ni kwa nini nimefikia hapo, ni kwamba nimefwatilia nyendo za Mlm Nyerere nikaona kwamba alisoma Tabora Boys, Shule ambayo ilijengwa na Waingereza kwa lengo la kukuza kizazi cha Waafrika watakaoachiwa nchi pindi muda wao wa kuondoka utakapofika, yaani Watawala wetu, Tabora Boys ilianzishwa kwa kufwata Mfano wa Eton college ya huko Uingereza ambayo mpaka leo Viongozi wa nchi hiyo wengi wao wanatokea hapo!

Baada ya kutoka hapo Bw.Nyerere alipelekwa moja kwa moja Scotland kusoma kwa udhamini wa Waingereza na alipokuwa huko ndipo alipokumbana ya mambo ya Ujamaa, ambayo baadae alikuja kuyapandikiza kwenye Nchi yetu!

Baada ya kutoka huko na baada ya Waingereza kuona sasa alishaiva ndipo wakamrudisha na kumkabidhi Nchi, kinyume na propaganda tunazolishwa kwamba Bw.Nyerere alileta Uhuru, ukweli ni kwamba alitayarishwa ali aje apewe kwa malengo ya kulinda na kutetea maslahi ya Wazungu (Waingereza) kazi ambayo aliifanya vizuri sana na mpaka leo watawaala wetu wanaiendeleza...

Hapo kwenye RED, Nyerere alipelekwa Scotland kwa udhamini wa mapadri wa Kanisa Katoliki.
 
Wa kutoka wapi? Kumbuka Wazungu wameanza mambo ya kutenganisha Serikali na Dini majuzi tu, lkn kabla ya hapo kulikuwa na Ushirikiano mkubwa sana kati ya Kanisa na Serikali, na ndio maana kuna Msemo kwamba Wamishionari walikuja Afrika na Biblia na sisi walitukuta Ardhi, baadae wakatupa Biblia na sisi tukawapa Ardhi!

Kwa kifupi nafikiri Historia ya vidato vya mwanzoni kabisa tunafundishwa kwamba Wageni wakwanza kuja walikuwa Wapelelezi na Wamishionari ambao walikuwa wanaripoti moja kwa moja kwenye Serikali zao, kwa maana nyingine waliweka au walitayarisha mazingira ya Ukoloni, hivyo hakuna tofauti kati ya yeye kupelekwa Scotland na Kanisa au Malkia, lengo lilibaki kuwa ni lile tu!

Mkuu umewakilisha mawazo yangu mwanzo mwisho. Kifupi hata wazalendo waliopoteza muda na uhai wao kupigania uhuru wa nchi alikuwa anawadharau tu kwani alikuwa anajua mwisho game itakuwaje. Hata alipokaribishwa na wazee wa kiislamu katika harakati za ukombozi ndani ya chama cha TAA tayari alikuwa ana ajenda zake za kuendeleza ukoloni mambo leo huku wenzake wakikusudia kumuondosha mkoloni na kung'oa mizizi yake, yeye alihakikisha mizizi yao inaendelea kunawiri.
 
Kumbe ulikua hujui ile Vita ya Uganda ilikuwa ni proxy war au vita ambayo Nchi fulani au kikundi fulani kinapigana kwa maslahi Binafsi ya Nchi au kikundi kikingine, bila ya hiyo nchi inayopiganiwa kujihusisha moja kwa moja, kama vile Kenya walivyo Somalia, au Majeshi yetu yalivyo Kongo hizo zote ni proxy wars kwa maslahi ya Marekani na Marafiki zake!

hii inamaana waliosoma tabora boys wote walipewa nchi...ila kumbuka sio wote wanaotaka kutumika huwa wanakubali utumwa hasa wakishagundua kuwa wanatumika na wanajua what is a right way to. Inawezekana ila kama ndo hivyo yeye alikiuka upapeti huo
 
Back
Top Bottom