Katika muendelezo wangu wa kutafuta kiini cha matatizo yetu hapa Nyumbani, nimekuja kugundua kwamba Raisi wa kwanza wa Tanzania au sijui Tanganyika Mlm Kambarage Nyerere alitayarishwa na Wazungu (Waingereza) tangu enzi akiwa kijana ili aje kupewa na kukabidhiwa Nchi!
Sasa ni kwa nini nimefikia hapo, ni kwamba nimefwatilia nyendo za Mlm Nyerere nikaona kwamba alisoma Tabora Boys, Shule ambayo ilijengwa na Waingereza kwa lengo la kukuza kizazi cha Waafrika watakaoachiwa nchi pindi muda wao wa kuondoka utakapofika, yaani Watawala wetu, Tabora Boys ilianzishwa kwa kufwata Mfano wa Eton college ya huko Uingereza ambayo mpaka leo Viongozi wa nchi hiyo wengi wao wanatokea hapo!
Baada ya kutoka hapo Bw.Nyerere alipelekwa moja kwa moja Scotland kusoma kwa udhamini wa Waingereza na alipokuwa huko ndipo alipokumbana ya mambo ya Ujamaa, ambayo baadae alikuja kuyapandikiza kwenye Nchi yetu!
Baada ya kutoka huko na baada ya Waingereza kuona sasa alishaiva ndipo wakamrudisha na kumkabidhi Nchi, kinyume na propaganda tunazolishwa kwamba Bw.Nyerere alileta Uhuru, ukweli ni kwamba alitayarishwa ali aje apewe kwa malengo ya kulinda na kutetea maslahi ya Wazungu (Waingereza) kazi ambayo aliifanya vizuri sana na mpaka leo watawaala wetu wanaiendeleza...
Matokeo ya NECTA form 4 2013 yameshatoka umepata div ngapi? Unachandika hata huwezi kukitetea! hivi kwa akili yako Waingereza wangemwachia nchi kiulaaini mtu ambaye hakuwa dini yao ya Anglikana? Hujui kuwa Pesa ya nauli au tiketi ya kwenda New York Nyerere alichangiwa na watu haswa kanisa.............,
Kwahiyo unataka kutuambia kuwa kuna mgombea urais ambaye ameshaandaliwa na alisoma hizo shule na chuo ulichokitaja?
Wewe ndio hujui unachokiandika aliyekwambia kwa Wazungu Dini inamata ni nani? Kwa Wazungu au Mabepari cha muhimu FAIDA tu, Mbona Iraq, Palestina, Sudani, Misri waliwakabidhi Waislamu? Mbona India waliwakabidhi Wahindu? Itakuwa Mlm Nyerere Mkatoliki?
Halafu unaongelea mambo ya kwenda New York, kwenda New York kulifwata baadaye sana baaada ya TANU ilikuwa imeshaanzishwa na hao hao Waingereza (TANU Ilianzishwa na Wazungu!) baada ya Mlm Nyerere kurudi kutoka Scotland alikopelekwa kusoma na Wazungu!
Mimi nimekwambia kuhusu Historia ya Mlm Nyerere, mambo ya Tabora Boys yameshakwisha kwa maana lengo lake lilishatimia kwa Wazungu, na kilichobaki sasa ni muendelezo tu wa yale Mlm Nyerere aliyoyaanzisha ya kulinda na kuteteta maslahi ya Wazungu, na ndio maana mpaka Sheria yote na lugha ya kimahakama ni Kiingereza, Kwa nini?
kwa nini Mlm Nyerere hakubadilisha hilo kwa miaka 24 aliyokuwa Raisi?
na mpaka leo akina Bw.Kikwete wanaendelea tu kuuza nchi kwa Wazungu, juzi Waingereza wameongea kidogo kuhusu meno ya Tembo nchi nzima kuanzia Raisi mpaka makatibu wa Wizara wakafunga Safari kwenda kujieleza huko, Uingereza kwa nini?
Kama ile habari ingeandikwa na Gazeti la Ujapani wangefunga Safari kwenda kujieleza?
Au wangetumia nguvu kuhamisha ndugu zetu na kuwaua kisa kulinda Tembo?
Hujui unachokiongea nchi za kiislam zilikuwa ngumu kutawalika, hivyo wazungu walifanya mfumo wa indirect rule.
Mkuu,
Kwa kadiri ya maelezo yako inawezekana ukamalizia riwaya yako kwa kusema baada ya kumaliza kazi yao, waingereza wakamuua Nyerere pale St. Thomas eh?
acha kujivua nguo ndugu..hakuna anayejua siku yake ya kufa so ni ngumu sana mtu kuchagua sehemu ya kwenda kufia..jaribu kuficha udhaifu wakoHilo nalo la kwenda kufia Uingereza linazidi tu kusiliba ukweli kwamba Mlm Nyerere alitayarishwa na Waingereza na ndio maana hata kufia alichagua kwenda kufia huko!
Wewe jiulize, miaka yote ametutawala amekuwa akituimbisha kwamba Ubepari ni unyama sasa iweje achague kwenda kufia tena kwa Wanyama kwenye Makao Makuu ya Ubepari?
Acha uongo wewe kwanza hoja zako ni hafifu kiasi kwamba hata mtoto wa darasa la 4 atajua tu kuwa wewe ni mwongo.swali..
1.Ulitaka nyerere asome wapi kwa kipindi hicho? kwani kulikuwa na shule zingine ambazo zilikuwa hazina mahusiano na wazungu?
2. Unaposema Nyerere hakuleta UHURU ni uongo kwa nini nchi zingine za kiafrika hazikupewa uhuru wakati nako kulikuwako na shule za waingereza mfano ni kenya......Na harakati alizokuwa akizifanya Nyerere,kambona,sykes na akina bibi titi zilikuwa za nini kama tulizawadiwa uhuru?
Acha kupotosha umma kwa makala zako zisizo na tafiti harafu unasema ndio ukweli kwa vigezo vipi?
Usitafute ufanano wa Nyerere na hao wengine kwa kutafuta vihoja vya ovyo......Binafsi sijawai shuhudia utawala wa nyere kwani amefariki nikiwa darasa la kwanza lakini mpaka sasa jina lake liko kinywani mwangu kuliko Marais nilioshuhudia uongozi wao
acha kujivua nguo ndugu..hakuna anayejua siku yake ya kufa so ni ngumu sana mtu kuchagua sehemu ya kwenda kufia..jaribu kuficha udhaifu wako
Duh, Kumbe Sio Makerere Ug Ni Scotland, Kwa Hiyo Nyerere Katoa Ujamaa Scotland? Scotland Walikuwa Wajamaa? Hata Hivyo Hadithi Yako Inavutia!
Embu toa ----- wako hapa,kwani wakati Nyerere anatayarishwa Babu yako au Baba yako alikuwa wapi na yeye asitayarishwe?wakati Mwl. Nyerere yupo Darasani anakuna Bongo,Babu/Baba yako yupo Kisiju akiandaa mdundiko kwa ya ndoa ya Mwajala ya Shangazi yako.
Uko sawa Kabisa na ndio maana aliweza kupata Scholarship ya Waingereza, kwa maana walikuwa wanatafuta Mtu mwenye uwezo ili waweze kumwandaa kumwachia Nchi na mwishowe kulinda maslahi yao, kitu ambacho alikifanya na mpaka waliomfwatia wote wanaendelea kukifanya akina Bw.Kikwete & Co.!
Babu yangu hakupata kwa kuwa kwa namna ama nyingine hakutimiza Masharti!
Duuuuuuuu ebwanae hiyo nayo kali. Sasa kama waingereza walimtayarisha na yeye alikuwa anatekeleza matakwa yao mbona tunabiwa au kusoma ktk historia kuwa kna wakati hao waingereza walimfungulia mashtaka kuwa anaenda kinyume na sheria zao? Yaani kuwa alikuwa anaupinga utawala wa wazungu? Na kes iliendendeshwa na Mwalimu alionekana ana hatia? Ilibibid watu wachangishe hela kulipa mahakamani ili Mwalimu asifungwe jela? Je hyo nay tunadanganywa? Inawezekana vp watu waliokuwa wanamuandaa wamfungulie mashtaka na kumtia hatian? Kisha wazalendo wa tanganyika wachangishane kumlipia ili asifungwe?