Mwl Julius K Nyerere: Anakumbukwa kwa lipi? na analaumiwa kwa lipi kama baba wa Taifa

Unapomjadili mtu, unajadili anakula nini? anavaa nini? anapenda kinywaji gani n.k, na unakuwa unajenga interpersonal conflicts ambazo zina reside kwenye akili na kunyima uhuru wa fikra kujadili mambo ya kimsingi. Tusijenge mitazamo ya kinafsi bali tujenge mitazamo ya kisomi inayolenga kuleta mapambazuko ya kifikra katika jamii. Tumkumbuke Nyerere kwa kutazama imani na mitazamo inayolenga kuibua fikra za kimaendeleo na sio misuguano ya kibaguzi inayolenga kusambaratisha jamii.
 
Ni kweli mkuu hata mmi sipingi mchakato "halali" mtakatifu nyerere amelifanyia mengi sana kanisa alipokuwa rais wa tanganyika. so he deserve the title.

Mkuu! Mara nyingi sipendi ku-prejudge mtu lakini naomba radhi kwa hili: Kuna kitu kinakusumbua? Intrapersonal Conflict, na hili litakusumbua sana ukiwa utashindwa kushape emotion zako kwenye mambo ya msingi, sentensi zako zimeficha unafsi ambao hauendani na maneno uliyoandika na najua upo against. Ipo mitazamo ya kiimani inayokusumbua...you better learn how unaweza kuondokana na misuguano hiyo.
 
Mwacheni Apumzike Jamani kwa Neema...

Kwanini Msiwajadili hao Walio Hai? Au ni kama Kichuguu?

Tumejaa utata sana...walio hai wanavulunda tumekaa kimya tukiwapongeza. Tunahangaika na wafu. Akili ya aina gani hiyo??
 
Unapomjadili mtu, unajadili anakula nini? anavaa nini? anapenda kinywaji gani n.k, na unakuwa unajenga interpersonal conflicts ambazo zina reside kwenye akili na kunyima uhuru wa fikra kujadili mambo ya kimsingi. Tusijenge mitazamo ya kinafsi bali tujenge mitazamo ya kisomi inayolenga kuleta mapambazuko ya kifikra katika jamii. Tumkumbuke Nyerere kwa kutazama imani na mitazamo inayolenga kuibua fikra za kimaendeleo na sio misuguano ya kibaguzi inayolenga kusambaratisha jamii.

MBELWA Germano, asante sana kwa kuliona hilo. Siku hizi usomi wetu unatia shaka sana. Badala ya kutupeleka mbele, kila siku unaturudisha nyuma step kadhaa. Tuna matatizo mengi ya kufanyia kazi. Tunayaacha kama hayapo. Tunahangaika na mambo ambayo hatuna namna ya kuweza kuyabadili. Nyerere is gone hata tufanye nini. Kumtukana au kumpinga au kumtusi hakutabadili kitu chochote.
 
Last edited by a moderator:
Mapungufu:
- kukomalia kutumia kiswahili wakati hakitupeleki popote wa-tanzania

Mazuri:
- aliweza kuongoza nchi kwa muda
mrefu bila watu kuyumba kiuchumi

Nadhani hujakuwepo wakati huo, usingeyasema hayo kwani Nyerere ndiye aliyeuwa uchumi wa Tanzania, kang'atuka hatuna hata kandambili wacha mengine, Njaa mtindo mmoja mpaka tunaletewa unga wa msaada wa kula farasi ndio tugange njaa (unga wa yanga).

Pole sana kama ulikuwa huyajui hayo.
 
Tumejaa utata sana...walio hai wanavulunda tumekaa kimya tukiwapongeza. Tunahangaika na wafu. Akili ya aina gani hiyo??

Na Wapo Walioandika Kitabu Juu ya Mafanikio yao na kukitanganza Nchini na Nje ya Nchi yaani hadi USA; Sasa tunashindwa hata kukisoma hicho kijitabu na kukijadili, tunarukia ya J.K. Nyerere

Hii ni Chuki au ni ufinyu wa hekima zetu?

Nadhani hujakuwepo wakati huo, usingeyasema hayo kwani Nyerere ndiye aliyeuwa uchumi wa Tanzania, kang'atuka hatuna hata kandambili wacha mengine, Njaa mtindo mmoja mpaka tunaletewa unga wa msaada wa kula farasi ndio tugange njaa (unga wa yanga).

Pole sana kama ulikuwa huyajui hayo.

Kwa hiyo alipokufa ukapata ardhi kubwa ukalima maana inaonyesha alikuwa amehodhi hiyo ardhi na ukapata jembe uakalima na hiyo njaa ikaisha. Umejipambanua kuwepo enzi za uongozi wa Nyerere lakini argument yako ni kama kijana aliyepitia shule za vodafasta aliyejawa na internal conflicts maana anafikiri shida zake zimetokana na waliokufa. Waache wafu wawazike wafu wao na let us be positive in argument. When you argue let your factors be rational and theoretical and not immotional and pragmatical
 
Wakuu habari,

Nikifuatilia minadala mbalimbali haya uhusuyo Muungano au maendeleo na umaskini wa Mtanzania huwezi kutaja bila kumuhusisha Nyerere.

Atakumbukwa kwa kuwapendelea wakristo na kuwanyanyasa waislam

.[NECTA MACHINJIO YA WAISLAM]
 
Kwa hiyo alipokufa ukapata ardhi kubwa ukalima maana inaonyesha alikuwa amehodhi hiyo ardhi na ukapata jembe uakalima na hiyo njaa ikaisha. Umejipambanua kuwepo enzi za uongozi wa Nyerere lakini argument yako ni kama kijana aliyepitia shule za vodafasta aliyejawa na internal conflicts maana anafikiri shida zake zimetokana na waliokufa. Waache wafu wawazike wafu wao na let us be positive in argument. When you argue let your factors be rational and theoretical and not immotional and pragmatical

Kama ulikuwepo, alipokuwepo ardhi ya kulima ilikuwa ya vijiji vya ujamaa, ambavyo havikuleta mafanikio yoyote. Na kabla ya kuja kwake kulikuwa kuna mashamba aliyoyataifisha yaliyokuwa bora katika Afrika, Mkonge ulikuwa namba katika dunia. Kauwa kila kitu.

Kwa sasa aaah, nna kijishamba changu (sio cha kijiji) nnalima na kufuga nipendavyo. Na juzi kilimo kwanza nakuja kulazimishwa nipewe tractor kwa mkopo bila riba. Na wataalam wa kilomo kila wiki mbili wanapitia mara moja, bure bilashi wa serikali. Yalikuwepo hayo wakati wa Nyerere? subutu.
 
Ndie alie ifikisha nchi hapa.i hate him,katiba mbovu na upumbavu mwingine,japo hakuwa mwizi hicho ndicho kinampa heshima,lakin kavuruga sana future yetu vijana.
Kweli wewe Ni Mangungo, yule Mpumbavu aliyeuza nchi kwa kubadilisha shanga! Nyerere atabaki kuwa Nyerere hata kama hamtaki wapuuzi wachache. Kaa kimya!
 
Kweli wewe Ni Mangungo, yule Mpumbavu aliyeuza nchi kwa kubadilisha shanga! Nyerere atabaki kuwa Nyerere hata kama hamtaki wapuuzi wachache. Kaa kimya!

Tunasikia kaburi liliwaka moto, alipozikwa tu, tujuze ni kweli?
 
Tunasikia kaburi liliwaka moto, alipozikwa tu, tujuze ni kweli?

zomba una mambo wewe! Kaburi likawaka moto kweli? kwa hiyo ndio maana maziko yalikuwa binafsi kwa kuwa maziko ya kitaifa yaliishia pale Uwanja wa Taifa? Mkuu lakini Nyerere aliitendea haki Tanzania; elimu bure, umoja wa kitaifa, heshima duniani, nk.
 
Hakuna cha bure, alitowa wapi hizo fedha za bure? ni kodi yetu. Umoja ulikuwepo hata kabla yake, fikiri, Yeye Mzanaki, Dar kawakuta Wamanyema, Wamakonde, Wanyamwezi, Wangoni, Wanyasa, Wazaramo, Waarabu, Wahindi na wakampokea na hiyo ilikuwa kwa Tanganyika yote, mshikamano na umoja hakuna kubaguana hata kidogo. Yeye Hakuna alichokileta ila kufarakanisha watu. Hata neno "mdini" alilizuwa yeye kwa Sheikh Suleiman Takadiri. Huyo bwana wasiomjuwa ndio wanadanganywa, tuliokuwepo enzi zake, na tulioona hii nchi kaikuta vipi hawezi kutudanganya mtu.
 
Kuna mtu alokuwa Mdini kama Takadir? waulize kina Mwapachu, Sykes na wengineo watakwambia huyu babu alikuwa udini kila kitu yaani hata kula na mkristu sahani moja alikuwa hawezi.. Acha hizo kaka...
 
Kuna mtu alokuwa Mdini kama Takadir? waulize kina Mwapachu, Sykes na wengineo watakwambia huyu babu alikuwa udini kila kitu yaani hata kula na mkristu sahani moja alikuwa hawezi.. Acha hizo kaka...

Hakuna kitu kama hicho. Huyo alimwambia Nyerere ukweli mbele ya halaiki ya watu, matokeo, akaja kumrundika jela.

Hivi kuna Sheikh wa zamani ambae hajawahi kuwekwa ndani na Nyerere? kama si ubaguzi wa kidini wa Nyerere ni nini huo?
 
Kuna mtu alokuwa Mdini kama Takadir? waulize kina Mwapachu, Sykes na wengineo watakwambia huyu babu alikuwa udini kila kitu yaani hata kula na mkristu sahani moja alikuwa hawezi.. Acha hizo kaka...

On February 25, 1965, Nyerere banned the Muslim Education Union which was founded to train Muslims who were not allowed into the government primary schools. He also banned the EAMWS in 1968 with following short statement:

The Minister of Home Affair has by command of the President (Julius Nyerere) declared the Tanzania Branch of the East African Muslims Welfare Society (EAMWS) and Tanzania Council of the East African Muslim Welfare Society to be unlawful societies under the provisions of section 6(1) of the Societies Ordinance. (The Standard, December 20, 1968).
 
Ndie alie ifikisha nchi hapa.i hate him,katiba mbovu na upumbavu mwingine,japo hakuwa mwizi hicho ndicho kinampa heshima,lakin kavuruga sana future yetu vijana.

Kijana unayetegemea serikali ujue tu kuwa huna future. Somalia wana zaidi ya miongo miwili sasa hawajui serikali na vijana wapo tena wenye matumaini ya future. Ulisikia au kuona timu yao ya taifa ya mpira wa miguu katika mazingira yasiyo na serikali. Tena katika hali ya vita wanayo ligi ya taifa. Wangekuwa kama wewe sijui ingekuwaje. Wewe unayengojea serikali ikutengenezee future, umekufa ungali hai. Jihuishe kijana kama kweli unataka future vinginevyo kweli itakuwa future yako imetangulia kaburini pamoja na mwalimu.
Wenzio wanapiga hatua katika kusaka maendeleo wewe unamlaumu mtu aliyefariki. Umeachwa. Lazima uwajibike kwa maisha yako mweyewe. Serikali ikiwa upande wako kukusaidia sawa lakini hata isipokuwepo pambana usonge mbele kama kweli wewe ni kijana. Usisingizie wazazi (wapo au hawapo) wala serikali, ni wajibu wako tena wako peke yako kujitengenezea (future yako) mustakabali wako.
 
Back
Top Bottom