Mwisho wa wiki mgumu na mchungu Tanzania

Lions Share

Member
Jul 14, 2012
91
203
Tarehe 30/04/2022 Jumamosi Kariakoo Derby Yanga Vs Simba baada ya DK 90 Kuna watu watalia na kusaga meno, mikeka itachanika, ndoa zitaingia Kizungumkuti na hata like tendo siku hii huenda baadhi litapoteza ladha, wengine watafilisika na mwisho kwa bahati mbaya wengine wanaweza kupoteza uhai kwa mshtuko wa matokeo (Mungu aepushie Mbali).

Tarehe 01/05/2022 siku ya Jumapili hii siku hii ni Mei Mosi. Hapa ni mtanange kati ya Watumishi wa Umma Vs. Rais Samia Suluhu. Hapa sasa ni kimbembe timu hii ya Watumishi wa Umma itakua inaongozwa na walimu hii mechi nayo inasubiriwa kwa hamu sana, katika mechi hii watu wataingia wakiwa na kipigo cha Jumamosi sasa hapa ndio wanaenda kumaliziwa kabisa na kuanza kujiuliza kama ni ndoto au kweli.

Baada ya hotuba kuna mawili kukidhi matarajio au kutokidhi. Hotuba iki kidhi matarajio basi wikiendi huenda ikaisha murua na watu wakasahau vipigo vya Derby ya Kakoo lakini Hotuba isipokidhi matarajio yao baada ya kusikia "Vita ya Ukraine inajulikana ilichofanyia uchumi wa dunia tusubiri uchumi uimarike" aina haja ya Kuongea sana Limeisha tusubiri Mwakani 2023.

Ikisikika hivi yawezekana Watumishi wengi waloingia na Mabango uwanjani yataanza kuwa mazito watayaacha na kuyatupa chini walio majumbani watapiga Remote za TV chini watavunja TV watajawa na Makasiriko. Kitachofata ni presure, stres, kuacha kazi, ndoa kuvunjika, makasiriko bila sababu, watoto kuchapwa ovyo, moraly ya Kazi kuisha kabisa maana ilishashuka kitambo, kufukuzwa kazi na mwisho kabisa vifo sababu ya Mshtuko (Ili atuliombei mungu aepushe mbali) na J3 Asilimia 40 ya watumishi hawataingia Ofisini hadi baada ya Eid ili kupoza machungu.
 
Aisee...wacha kwanza tuteteme hiyo jumamosi halafu ndiyo tusubiri hiyo may day
FB_IMG_1650146145991.jpg
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom