...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!




Ben Saanane

Hongera kwa kutoka hadharani na nina imani kuwa leo utakua na ujasiri wa kukaa hapa na kujibu hoja zaidi ya kukimbia na pengine ukaingia na silaha za msituni(ID fake)

Hoja yangu nilianza kuijengea juuu ya msingi wa kilichoripotiwa na vyombo vya habari na pia baada ya kuona Tweets malalamiko mengi ya wazee dhidi ya kauli hiyo zikiwamo Tweets za Mzee Reginald Mengi.

Nadhani hizi tuhuma za 'Mwisho wa UONGO NI AIBU' zinafaa kukurudia maana ungekua mkweli ungeweka video yote.Je kuweka video ya Youtube hapa inatosha?Ni kitu gani kitakachothibitisha kuwa hii video haijawa Edited na kuondolewa vipande ambavyo ni awkward ikiwemo hiyo kauli 'Wazee wanaosubiri kufa Kesho'?Tangu tuhuma hizi zilipoibuka ni siku nyingi zimepita sasa hiyo video ulikua ukiifanyia nini?

Kama ulisoma post yangu vizuri uliona kwamba nilianza kuamini kilichoripotiwa kutokana na rekodi ya matamshi yako ya kibaguzi na mengine ya kukurupuka.Historia ndiyo inayokuhukumu.Rekodi zako ndizo zinazokuhukumu.

Hapa hapa umekurupuka na kudai tunatumwa bila uthibitisho wowote.Nadhani sasa title ya hii thread yako inakufaa maana unasema uongo hadharani bila kujali nafasi yako katika jamii.Hii inathibitisha ulaghai katika mambo unayofanya na hata hii video itakua na chembe za ulaghai kama vile kufanyiwa 'Editing' maana kama katika post hii tu umedanganya,ni mangapi utakua umedanganya?Post yangu ya jana ilikua hivi



''Nimesikitishwa sana na kauli iliyonukuliwa kutolewa na Nape Nnauye(Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM).


Gazeti la MAWIO la tarehe 8/8/2013 toleo namba 055 ukurasa wa 5 lililikua na kichwa cha habari NAPE NA CCM 'Ni ama Aiue Ama Imuue'

Katika kauli zake nyingi zilizokosa umakini Kwanza kama mwanasiasa Kijana(Namaanisha Muonekano yaani Physical appearance bila kujali weledi wa kifikra) na Pia kama Mwanasiasa msomi mwenye Taaluma ya diplomasia,Taaluma ya Uandishi wa Habari(Kutoka Chuo kikuu cha Acharya maana Syllabus yao naifahamu na ilihusisha somo la saikolojia) na pia kama msomi wa shahada ya uzamili aliyemudu kuandika Tasnifu(Thesis) na ikapitishwa na Maprofesa hakupaswa kutoa kauli hizo ikiwemo kauli hii iliyokera sana, kwamba Wajumbe wa Tume ya Katiba wanaounga mkono serikali 3 ni wazee na wanasubiri kufa.

Hii ni kauli ya kipuuzi kabisa na inadhalilisha taaluma zote nilizotaja hapo juu na weledi anaopaswa kuwa nao.Kauli hii haidhalilishi taaluma tu,bali hata Mwenyekiti wake aambaye ametimiza miaka zaidi ya 60.Kauli hii inawadhalilisha viongozi na wanachama wote wa chama chake na serikali waliovuka umri wa ujana kwa mujibu wa sheria zinazotambulika na vigezo vyote vya kinadharia.Zaidi Kauli hii inatudhalilisha vijana maana hata sisi ipo siku tutakuja kuwa wazee.Sasa kauli hii inaweza kutumika dhidi yetu kwamba tukipewa mamlaka tunaweza kuharibu kama waliopewa ridhaa na vyama vyao bila kujali itikadi wanaweza kuwa na mtazamo wa aina hii.Ni kauli mbaya na ya kibaguzi

Kumbe Kauli ya Kumuita Dr.Slaa Babu ,Haikumaanisha kauli ya kipinzani?Nakumbuka Dr.Slaa aliwaambia Wanachama wa CHASO(Taasisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni Wafuasi wa CHADEMA) kuwa akiitwa Babu ni heshima kubwa kwake maana uzee unaashiria hekima na busara.Lakini sasa kauli za Nape kumbe zililenga ubaguzi dhidi ya wazee na sio kwa nia njema.Kumbe Nape nnauye anapomtazama Mwenyekiti wake,Katibu mkuu wake,Makamu mwenyekiti wake,waziri mkuu,Makamu Wa Rais,Spika Wa bunge anaona kwamba hao wote wanasubiri kufa?Anawaona wazee Salim Ahmed Salim,Mzee Waryoba na Mzee Lowassa kwa jicho hilolo hilo mana suala hapa sasa limekua umri aidha unaunga mkono serikali 2 au unapinga.Ni jambo la ajabu kuwa Nape alituhumiwa kushiriki kuasisi CCJ,huku akijua washirika wenzake waliotajwa yaani Mzee Samweli Sitta ni mzee na hivyo anasubiri Kufa pengine yeye akifikiria kuwa atakua na fursa muhimu ya ku-takeover chama cha CCJ?Yaani Mwenzako anawaza huyu nipo nae leo lakini "Anasubiri kufa Kesho"?Unafiki huu haufai hata kidogo.

Kauli hii ni ya kulaaniwa na vijana wote bila kujali itikadi zetu za kidini na kisiasa.Mwanzoni niliposikia kauli hii niliona tweets za Mzee Reginald Mengi akitoa ushauri wa busara kwa Nape na kumuonya kuwa ‘Yeye(Nape) Sio Mungu'.Mlolongo wa kauli za kukurupuka ulioanishwa leo hasa ule wa kuwapa mafisadi siku 90 za kujivua Gamba,kauli hii dhidi ya wazee nami naongeza/nakumbushia Kauli ile nyingine ya kuwa 'Wachagga sio watu wa kujichanganya nao'(akilenga rhetorics za Ubaguzi dhidi ya CHADEMA ) bila kujali kuwa ndani ya CCM kuna viongozi na pia serikali ya chama chake ina Mawaziri ambao wana asili ya uchagani na ama wameoa au kuolewa na wachagga ni ulimbukeni.

Kijana yeyote katika jamii iliyostaarabika mwenye ujasiri wa kuwatukana wazazi na hata wakwe zake kwamba 'Ni wazee wanaosubiri kufa' anazua maswali mengi.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM anapotangaza maneno hayo inamaanisha kuwa anaeneza sera za chama chake kilichounda serikali inayoshindwa kuwalipa wazee wa Afrika Mashariki kwa sababu tu ya dhana na fikra potofu kuwa ni 'Wazee wanaosubiri Kufa Kesho'
? Bila shaka kama sio msimamo wa chama chake basi Madaraka aliyopewa ni makubwa sana kwake

Wazee ni tunu inayopaswa kuheshimika.Kupitia Itikadi zetu tujifunze kushinikiza kupitia ujana wetu kuhakikisha vyama vyetu vinatunga sera zinazoheshimu wazee.Kwa kufanya hivi tutakua tumejenga utamaduni na misingi inayoheshimu wazee
Nape Nnauye atoke hadharani sasa kueleza alichomaanisha kuhusu kauli hii na hayo mengine yaliyonukuliwa.Asipofanya hivi,vijana tumuhesabu kama msaliti wa vijana na tujitenge na kauli hii aliyoitoa.Kama kweli alisema,Labda pengine msimamo huu ni wa chama chake ambacho naamini kuwa vijana wanaoheshimu wazee hawataiunga mkono.

Msomi Mzuri ni Yule anayechagua cha kuongea,Mwanasiasa mzuri ni Yule anayechagua maneno.Kijana mzuri na makini ni Yule anayeheshimu tunu za uzee bila kushinikizwa na itikadi au mazingira yoyote.Binadamu mzuri ni Yule anayeheshimu uhai wa mwenzake.Binadamu mstaarabu ni Yule anayeheshimu mamlaka ya kiroho na pia anayeheshimu katika falsafa ya ‘Law of Nature'.''



CC: Paw , PainKiller , Fang , bachanan
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ziweke vizuri hizo link na youtube hazieleweki
 
Njoo na takwimu zenye kueleweka..sasa hicho ndio nini!!
 
Umejitahidi kuweka link vizuri lakin naskia makelele tu hakuna kinachosikika....
 
'ikulu siyo wodi ya wagonjwa', 'kwani hamuwaoni wagonjwa mahututi wanaotafuta urais mpaka makanisani'

nukuu kutoka kwa Nape ziarani Mara

chanzo:Mawio
 
Nape nilitegemea wewe kama Kiongozi utajutia kauli ulizotoa. Waliokuwekea kauli zako wamesahau hii ya siku za hivi karibuni uliyosema wenye akili timamu ni wale wanaosimamia msimamo wa serikali mbili, ikiwa na maana kuwa wasio waumini wa msimamo huo hawana akili timamu.

Rasimu ya Katiba imeletwa tujadili wote kwa kuheshimu uhuru wa mawazo. Wewe unasema sisi tusiounga mkono hoja za CCM hatuna akili timamu. Nilitegemea hili unalielewa hata baada ya kujadiliwa na vyombo vya habari na mitandao, kukomaa kwako kwa jambo hili sikuungi mkono.

Kila tamko lina gharama, lakini sisi tunakuambia kwenye mitandao tu. Subiri wazee kama watakuelewa au watanzania wengine watakaotafsiri kauli zako.
 
Haiwezekani kwenye mkutano mtu akazungumza within 11 minutes, hii video imechakachuliwa.

Kingine kinachonyesha video hii imechakachuliwa haijaanzia mwanzo wala haina mwisho ina maana mtu anaanza tuu kuongea from no where hakuna hata kuwasalimia wananchi hakuna?

Halafu unamaliza kuongea hata hakuna kuwashukuru wananchi? uongo mwingine mjipange kabla ya kupost


Na mwisho uombe msamaha kwa kuandika jina la mtu kwa kejeli
 
Hiyo clip ina dakika 11 tu
Haijaanzia mwanzo alipoanza kuogea,haionyeshi maneno yake ya mwisho wake akihitimisha,
The video is not proved not to be eddited
hatujaona ushahidi wowote wa aliepost na alierekodi kuonyesha haijafanyiwa edditing,
In that reason waandishi na wahariri wa magazeti mawili tofauti kukaa chini kutunga habari na kuandika habari zinazofanana sio rahisi
Hatujaona mlengwa akikiwaandikia demand note wahariri hao kukanusha kauli yake kama alivonukuliwa
Hatujaona hadhira aliyowahubiria nape wakikanusha hii habari hukutamka haya maneno dhidi ya wazee wetu.
Bado nasisitiza video iliowekwa hapa ni fake,it is modified to clear nape,
bora angekaa kimya...
Tutaitafuta clip nzima na suppoting evidences tutaziweka hapa jf.time will tell
 
hebu twambie kwa kuandika uliongea nini kuhusu wazee? maana hata link haieleweko zaidi ya kelele tupu.

Ina maana hukusema kuhusu wazee wetu?
 
Nape, kwangu mimi nakuona kama umepwaya mno kwenye kiti ulichopewa cha itikadi na uenezi. Hakika kwa kijana kama wewe kuwa unatoa threads kama hizi mitandaoni nakuona licha ya kupwaya kwenye kiti pia una tatizo la ufahamu wa siasa hasa za kisayansi!!
 
Nape haishii tu kumwita Dr. Slaa kibabu kwamba hana faida na asisikilizwe, amenukuliwa "wazee wanaopendekeza serikali 3 wanasumbuliwa na uzee na wanasubiri kufa", 'kama ni wanaccm ni oil chafu'

chanzo:Mawio

My Take:kama ni kweli
nape hana wazazi?
hana heshima na anajitabiria kifo ujanani na kutoufikia uzee
 
Kwisha ccm ...baba yangu ameapa kurudi ccm kwa ajiri ya vijana waharibifu kama wewe na nchemba
 
Kwa Ben Saatisa, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!



Hivi nape unadhani watu wanavyoibeza ccm ni nini sababu au mnaonewa...kutakuwa sehemu mmekosea sasa mlivyokuwa sikio la kufa hata miguno y andani kwenu (ccm ) hamsikii
 
Last edited by a moderator:
Makamanda wa Chadema wanaoinyima usingizi ccm wanazidi kuongezeka. Ben Saanane naye kumbe ni tishio mtaa wa lumumba. Sasa makamanda tuongeze kasi ya mashambulizi kwakuwa ccm inakaribia kuachana mwili na roho.
Dkt. Slaa na Kamanda Mbowe endeleeni na kazi hiyo hiyo nzuri ya kuwapika kiukomavu vijana wengi zaidi ili kazi yetu ipate kuwa ya uhakika na nyepesi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Haiwezekani kwenye mkutano mtu akazungumza within 11 minutes, hii video imechakachuliwa.

Kingine kinachonyesha video hii imechakachuliwa haijaanzia mwanzo wala haina mwisho ina maana mtu anaanza tuu kuongea from no where hakuna hata kuwasalimia wananchi?

Halafu unamaliza kuongea hata hakuna kuwashukuru wananchi?

Na mwisho uombe msamaha kwa kuandika jina la mtu kwa kejeli
Kama wewe unajua imechakachuliwa, lete ya kwako ambayo haijachakachuliwa tuione.

Jenga hoja kwa evidence na siyo mihemko ya kibavicha.

Hizi kelele unazopiga ni kelele za debe tupu. Huoni huyo aliyeleta uwongo kuhusiana na hili swala ameamua kufunga thread yake haraka na kuukimbia uongo wake.
 
Back
Top Bottom