Hivi Idd Simba yupo wapi?, Jamaa alikuwa na sera ya Uzawa wakamuona mbaguzi, ila alikuwa anaona mbali sana. Nchi zote makini hukaribisha wageni kwa lengo la kuingiza mitaji nchini kwao na kukuza uchumi, sisi Tanzania tunakaribisha wageni waje kuchuma na kwenda ku-invest Canada, UK et al. Hakuna suala la ubaguzi hapa, kama mgeni anaishi kwa taratibu na sheria za nchi, yaani haliibii taifa kwa kushirikiana na wanasiasa wasio wazalendo, hatoi rushwa, hakwepi kodi basi ana haki ya kulindwa kwa nguvu zote na sheria. Ila kama ni wachumaji tu na kutoroshea nje ya nchi mtaji anaoupata badala ya ku-invest Tanzania basi hafai hata kidogo. Leo hii CCM wanahaha kutafuta wachawi kwa kuchukiwa na wananchi, lakini wamesahau kuwa kwa wao kukumbatia wageni kwa kuwa wananchangia chama kunawafanya hawa jamaa kuwa na kiburi cha kuvunja sheria kwa kuwa tu wananchangia chama.
Tuwaambie kabisa kuwa wanakarishwa Tanzania na watalindwa kwa sharti la kudumisha utamaduni na uchumi wa nchi hii. Kwanza ni lazima wajifunze kiswahili, yaani kama muhindi anaomba uraia sharti la kwanza liwe anajua kiswahili, halafu ni lazima wawe inclusive siyo wanajitenga maeneo fulani kama vile wapo nchini kwao. Iwekwe sheria kuwa mfanyabiashara yeyote wa kigeni ni lazima awe na mali isiyohamishika, (i.e nyumba) NHC itoe morgage kwa hawa watu kwenye nyumba wanazojenga na zile za kupangisha ziwe za watu wenye vipato vya chini tu. Tusipoangalia tutabakia na mabua, hawa si watu wazuri kabisa. Wapo wahindi wazalendo ambao kweli wanauchungu na Tanzania kuliko mmbatumbi ila tuwatumie hawa kuwaelimisha wenzao kuwa nchi hii si shamba la bibi, kama wanakuja kutafutia mtaji hapa na kwenda ku-invest nchi nyingine basi hawafai.
Kigezo cha kwanza cha kupata uraia kiwe kaja Tanzania na nini?, siyo anaingia na briefcase yenye pants anaondoka na briefcase yenye USD.