Mwinyi: Sikuishutumu awamu ya nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwinyi: Sikuishutumu awamu ya nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  RAIS mstaafu wa awamu ya pili, mzee Ali Hassani Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa amesema kuwa hakuikandia serikali ya awamu ya nne wala kuihusisha na kukithiri kwa rushwa kwa kuwa rushwa ilianza tangu zamani.

  Mzee Ruksa alisema hayo Ijumaa iliyopita alipozungungumza na wahariri wa gazeti hili nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam kufafanua alichozungumza katika mahafali ya 12 ya Chuo cha Teknologia ya Habari (IIT) alikoalikwa kama mgeni rasmi.


  Mzee Mwinyi alisisitiza kwamba; alipotangaza zama za ruksa, takribani miongo miwili iliyopita hakuruhusu rushwa iwemo katika zama hizo, lakini wajanja wachache wasiokuwa na mapenzi mema na taifa waliingiza tafsiri zao na kutumia vibaya nafasi hiyo.


  "Wakati ule (alipotangaza) ruksa kwa uhakika kabisa suala rushwa halikuwa miongoni mwa mambo yaliyoingia katika azma hiyo. Wabinafsi wachache wasiokuwa na mapenzi mema na nchi hii waliitumia ruksa hiyo vibaya. Ni lazima wakomeshwe, tuseme inatosha na lazima tushinde vita hivi," alisema Mzee Ruksa.


  Aliwataka Watanzania wazalendo walioshikilia nafasi zozote na popote walipo kujiunga katika mapambano dhidi ya rushwa, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, wafikirie juu ya Watanzania wenzao walioathiriwa na umasikini na kuwasaidia kuondokana na madhila hayo.


  "Kuweni wazalendo kwa mustakabali wa vizazi vijavyo. Kuweni jasiri, pigeni kelele mkiweza. Neno litakaloongoza maisha yenu liwe uadilifu," alisema Mzee Mwinyi.


  Aliwataka Watanzania kuwa raia wema na wawajibikaji wanaoipenda nchi yao na walio tayari kwa njia yoyote kuijenga nchi bila kuingiza ubinafsi.


  "Nina uhakika juu ya mapambano yanayoendelea dhidi ya rushwa nchini Tanzania. Kwa muda sasa wananchi wetu wamekuwa wakilalamika maafisa wa serikali kuwaomba rushwa ili maafisa hao watekeleze wajibu wao. Inaonekana utamaduni wa rushwa unaota miziz taratibu katika jamii yetu," alisema.


  Alisema kuwa fedha zilizokuwa zimelengwa kujenga shule, hospitali, vituo vya afya barabara na miradi mingine zinaliwa na watu wachache kwa ulafi tu, jambo ambalo alitaka lisivumiliwe na likabiliwe hadi ihakikishwe limetokomea.


  Akifafanua alichaosema katika mahafali hayo, Mzee Mwinyi alisema: "Mimi ni mtu mzima sina ‘ambition’ (matarajio) yoyote kisiasa na hata kwa namna yoyote ile, nimelitumikia taifa hili kwa nafasi mbalimbali nimemaliza muda wangu sasa hivi nimestaafu kwa maana hiyo mimi si tishio kwa mtu yeyote awe mfanyakazi, kwa nafasi ya kisiasa, wala sitegemei kuomba kazi yoyote.


  "Mimi nilialikwa katika mahafali na kuwapa tuzo waliofanya vizuri katika masomo yao na niliyoyasema kule ni mamneno ya kuwatia nguvu, kuwaasa na kuwapa dira njema ya maisha yao, sikuwa na madhumuni mengine.


  “Niliwaambia kuwa wame mstari wa mbele kupigana na rushwa ambayo ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya taifa letu, hivyo tuweke nia na kuelekeza nguvu zetu katika kupambana nayo”.


  Mwinyi: Sikuishutumu awamu ya nne
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee tunamuheshimu asianze kubadili badili maneno hana sababu ya kuogopa kwani alichosema ni uongo?

  Japo ni kweli wakati wake wale wajinga wote tuliowashinda shuleni ndio walikua wanapeta nchi hii, bado rekodi ya Mkapa kwenye kurekebisha uchumi ni kiboko, ni pale tu alipoingizwa na RA kwenye ufisadi otherwise mzee huyu alishaandika historia nzuri sana duniani
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ameshatembelewa.... walijaribu haya kwa Nyerere walishindwa someni "UWHT"...
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama nimemuelewa huyu basi mnitwange risasi. Huyu mtu hatenganishi black and white, kwake ni all grey! Hakuna anayesema ufisadi umeanzia kwa JK, lakini umekithiri katika kipindi chake -- na hasa jinsi JK alivyokuwa mwoga kuishughulikia kikamilifu kwa sababu ya kulindana.

  Na Mwinyi anaposema yeye sio tishio kwa mtu yoyote kwani hawanii nafasi yoyote ya kisiasa haina maana yoyote iwapo hawezi kutumia nafasi hiyo muafaka kuukosoa ufisadi uliyokithiri nchini - without mincing words! Every leader in CCM, past and present are becoming mere fools when the question of ufisadi is raised! They always develop rubbery legs! All talk in the same lingo! it enrages, it really does.

  Who then, in CCM, is going to salvage the ship from the blind sailors?
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naamini Mwinyi ameanza kuandamwa kama akina Butiku.JK na wapambe wake hawataki kusikia criticism ya aina yoyote ile.

  Sent from my HTC Desire using Tapatalk
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nidhamu ya uoga na kutojiamini. Basi ni bora awe anafunga mdomo wake.
  Au anaogopa makofi!.
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji UWHT ndi nini? naomba ufafanuzi tafadhali
   
 8. B

  Bobby JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kweli ashauriwe afunge mdomo wake aendelee kula pensheni yake tunayomlipa otherwise asitutafute watu ubaya bure jamani.

  Eti rushwa ilianza siku nyingi so ianchwe tu iendelee kuwatesa watanzania huu kama si upuuzi ni nini? jk alipokuwa criticized na wazee fulani nakumbuka alisema hivi, nakuu "Hawa wazee nawashangaa sana kwani hata awamu zao walifanya makosa" mwisho wa kunukuu.

  OMG my God nilitamani kuipinga ngumi luninga yangu sikutarajia kusikia maneno hayo kutoka kwa rais "tumani lililorejea" So Mr. president kwa kuwa awamu zilizopita zilifanya makosa ndio maana na wewe unaendelea kufanya makosa tena yale yale?

  Kwa kuwa awamu nyingine zilikuwa na rushwa na wewe umeamua kuichekea rushwa mpaka mizaha mbele ya maaskofu? Do you know kwamba gharama ya kuendela kufanya makosa yaliyofanywa huko nyuma ni upotevu wa maisha ya watanzania wasio na hatia?

  Please rejea maneno ya Baba wa Taifa "Tatizo la awamu hizi ni kwamba yale mabaya ya kuacha wao wanaendeleza na yale mazuri ya kuendeleza wao wanaacha kuyafanya" Tanzania nakupenda lakini zaidi nakuonea huruma kwani wewe ni zaidi ya mtoto yatima kwani watoto yatima wana orphanage centers, nadhani ipo haja ya kuwa na orphanage centers za nchi pia kwa ajili ya zile nchi zilizokosa wazazi kama yetu.
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sipendi kuisema hii... lakini kwa hasira nalazamika: Ndo maana alinaswa kibao! Ana maudhi sana.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wachumia tumboni dot com
   
 11. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania.

  MJ
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee ndio maana nilisema katika thread iliyopita bora akae kimya maana watamnasa vibao watu
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mimi nilishangaa kusikia kwamba ndiye kasema maneno yale. Kama aliyasema aliyasema kwa bahati mbaya maana yeye ndiye muhunzi wa serikali tuliyonayo. Ni matunda ya shule yake ya uongozi. Bila yeye nani angemjua huyu mkwere?
   
 14. M

  Mkono JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee anajua madhara ya kumkosoa mkuu wa nchi mnataka azushushiwe jambo,huku anahakika mwanaye kukabidhiwa ikulu kama si ile ya magogoni basi walau hata ile ya Zanzibar .Ninyi mnaolaum ni kwa kuwa hamjui ikilu nini.
   
 15. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sidhani!!
   
Loading...